Michezo

KUFUATIA MGOGORO WA NGAWIRA:

Yanga kuishitaki FAT, FIFA

Na Pelagia Gasper

KLABU ya Yanga ya jijini imesema itakishitaki Chama cha Soka nchini(FAT), kwa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), kutokana na kuwadhulumu fedha za zawadi ya Ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati.

Fedha hizo zilitolewa na Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Makamu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Yanga, Isack Joseph Shekiondo, aliliambia KIONGOZI mwanzo mwa wiki kuwa hatua hiyo inalenga kuonesha kuwa, klabu hiyo imeazimia kukikomesha chama hicho dhidi ya ubabaishaji wake. Shekiondo alisema kuwa hatua hiyo itachukuliwa muda wowote kuanzia sasa kwani Yanga ipo katika maandalizi ya msingi ya kufanya hivyo.

"Sisi tutaiandikia FIFA kuhusiana na madhambi hayo ambayo FAT imetufanyia kwa muda mrefu sasa maana, hawa FAT wamezoea kutudhulumu," alisema

Aliongeza kuwa moja ya vitu watakavyoambatanisha katika malalamiko yao kwa FIFA, ni hati ya makubaliano iliyoitiwa saini kati ya Mwenyekiti wa FAT, Muhidini Ndolanga na uongozi wa CECAFA kuhusiana na kuchukuliwa kwa dola za Marekani 2500.

Kwa mujibu wa hati hiyo, Ndolanga alikabidhiwa dola hizo mjini Kigali, Rwanda kwa ajili ya kuikabidhi Yanga pamoja na nyingine 7500 ambazo FAT ilitakiwa kuipa Yanga, jijini.

Mbali na hiyo Shekiondo amesema pia watawasilisha hati mbalimbali ambazo wao walikuwa wakitumia kuwasiliana na CECAFA katika kudai fedha hizo.

Alisema kuwa katika hali hiyo wanatarajia kukutana hivi karibuni kujadili na kupanga mikakati ya kuhusiana na hali hiyo.

FAT inadaiwa kula fedha za Yanga kiasi cha dola za Kimarekani 2,500 na chama hicho kukiri kuwa kimechukua fedha hizo kufidia deni la mamilioni ya fedha ambayo kimekuwa kikidaiwa.

Hata hivyo, uongozi wa chama cha Soka Nchini (FAT) haukupatikana kuzungumzia madai hayo ya kufikishwa mbele ya FIFA.

PAMBANO LA SIMBA NA YANGA JUMAPILI:

Polisi watakiwa kuwa ngangari

Na Mwandishi Wetu

POLISI jijini wametakiwa kuwa makini zaidi katika pambano kati ya watani wa jadi, Simba na Yanga, Jumapili hii ili kuepusha balaa kufuatia kuzuka kwa mtindo wa washabiki kuwapiga waamuzi hivi karibuni.

Ombi hilo limetolewa jana na mashabiki wa soka walioshuhudia ghasia kama zile za mashabiki wa Uingereza katika pambano la Simba na Kajumulo.

Wakitoa ombi hilo kupitia gazeti hili, mashabiki hao walioongozwa na mmoja wa waamuzi wa siku nyingi nchini, Bw. Omar Athumani, walisema kama polisi hawatakuwa makini katika pambano hilo, basi tunaweza kushuhudia mauaji kama yale yaliyotokea katika mpambano wa kutafuta bingwa wa Ulaya.

Alitoa mfano wa pambano la Kajumulo na Simba, ambapo mwamuzi alitwangwa ngumi, mawe na kurushiwa chupa na mashabiki wa Simba, tena mbele ya polisi.

"Kinachoonekana sasa hivi ni kuwa mashabiki wa hapa kwetu wanaiga staili ya Uingereza. Hii ni hatari sana, ni lazima jeshi la polisi lijisuke vema katika pambano la Jumapili," alisema kiongozi mmoja wa chama cha soka nchini-FAT.

Simba na Yanga zinapambana Jumapili kwenye Uwanja wa taifa jijini katika mzunguko wa pili wa "Nane bora" katika Ligi kuu ya Soka ya Safari Lager.

Yanga, inapewa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi katika pambano hilokutokana na kuwa na safu nzuri ya washambuliaji wenye uchu wa kuziona nyavu, wakiongozwa na mfungaji bora Mohamed Hussein-(Mmachinga).

Tyson kupanda tena ulingoni,aapa kujeruhi mtu bila uzalendo.

LONDON, Uingereza.

BINGWA wa zamani wa uzito wa juu katika masumbwi ya kulipwa ulimwenguni, Mike Iron Tyson, ameapa kumtwanga Mmarekani mwenzie Lou Saverese, na kunyoosha njia yake ya kumfikisha katika mpambano na Lennex Lowes wa Uingereza.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari juzi baada ya kufika nchini Uingereza kimya kimya ili kufanikisha juhudi zake za kuwakwepa mapaparazi, Tyson alisema kuwa atamtwanga Mmarekani huyo mwenzake bila huruma wala uzalendo ili atengeneze mapito ya kupambana na adui wake namba moja duniani, Lonnex.

Katika pambano hilo linalotarajiwa kuoneshwa moja kwa moja na Kituo cha Televisio cha DTV na Chaneli TEN usiku wa kuamkia Jumapili, ana rekodi

Kupigana mapambano 39.

Lou, anaonesha kuwa ameshinda mapambano yote hayo bila kupoteza hata mmoja na 32 kati ya hayo, alishinda kwa knock out.Tyson alisema kuwa ingawa pambano hilo si laubingwa wowote, lakini ni la muhimu sana kwake na lazima ahakikishe anashinda, tena mapema mno.