Matangazo ya tiba dhidi ya Ukimwi Serikali imekosa neno?

HIVI karibuni Rais Benjamin Mkapa ameionya jamii ya Watanzania hususan vijana kutoufanyia mzaha ugonjwa wa Ukimwi.

Kwamba viongozi wa juu kabisa wa Serikali wameonelea kujitosa katika kampeni ya kupambana na balaa hili la Ukimwi ni jambo la kutia moyo na kupongezwa.

Rais aliwataka Watanzania kujuepusha na zinaa, uasherati na ujinga mwingine unaoneza Ukimwi. Akisisitiza kwamba serikali kwa upande wake inafanya umakini mkubwa kuhakikisha kwamba kwa vile tu hajui unavyoambukizwa au kwa kuongezewa damu yenye virusi hospitalini.

Lakini Rais pia hakulifumbia macho suala wapuuzi wanaojiita waganga wa kienyeji ambao wamekuwa wakipotosha uma kwa muda mrefu kwa matangazo yao ya uwongo kuwa wanatibu Ukimwi licha ya ukweli ulio wazi kwamba ugonjwa huo haujapata tiba.

Waganga hawa wa kienyeji wamekuwa wakiupotosha uma kwa muda mrefu kwa matangazo yao ya uwongo kuwa wanatibu Ukimwi licha ya ukweli ulio wazi kwamba ugonjwa huo haujapata tiba.

Waganga hawa wa kienyeji wamekuwa wakijificha chini ya kivuli cha kufanya utapeli na wamekwishasababisha madhara makubwa katika jamii.

Kwa kusema hivyo hatumaanishi kuwa hatutaki ‘waganga’ hao washiriki katika utafiti wa dawa ya Ukimwi.

Tunawashauri ni kwamba waganga hawa wanapopata matokeo ambayo yanaonyesha maendeleo kidogo katika utafiti wao wasikurupuke kutangaza kwamba tayari wana ‘dawa ya Ukimwi’, hadi pale viwango vya tiba zao na uwezo wake vitakapothibitishwa pasipo mashaka. Haifai kabisa kuwajengea wagonjwa wa Ukimwi matumaini hewa kwa vile tu wako katika wakati mgumu.

Akilini tabia ya waganga hao ambao wenyewe hupenda kuitwa wa jadi, Rais Mkapa aliwaonya wananchi wananchi kutoamini matangazo ya waganga hao.

Cha kusikitisha ni kwamba wakati vyombo vya habari vinavyojiheshimu na viadilifu hapa nchini hutokea kutoa matangazo ya waganga hao bila kujali kuwa ‘wanafukuza pesa’, vyombo vingi visivyo makini ikiwa ni pamoja na redio na magazeti vimekuwa vikitumiwa kwa ‘vipesa’kidogo kueneza uongo huo unaoua.

Bila shaka sasa umefika wakati ambapo serikali inapaswa kufanya mambo yake kwa kumaaosha kwani itasaidia nini Rais Mkapa atangaze siku moja kwa mwaka kuwa Waganga wa jadi wanadanganya umma wakati matangazo ya wanganga hao yanaendelea kupingana naye kila siku redioni na magazetini?

Ni wakati ambapo serikali inatakiwa kuonyesha meno yake kwa kupiga marufuku matangazo yote ya namna hiyo redioni, magazetini na mitaani vinginevyo haiwezi kujiaminisha kwa umma kwamba imedhamiria kwa dhati kuokoa maisha ya wananchi wake.