Tutumie vizuri muda tulio nao

MARA kwa mara tumesikia wataalamu wa kituambia kuwa wakati ni mali na tunapaswa kuutumia vizuri. Hao wataalamu hutuambia kuwa muda tunaokuwa nao kwa ajili ya kufanya kazi huwa ni mfupi sana kwani tunao muda wa kupumzika usiku kwa zaidi ya masaa matano, tunao muda wa kula chakula, ambao pia haupungui masaa matatu kwa siku. Tunao muda wa burudani na michezo, ambao pengine huzidi hata masaa matano kwa siku. Kwa wale waumini, wanao muda wa kusali ambao kwa siku pengine siyo pungufu ya saa moja. Tunatumia pia muda mrefu katika kuwa hudumia wenzetu, kama vile kwenda kuwaangalia wakiwa huko mahospitalini au m ajumbani wamelala. Tunatumia masaa mengi sana katika kusafiri kwenda huko na huko kikazi. Kila mmoja wetu hutumia muda wa kutosha katika mambo ya usafi wake binafsi, usafi wa mazingira anamoishi, usafi wa vyombo, usafi wa nguo zake nk.

Ukishaangalia hivyo jinsi muda unavyotumika au pengine unavyopoteza hapo utatambua kuwa tunakuwa na muda mfupi sana katika kufanya kazi za maendeleo. Lakini jambo la kusikitisha, ni kwamba licha ya kuwa na huo muda mfupi katika siku nzima kwa ajili ya kufanya kazi, bado kuna wananchi wengi ambao hawautumia muda huo sawa sawa. Wako wengi ambao wamejenga ile tabia ya kupoteza muda. Kwao hao ndugu kuwahi mahali wanapotakiwa ni vigumu sana, na hivyo huanza kazi wakiwa wamechelewa. Ni tabia mbovu sana ya mtu kuchelewa kuanza kazi anapotakiwa. Tabia ya kuchelewa imejengeka kabisa ndani ya wananchi wengi hapa Tanzania. Hapo hawakumbuki kabisa kwamba wanapochelewa wanakwamisha pia ufanisi wa shughuli katika sehemu zao za kazi.

Siku ya leo hasa katika miji kuna visingizio vingi vya watu kuchelewa kufika kazini mapema. Kisingizio kikubwa kinachotolewa ni kila cha ugumu wa usafiri. Hilo ni kweli, lakini ikiwa mtu anajua kuwajibika atapanga kuwahi kuondoka nyumbani mapema. Na akifika kule kazini ni sharti ahakikishe kwamba anafanya kila jitihada ya kulipiza ule muda ambao amechelewa kwa kutia bidii zaidi ya utendaji. Lakini inashangaza sana kuona mfanyakazi kachelewa kufika kazini, na akifika kule kazini anatumia muda mrefu sana katika kuzurura na kufanya mambo yasiyohusikana na kazi yake. Wengi wa wafanyakazi hujivutavuta kazini na kupoteza muda mwingi sana katika mambo ya upuuzi.

Kati ya mambo mazuri yaliyotokana na sera ya ubinafsishaji mashika mbalimbali ni wafanyakazi kuwa na bidii katika sehemu zao za kazi. Wale wanaofanya kazi katika mashirika yale ambayo yamebinafsishwa wanajua jinsi ya kutumia muda. Kwa vile riziki yao hutegemea sana jinsi wanavyotumia muda wao, hapo tunao kuna uzalishaji wa hali ya juu sana. Hivyo pia ni katika ajira katika shughuli na kazi za watu binafsi, kwani kipato chao kwa vikubwa hutokana na jinsi wanavyozalisha au wanavyotumia muda wao wa kufanya kazi.

Tumeambiwa mara kwa mara kuwa muda ni mali, na hivyo inatupasa kuutumia vizuri katika uzalishaji. Kwa bahati mbaya kuna wengi wa wananchi bado wanatumia muda wao vibaya na hata kuna wengine ambao licha ya kulala usiku kucha, bado wanalala hata mchana bila kufanya kazi. Tunaambiwa kuwa kazi ni uhai, lakini wananchi wengi wanaona kuwa kazi ni utumwa na hivyo hawataki kabisa kufanya kazi ya kuajiriwa na hata ile ya kujiajiri. Watanzania walio wengi hutumia muda wao mwingi sana katika kuzungumza bila kuchoka na hivyo hakuna kinachozalishwa, licha ya kuwa na nguvu pamoja na afya nzuri.

Mara nyingi tumesema sana katika safu yetu hii kuhusu uvivu na uzembe. Tungeweza kusema kuwa tabia hiyo ya uvivu ni kama donda ndugu kwa Watanzania walio wengi. Vijana wengi na hata watu wazima wameridhika kabisa na hali duni walio nao na hivyo wanautumia muda wao mwingi sana katika mambo ya upuuzi. Tunazo nguvu kazi nyingi sana, yaani vijana na watu wazima wenye nguvu ya kufanya kazi za kuiendeleza nchi yetu hii, lakini muda huo hutumika katika ulevi na uzururaji mitaani.

Watanzani wengi tunaishi bila kuwa na ratiba ya kufanya kazi na wala kuwa na mipango ya kazi. Wengi huishi kwa kubahatisha kwani hakuna mipango yo yote ile ya kujiendeleza. Hata hivyo kuna baadhi ya Watanzania ambao wametambua kwamba muda ni mali na sharti kujiletea maendeleo katika maisha yao. Hao hutumia muda wao vizuri wakiwa wanayo ratiba ya siku nzima. Wamejipangia ni saa gani ya kuamka, saa ya kwenda kazini, saa ya kula chakula, saa ya kupumzika na kwenda kulala. Hao tunasema huishi kwa mipango na pia wana uchu wa maendeleo. Lakini kwa bahati mbaya utakuta pembeni mwao kuna wale ambao hawashtuki na lo lote liwe, hawana wivu wa kimaendeleo wanayoyaona kwa majirani zao.

Kwa nini mtu anaridhika kabisa na hali duni, licha ya kuwa na akili pamoja na nguvu? Kwa nini mtu anaridhika kuwa na nguo hafifu na papo hapo jirani ana nguo nzuri? Kwa nini mtu aishi katika nyumba mbovu, na papo hapo jirani yake awe na nyumba nzuri katika mazingira hayo hayo. Jibu lake tunasema ni kiburi na tabia ngumu ya kutopenda kuiga mazuri ya wenzetu. Leo tumo katika mwaka wa 2000 wa sayansi na tekinolojia. Haitawezakana kamwe kujivunia mwaka huu au

Wataamu huzidi kutuambia kwamba kinachohesabika hasa siyo wingi wa miaka tuliyoiishi hapa duniani, bali ni kitu gani tumekifanya wakati tukiwa duniani. Kuna wengi wameishi zaidi ya miaka 50, lakini wameacha umaskini tu hapa duniani. Uthibitisho wa jambo hilo tunaushuhudia wakati wa kufa jamaa ambaye alikuwa na uwezo baada ya kutumia nguvu na muda wake vizuri akaweza kujipatia mali.Ni kwa jinsi gani wanafamilia na wanaukoo wanavyogombania mali ya marehemu. Tunasema ama kwa haki ni tabia mbovu sana kutegemea cha ndugu wakati wewe mwenyewe una nguvu na wasaa wa kuzalisha unapokuwa mzima.

Tunamalizia Kauli Yetu kwa kuwasihi Watanzania kutumia muda katika kufanya kazi za kujiendeleza kwa ajili yao binafsi na hasa kwa ajili ya ndugu na jamaa pamoja na taifa hili kwa ujumla. Tuige mifano ya wenzetu walioendelea kwani maendeleo hayo yametokana na kufanya kazi kwa bidii wakitumia muda wao vizuri. Tusipofanya kazi kwa bidii tutazidi kuwa maskini na pia watumwa wa wale wenye kujituma katika kufanya kazi. Mwaka huu wa 2000 uwe ni mwaka wa kutumia muda vizur i zaidi na kuwa na mipango ya utendaji kila mahali inapotupasa kushughulika. Kazi ndiyo pambo la maisha ya binadamu.

Salamu kwa Wafungwa

Wapendwa sana ndugu wafungwa,

Mimi ni mama Ebliible, mama kiroho Italiano.

Ninaandika barua yangu Italia ndugu! Hamjambo? mimi mzima, asante Mungu. Hapa Kipupwe baridi nyingi ndugu, msiwe kuwa na huzuni lakini ninyi kupiga moyo konde. Ndugu, Msiogope, Yesu Kristu Mungu, ni karibu nanyi siku - usiku......... ndugu! Yesu Kristu Mungu anasema moyo wangu, moyo wako, moyo wa watu wote, sisi sote tunasikiliza !... Mungu anapenda watu wote ninyi zaidi. Sa......! ndugu imani inatusaidia kushinda matatizo ya maisha yote. Mimi najifunza swahili nyumbani, sasa haiwezekani kwenda shule jioni, mama mzee, lakini ninasoma kwa bidiii. Mimi natumaini ninyi kuelewa maneno yangu. Asante ndugu! kila siku mimi ninasoma Injili swahili na polepole ninalinganisha Injili Kiitaiano, ili nimeelewa maneno Matakatifu Mathayo, Marko, Luka, Yohane. Ndugu , tafadhali, ninyi kusema polepole Injili kama mama Elotitole. Ndugu ...... Injili! Asante ndugu!

Mimi nimejifunza kwa moyo swahili "ishara ya msalaba asubuhi na jioni, mimi kusema kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu Amina"

Hapo sasa, usiku baridi lakini mimi kila siku nyumbani kupiga magoti ninaomba Yesu Kristu Mungu na Bikira Maria Mama wa Yesu pia ninyi jamii wenu wote. mimi kuomba ...... Yesu njoo uwasaidie, Yesu Njoo unisaidie ili watu wote wakusadiki wewe ni Mungu MARANATHA! Imani yangu haina mipaka.. kila siku ninaomba mwenye Heri Katerina De Maltei ........ pia ninyi, watu wote Tanzania, Ndugu Amani iwe kwenu.

Nawatakia Krismas ya heri . Mungu awabariki kaitka mwaka mpya

Ndugu, wamisamehe naskosa swahili Asante sana

Mama Elotilole

Watoto zingatieni ujumbe mliopewa na Askofu Pengo

Ndugu Mhariri,

Nitafurahi sana endapo utanipa nafasi katika gazeti lako la KIONGOZI ili niweze kutoa maoni yangu kuhusiana na ujumbe waliopewa watoto na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo wakati wa kuadhimisha Jubilei yao iliyofanyika Desemba 28 mwaka huu.

Nasema hivyo kwa sababu Jubilei Kuu imeanza kuadhimishwa rasmi Desemba 25 mwaka huu na inatarajia kumalizika mwaka 2001 na kwa mwaka mzima Jubilei zitakuwa zinaadhimishwa Jubilei za makundi ya watu mbalimbali na kwa bahati nzuri watoto ndiyo wamekuwa wa kwanza kufungua mlango wa Jubilei na pia watafunga mlango huo pia Jubulei itakapomalizika.

Katika Jubilei hiyo ambayo ilihudhuriwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Pengo na kuwataka watanzania wote kuwajali watoto na kuwatetea kwenye haki zao na kuwataka watanzania wote wanapoadhimisha Milenia mpya iwe yenye amani haki na mtumaini bora kwa watoto kwani watoto ni kiungo bora cha Taifa la Kesho ni lazima wapatiwe Elimu pamoja na mahitaji ya maisha yaliyo muhimu.

Katika Millenia mpya inayoadhimishwa dunia iko katika sura mpya ambapo binadamu watu wazima wamegeuka kuwa kama wanyama hali ambayo inapoteza matumaini hususani suala la ubakaji ambalo linaongezeka kwa watu wazima kuwabaka watoto wadogo bila kujali umri walio hao, hivyo aliwataka watoto kupiga yowe pale wanapokabiliwa na pia aliwataka watoto wamtegemee Mungu wamkimbilie wamuombee na kumtumainia kwani yeye ndiye mtoaji wa yote.

Pia aliwataka watoto kuwaepuka marafiki wabaya ambao wanawadanganya katika kutenda mambo mabaya na kuwaheshimu na kuwasaidia wazazi wao na wazee wasiojiweza na kuwaheshimu wakubwa.

Wenu Katika Kristo,

Dayness Fortunatus,

S.L.P 61431

Dar es Salaam.