Michezo

Yanga yalilia mfumo wa ligi

lYasema imeondoa kinga kwa timu nzuri

HUKU ikikabwa koo na Kajumulo World Soccer na Kariakoo ya Lindi, klabu ya Yanga imelalamikia mfumo mpya wa ligi kuwa ni hatari.

Akiongea na gazeti hili hivi karibuni Katibu Mipango wa Yanga, Abdul Sauko alisema mfumo wa sasa wa ligi si mzuri kwa kuwa unaweza kuzifaya timu kubwa kuenguliwa mapema.

Alisema mfumo wa ligi ya makundi ni hatari kwa soka la Tanzania kwa kuwa hauna kinga kwa timu kuwa na zinaweza kuenguliwa mapema.

"mfumo huu haukufanyiwa utafiti wa kina kabla ya kuanza na kinachoweza kutokea ni timu kubwa kuondolewa kwenye hatua za awali halafu "super Leangue" itakosa msisimko.

Hata hivyo Sauko alisema timu yake imefanya vibaya katika mechi zake za awali kutokana na wachezaji wake nyota watano kuwa kwenye timu ya taifa ya Tanzania "Taifa Stars" iliyokuwa Ghana.

Yanga inashuka nafasi ya pili kwenye kundi la Mashariki lenye timu za Kajumulo, Kariokoo, Lindi, Bandari Mtwara na Reli ya Morogoro.

Pamoja na kushika nafasi ya pili baada ya kuifunga Bandari ya Mtwara bao 3-0 Yanga haijajihakikishia kuvuka hatua hiyo ya makundi kwani bado wapinzani wake wakubwa Kajumulo na Kariakoo Lindi zinaibana.

Yanga imebakisha mechi mbili dhidi ya Kajumulo na Reli ya morogoro ambazo inapaswa kuzishinda ili kusonga mbele.

Kutokana na mfumo wa sasa wa Ligi Kuu Bara safari Langer, timu mbili za kuanza kutoka katika kila kundi zimeshika Super League na mbili zimesubiri mwakani wakati moja toka kila kundi itashuka daraja.

BACKHAM AZIDI KUWACHANGANYA WAINGEREZA:

Anyoa nywele kwa fidia ya milioni 400

London, Uingereza

Kiungo mashuhuri wa timu vya Manchester United ya Uingereza Devid Backama amezidi kuwatia kiwewe washabiki wa soka nchini Uingereza kutokana na vituko vyake katika ulimwengu wa soka.

Backama ambaye ni miongoni mwa wanasoka ghali dunianai, katikati ya mwezi huu alivunja rekodi pale alipolipa jumla ya shilingi milioni 400 ili akate nywele zake.

Akikaririwa na gazeti la Sun la Uingereza Beckama alikiri kuwa kampuni moja ya kutengeneza mafuta ya nywele ilimlipa jumla ya shilingi milion 400, ilikubali kukata nywele zake ziwe fupi ili zisimame na kuonesha uwezo wa mafuta hayo.

Mwanasoka huyo baada ya kukunja kitita hicho cha fedha alinyoa nywele zake zote na kumfanya awachanganye makipa wa timu mbalimbali ambazo Manchester imecheza nazo.

Moja ya timu ambazo zimeathirka na mpango wa Beakam wa kunyoa nywele ni Leasiter City ambayo kipa wake alifungwa na kiungo huyo kwa mpira wa adhabu ndogo.

Kipa wa tiu hiyo aliviambia vyombo vya habari kuwa alifungwa bao hilo kwa kuwa alipanga ukuta wa mabeki akijua kuwa mpigaji ni Rayal Keen, na hakufahamu kuwa ni Beckam.

Mkasa huu wa nywele za Beckam umekuja mwezi mmoja, baada ya Chuo Kikuu cha Manchester kutangaza kuwa kitatoa shahada kwa mtu yoyote atakayefanya utafiti wa kutosha wa maisha ya mwanasoka huyo na nishani hiyo itatwa Beckam.

Kabla ya hapo magazeti ya uingereza yalimpigia kelele Beackam kwa kutumia jumla ya shilingi milioni 10 katika sherehe ya mwanaye kutimiza mwaka mmoja.

Yalisema kuwa ni heri sehemu ya fedha hizo angezitumia kwa kusaidia maskini na wagonjwa duniani.

 

 TEFA kuchagua manahodha wapya

CHAMA cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Temeke {TEFA} Jumamosi hii kinafanya Uchaguzi Mkuu wa kuwapata viongozi wapya watakao ongoza jahazi baada ya kurekebisha yake katiba mara mbili.

Katibu Msaidizi wa TEFA Bw. Hassan Mpanjila mwishoni mwa juma alisema, "Uchaguzi utafanyika Jumamosi hii katika ukumbi wa Brass Band uliopo katika kambi ya JKT Mgulani ambapo utawashirikisha wajumbe wote waliochaguliwa na wanachama wao".

Bw. Mpanjila alisema kuwa wanakila sababu ya kujivunia katika kipindi chote cha uongozi ambapo waliweza kuleta maendeleo makubwa ya kujenga uwanja wa mpira, ofisi ya makocha, ofisi ya Waamuzi pamoja na ukumbi wa mikutanao ambao hutumiwa kama darasa la awali kwa watoto wadogo.

Nafasi zinazogombaniwa katika kinyang’anyiro hicho ni uenyekiti,uenyekiti msaidizi nafasi moja, katibu,katibu msaidizi nafasi moja, mweka hazina na msaidizi wake nafasi moja, nafasi ya mjumbe wa mkoa moja pamoja na nafasi ya tatu za kamati ya utendaji.

Katibu msaidizi alisema kuwa katika uchaguzi huo mkuu atarajiwa kuwepo mbuge wa jimbo la Temeke Bw. John Kibaso na utazamiwa kuanza hapo saa mbili asubihi.