Askofu Mstaafu aliweka Kanisa katika uangalizi

Texas,

ASKOFU Mstaafu wa Kusini Mashariki mwa India Kononkuratus Samwel ameliweka kanisa lake katika uangalizi alipotembelea Baraza la Maaskofu la Texas na kusema kanisa nchini India lilikuwa limechua hatua katika kukomesha umaskini, kwa kuangalia umuhimu wa wanawake na maendelo kwa vijana.

Naye Askofu Safrigan Leo Aladi amesemakuwa, Askofu Samweli ametoa zawadi yake kwa Mungu kwa kuwepo kwake katika sehemu hiyo.

"Amelileta Kanisa lake kwao na hivyo watu wajione kama kweli wao ni Kanisa moja katika misheni, iwe Texas au hata India Kusini." Alisema Askofu Leo

Mfano halisi wa picha ya misheni ni jamii ya makasisi katika Dayosisi ya Kilara Mashariki ambayo imeongezeka na kufikia 350 katika miaka 17 iliyopita.

"Hii ni sehemu yenye watu wengi ambao ni maskini na ambao hawajasoma na wasio na thamani katika jamii," alisema Askofu Samweli.

"...Umaskini ni adui mkubwa kwa Kanisa," alisisitiza

Akizungumzia ukuaji wa Kanisa, Askofu samweli alisema kuwa, wakulima wa chai waliojitenga mbali na jamii, mara nyingi wanafanya kazi za misituni na kujipatia fedha za matumizi yao kwa siku.

Aliongeza kuwa hao, huanzisha makanisa katika sehemu hizo lakini, wengi hushindwa kuelewa maana halisi ya Kanisa.

Alisema Dayosisi imeongezeka mara tatu toka 20,000 hadi 75,000 tangu mwaka 1987 na kuongezeka katika makanisa toka 80 hadi 175 ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa pamoja na waamini angalau 20,000 kila mwaka.

Mapema katika ziara yake Askofu Samweli, aliiambia Kamati ya Dunia ya Misheni kwamba, wameitwa katika jamii ili kuwa Kanisa moja.

Alisema ingawa kuna vishawishi vya hapa na pale, lakini wanao uwezo wa kuvipinga

Vatican yataka mauaji ya Kardinali Juan yachunguzwe upya

Vatican City

MAKAO Makuu ya Baba Mtakatifu, Vatican yameitaka Serikali ya Mexico kuchunguza upya mauaji ya Kardinali Juan Jesus Posadas Ocampo yaliyotokea mwaka 1993.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Vatican, Joaquin Navarro-Valls, imesema uchunguzi uliofanywa umeonesha kuwa Kardinali huyo ambaye ni M-mexico, aliuawa kwa njama zilizofanywa na viongozi wa ngazi za juu serikalini.

Taarifa hiyo imesema kuwa, uongozi wa Vatican una kila sababu ya kufungua upya kesi hiyo kutokana na kupata ushahidi wa kuthibitisha mauaji hayo.

Marehemu Kardinali Juan Jesus Posadas Ocampo aliuawa Mei 24, 1993 katika uwanja wa ndege wa Kimataifa na Guadalanjara nchini Mexico.