Pendo (3)

 

JIONI ya Jumapili hiyo tulikuwa tunapunga upepo chini ya mti uliokuwa mbele ya jumba letu la kifahari lililomalizika ujenzi hivi karibuni kama miezi miwili iliyopita, tulikuwa tumepanga na Ommy, ni wapi pangetufaa kwa matembezi siku hiyo iliyoonesha kila hali ya kustarehesha na kuchangamsha hata mtu akaifurahia dunia. Endelea na Mtunzi wetu mahili, ujue kulikoni mbele ya safari katika sehemu hii ya tatu ya simulizi.

Pia wapo ambao badala ya kunipunguzia matumizi, walizidi kunipa ahadi za njoo kesho huku wakijua dhahiri kuwa, hakuna nitakachoambulia.

Nilihangaika hadi Jumatatu iliyofuata Mungu aliponihurumia nilipojikuta nimefika ofisi za Idara ya Maliasali zilizoko barabara iendayo TAZARA toka Kariakoo.

Hapo, nikaambiwa ipo nafasi ya kusafisha vyoo na kwa siku wanalipa shilingi 300 hapo, nikajiona nimeukata kweli kweli. Nikaona maisha kwangu ndio kumekucha. Hivi Mungu anipe nini zaidi?!

Ingawa mimi nilifurahia kazi hiyo, nilianza kuiona kama mateso maana kila aliyeniona nikifanya kazi yangu, alikuwa na lake la kusema. Wengine wakawa wakiniambia, "Ramba mavi," nawengine wakiniita, " komba komba."

"Mwanangu! Riziki ni popote na hutoka kwa Mungu," aliniambia Mzee Mwaishima kila alipoona watu wananisonga songa kwa maneno hayo.

Mara nyingine alisema, 'Mjukuu wangu, usifanye hasira wala usidharau kazi aliyokupa Mwenyezi Mungu. Siku moja atakushushia baraka zaidi yao hao wanaokutambia sasa hivi.

Hawajui riziki hutoka kwa Mungu" niliamini maneno hayo na hata kukumbuka usemi usemao "Maisha ni mzunguko; leo kwangu na kesho kwa mwingine."

Nikaendelea na kibarua changu hicho kwa muda wa miezi minane nikaonekana mtoto mwenye tabia nzuri na busara kwa mabosi wangu .

Tabia hiyo ingeweza kuigwa kama si kutolewa mifano kwa watu na hata wasichana wengine walio na umri kama wangu.

Ni utendaji kazi wangu uliokuwa safi uliowafanya mabosi kunihamisha toka kitengo cha usafi wa vyoo, na kunipeleka katika ofisi zao kwa ajili ya kuanzia pale shughuli za ufagiaji na kupiga deki.

Nilikuwa nalipwa shilingi 700/= kwa mwezi na kwa jinsi nilivyokuwa, niliiona nazidi kuiona kazi ni nyepesi sana; tena isiyo na ugumu.

Nikaanza kubadilika hata ngozi na kuzidi kunawiri.

Kwa hali hiyo, nikaonekana kuzidi kuonesha uzuri niliojaliwa kuwa nao. Umbo langu ni zuri na shingo yangu ni nyembamba na ndefu yenye pingili pingili, mithili ya zile za mua. Macho manene yaliyofunikwa na nyusi nyeusi tii, nywele nyeusi, mguu wa mkubwa mithili ya chupa ya bia na rangi ya maji ya kunde kama wanavyoiita wajanja, ndivyo vilivyozidi kuibuka na kutesa kwangu.

Hata mabosi wangu walianza kunifuatilia na kubuni mbinu na mikakati mbalimbali ya kunirubuni ili nikiuke maadili ya Kimungu.

Kwa jinsi nilivyo kuwa nimependeza, hata wewe ambaye ni msichana kama mimi, ungenitama. Niliukumbuka usemi wa mzee yule Mwaishimo kwamba, riziki hutoka kwa Mungu.

Lakini, hata hao wakubwa wangu wa kazi, nilijaribu kuwakwepa kwa kila hali niliyoiweza kwani sikuona kuna sababu gani ya kuniwezesha kufanya kitu kama hicho na mabosi wangu.

Pili, tabia niliyokuwa nayo, ilikuwa ni kinga tosha ya kuniepusha katika vishawishi vibaya vinavyo hatarisha mahusiano yangu na Mungu, na hata pengine kuhatarisha maisha yangu.

Ilifika hatua hata wengine wakiwamo mabosi wangu na wafanyakazi wa ofisi jirani, wakafanya majaribio ya kunizuzua na vijizawadi vya shilingi elfu tanotano, au elfu kumikumi.

Nilijua dhahiri kuwa sikuwa pale kupewa elfu kumi bila kuzihangaikia kihalali maana najua sana sana, zingeweza kuhitishwa kwa kunitokea puani huku afya yangu ikibomoka na hadhi yangu, ingeakunguka mbele ya macho ya watu.

Licha ya mbinu mbalimbali zilizotumika kunitia mitegoni, hakuna iliyofanikiwa kuninasa na ikabidi wengine wachune nyuso zao na kunifuata uso kwa uso kuzungumza kunizungumzia juu suala hili zito.

Kila aliyenifuata kwa hoja hiyo, nilimjibu vizuri na tena kiungwana kabisa.

Hii iliyokana na ukweli kuwa nilijua wapo "wachafuzi wa mazingira" na wengine wapo wanaotafuta "karata isiyo galasha" waliyotayarishiwa na Mungu .

Nikajua huenda, na mimi hapo hapo ipo yangu.

Watu wa namna hiyo kuwajibu kwa ghadhabu au karaha, ingekuwa ni sawa na kuwatukana wakunga wakati bado uzazi ungali upo.

Siku moja nikiwa njiani kuelekea nyumbani toka kibaruani, mara nikavamiwa na kupigwa na butwaa nilipoliona gari lile linasimama mbele yangu.

Kabla ya lingine

lolote kufanyika, sauti ikatoka ikisalimia,

"Anti habari yako." Kabla ya kumjibu, nilianza kujiuliza na kutafakari ni vipi dereva aendeshe rafu namna hii na hata ashikie breki mbele yangu namna hiyo "Panda ndani ya gari nikusindikize basi huko uendako" "Asante. Nashukuru sana," nilisema na kuongeza huku nikifafanua, "Samahani Anko usinielewe vibaya. Nashukuru nitafika tu."

Dereva huyo kijana wa umri wa kati, hakuridhika na majibu yangu. Akateremka na kunisogelea, ' "Nielewe anti mimi nimpenda nikupe usafiri mpaka uendako. Nimejisikia mwenyewe kufanya hivyo." Sikutaka niendelee kuongea nae zaidi. Nikaondoka zangu na kumuacha ameduwaa huku akinisindikiza kwa macho yaliyoashiria kitu fulani.

Siku ya pili wakati nakaribia ile nyumba kubwa niliyokuwa naishi nikitoka kazini, mara naiona gari ikitokea upande wangu wa kushoto kwa mwendo wa taratibu.

Nilijua labda mwenye gari hilo kuna nyumba ana jaribu kuiangalia kwa makini au labda ameisahau.

Kadri ilivyokuwa inakaribia jirani nami, ndivyo kumbukumbu yake ilivyozidi kunirejea.

Nikatambua mara moja kuwa, ni ile ile gari niliyoiona jana pindi natoka kibaruani na dereva ni yule yule. Kwa mwendo wa haraka, nikazipanda zile ngazi chapuchapu na kuingia ndani kiasi kwamba, yeyote ambaye ningemkuta mle ndani lazima angedhani nafukuzwa na mnyama mkali, labda simba.

Baada ya kuingia chumbani nilijiandaa kuingia bafuni, "Dada Pendo!" "Bee!" nilisikia sauti ya mpangaji mwenzanguikiniita, nami nikaitika huku ni nilielekea huko sebuleni.

Nilipogonganisha macho yangu na ya Rozi, alitabasamu na kisha kuniambia, "Kuna mgeni wako hapa." "Mgeni wangu toka wapi?" Nikauliza kwa hali ya mshangao. Nilipomuona tu, nikamtambua kuwa ni yule niliyemuacha hapo nje akiwa ndani ya gari hisia zikanijia za uoga. "Hivi huyu kaka amesahau nini kwangu! Hawa ndio wachuna ngozi, tangu jana ananifuata fuata!" nilijisemea kimoyo moyo.

"Mh! Lakini alivyokuwa nadhifu, alionekana mtanashati mustachi wake ulioonesha kutengenezwa na mafundi stadi.

Kwa hakika, alionekana kupendeza sana.

"Habari yako!", "Nzuri," nilimsabahi. "Karibu mama mdogo," Kaka yule akanikaribisha. "Asante," nikaitikia hku nikienda moja kwa moja na kuketi.

"Mimi kwa jina naitwa Ommy King John; sijui wewe mwenzangu unaitwa nani?" alimaliza kujitambulisha nami nikajitambulisha kwake kuwa, ninaitwa Pendo."

"Pendo mimi nimekupenda sana tangu ile jana nilivyo kuona pale. Nafikiri unanikumbuka vizuri" "Nakukumbuka saana." "Basi Pendo, mimi sihitaji penzi kwako bali, nahitaji uchumba, ninachoomba mimi ni kutaka unioneshe wazazi walipo nionane nao ili niweze kuongea nao na ikiwezekana nitoe posa sio masihara wala utani'.

Hayo maneno yaliyotoka kinywani mwa kijana huyu kwa mfululizo bila kupumzika, yalinitia hofu sana kiasi kwamba sikuyaamini na nilimuona kama mtu wa ajabu sana kama miujiza.

Mara akaniomba, "Pendo naomba unisindikize hapo jirani halafu tutarudi wote." "Siwezi kutoka hapa sasa hivi." aAkaondoka kimya kimya bila hata kuaga.

Kwa hisia zangu, nilianza kuhisi vitu vya ajabu ambavyo inawezekana havikuwepo kichwani mwake.

Muda si mrefu, nikaiona gari yake inakuja na kupaki mbele ya nyumba yetu, mara anaingia ndani huku akiwa ameshikilia Brief Case moja kubwa kisha kuniomba niipokee. Nikaona kutoipokea ni ushamba uliokubuhu na hata nikajua dhahiri kuwa kama nitamdhalilisha.

Nilisogea hatua mbili mbele na kuipokea.

Akanionesha tabasamu la kukata na shoka, badala ya mimi kumshukuru japo sielewi zawadi hiyo ambayo sijaifanyia kazi ina lengo gani, akanishukuru yeye. "Nashukuru Bi. Pendo kwa kuupokea huo mzigo; ni zawadi niliyokupa kwa upendo nilionao kwako utaniruhusu niondoke?" kabla sijamjibiu lolote, akaongezea, "Ila kesho kutwa naomba nije kwa ajili ya kunipeleka kwa wazazi ili niweze kuongea nao vizuri juu ya suala hili nyeti'.

kisha akaaga na kuondoka.

hadi anapanda ndani ya gari, bado tu nilikuwa nimesimama nikimuangalia na kumtumbulia macho ya mshangao, hasa nikikumbuka aliyonifanyia.

Nilingia chumbani na kuifungua ile briefcase na kukutana na kila aina ya vazi kuanzia viatu, nguo na vipodozi vya kila aina. Niliwaza sana juu ya kijana huyu hivi ni ya