MIGOGORO NA VITA INAYOTOKEA AFRIKA

Yadaiwa kuwa ya kipindi cha mpito

BARA la Afrika limesambaratishwa kwa migogoro, hivyo kuna matarajio ya kuwa na mustakabali bora zaidi. Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mintarafu Amani na Udhibiti wa Silaha ambayo iko chini ya Umoja wa Mtaifa, Bw. Ivor Fung, 0.anaamini kuwa hata hivyo Bara hili limo katika kipindi cha mpito kwani mabara mengine nayo yaliyoendelea nayo yalipitia hatua kama hiyo.

Maelezo hayo aliyatoa alipohojiwa na gazeti la Kiingereza la 'New People’ na limetafasiriwa na John P. Mbonde.

Kwanini ni vigumu kujenga utamaduni wa amani barani Afrika?

Fung anasema kuwa katika Afrika kuna tamaduni nyingi za asilia lakini pia kuna tamaduni za kigeni ambazo zinaathiri na kupotosha maadili ya jadi kuhusu amani na usalama. Afrika imeathiriwa na tamaduni mpya nyingi, mathalani miaka ya nyuma bara la Afrika kamwe hatukuona makombora , mabomu au kila kiitwacho "khalachinov".

Zote hizi ni zana zinazoingizwa Afrika kutoka nchi za nje na kwa jinsi hiyo vijana (kizazi kipya) katika Afrika kinakabiliana na utamaduni wa kifo Katika miaka hiyo vijana wakiwa majumbani mwao walikuwa wanafundishwa juu ya tunu ambazo ni za Kiafrika.

Siku zinavyozidi kwenda, jamii ya kiafrika inakutana na tamaduni nyingine ambazo sasa sijui niseme zinaelekea kutuvutia na kutusisimua?

Naweza kusema hali hii zaidi imechangiwa na suala la uingiaji wa vitu mbalimbali likiwemo suala la Televisheni.

Vijana wanapokwenda kuangalia filamu za sinema wanamwona Rambo na picha nyingine za mapigano mithili ya kivita, polepole utamaduni wetu unaathiriwa kwa kasi isiyo na kifani.

Jambo lingine ni lile wimbi la demokrasia ambalo wakati mwingine hupewa tafsiri potofu na hivyo kueleweka isivyo na kuwakengeua na kuwafanya walinganishe na mapambano ya kihasama (‘jino kwa jino’ ‘Ngangari’ ‘Ngunguri) na hivyo hujijengea uahalali wa kufanya fujo na vitendo vya hatari kama wapendavyo, mitafaruku na ghasia huzuka, na hivyo utamaduni mpya tofauti kabisa (utamaduni wa kifo) na ule wa asili huria na kudumazwa kwa kasi ya uibukaji utamaduni mpya barani Afrika.

Ili kuhamasisha utamaduni wa Amani umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na UNESCO (shirika la Elimu, Sayansi na utamaduni) wamepewa majukumu ya kuandaa programu za mitaala ya elimu kuhusu amani ili iweze kufundishwa katika mashule, vyuo mbalimbali sambamba na masomo mengine.

Kuna vita vinavyoendelea na kuleta hofu na wasiwasi katika maeneo mengi ya Afrika, ni Kigezo gani ambacho kingekuwa ni muhimu kuleta suluhu ya kudumu ya kitedawili hiki?

Fung Mwenyewe anabainisha kuwa migogoro mingi katika Afrika ni matokeo ya uhasama ,mintarafu, umilikaji wa maliasili ni jambo muhimu kufahamu kuwa tuko katika kipindi cha mpito (kipindi cha majaribio) cha historia ya Afrika, Afrika oliyo jikomboa dhidi ya ukoloni mkongwe , sasa imejikuta imeathiriwa na kusambaza aina nyingi na kuendelea kung’ang’ania mning’inio wa ziada wa ukoloni. Wakati huo huo, Afrika inapaswa kuyashughulikia matatizo mengine mengi ambayo yamesababishwa na kuibuka kwa kipindi fulani ambapo jamii fulani inakuwa na taifa lake lenyewe.

Hayo yote huchangia katika ugumu wa kuelezea na kubuni mbinu na mikakati ya kuleta ufumbuzi dhidi ya migogoro ya Afrika kwa njia ya amani ya haraka.

Vita hivyo hudhamiria kupata uwezo wa kumiliki maliasili ni sehemu ya harakati za kuwania ukubwa?

Fung anasema kuwa ni wengi kabisa! Harakati za kuwania ukubwa katika Afrika siyo tofauti na mashindano ya kudhibiti na kuhodhi milki za Maliasili.

Migogoro mingi barani Afrika yahusiana na mapambano ya kihasama ya kutaka kuvuna maliasili. Hata katika hali halisi ya kijadi daima utagundua ajenda ya siri nyuma ya kila mgogoro au vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kwa kadiri ya maoni yangu ni mapambano ya kushindania umilikaji wa maliasili.

Kikundi au ukoo mmoja waweza kuwa na bahati ya kuwa katika hali bora zaidi (kiuchumi na kijamii) kuliko kikundi/ ukoo mwingine kwa misingi ya kihistoria kwa mfano kikundi kimoja kilibahatika kuwa na madaraka ya kiutawala na hivyo kuwa na uwezo wa kuhodhi matunda ya maliasili hali ambayo hupelekea kuibuka na kuenea kwa mapambano ya kivita baina yao.

Maisha

Wajue watoto wanaoendesha maisha kwa kutumia uimbaji

lmmoja ni kipofu, mwingine yatima

lHuingiza kati ya sh. 4,000-5000 kwa siku

lWawalaumu watoto wenzao ambao ni ombaomba wa Barabarani

Na Benjamin Mwakibinga

LIMEKUWA jambo la kawaida kuwaona watoto ambao wamefiwa na wazazi wao ama ambao wazazi wao hawana uwezo, wakiombaomba barabarani. Hali hii ni tofauti na mawazo na matendo ya watoto hawa wawili ambao mmoja wao ni mlemavu wa macho, mwingine ni yatima. lakini, kwa umri wao mdogo na hali ngumu walizo nazo katika maisha. Badala ya kujiingiza katika miradi ya kuombaomba au kushiriki uhalifu, tayri wamekwisha jiajiri wenyewe kwa kutumia vipaji vyao.

 

 

Mbali na kundi hili la ombaomba pia wapo wale watoto ambao hutumia vilema vyao aidha vya kuzaliwa navyo ama vinavyowapata ukubwani, kama mtaji wa kuombaomba.

Hali hii inapingwa vikali na watoto Ramadhan(15) maarufu kwa jina la Mbuta Likasu ambaye alizaliwa akiwa na kilema cha upofu wa macho na mwenzake Abdalah Hamad ambaye kafiwa na wazazi wake.

Watoto hao ambao wanakaa eneo la Mbagala Kiburugwa Manispaa ya Temeke mkoani Dar-Es-Salaam, wanasema kuwa pamoja na hali walizo nazo,hawakubali kuwa ombaomba wa barabarani na badala yake wameamua kuanzisha kikundi chao cha kuimba.

Wakizungumza na Mwandishi wetu,watoto hao wanasema kuwa katika hiyo shughuli yao ambayo huifanyia katika vituo mbalimbali vya magari,kumbi za starehe na maeneo mengine ambayo yana mkusanyiko wa watu, hujiingiazia kiasi cha sh.4,000 hadi 5,000 kwa siku.

"Usione hii kazi yetu siyo ya kila siku, lakini tukifululiza kuimba, inachanganyia kweli,tunapata hela ya kutosha" anasema Likasu

Hata hivyo katika uimbaji huo watoto hao wanasema kuwa, mwimbaji ni Lisaku na Abdalah husaidia kumwongoza mwimbaji huyo ambaye haoni(ni kipofu) na wakisharudi nyumbani, hufanya mahesabau na kila mmoja huchukuwa haki yake.

" Mimi hupewa pesa yangu ya kumwongoza Mbuta, naye Likasu huchukuwa pesa yake bila kugombana" anasema Abdalah.

Katika kazi yao hiyo ambayo Likasu hutumbuiza watu kwa kuwaimbia nyimbo za Kikongo, kila mtazamaji hutakiwa kutoa shilingi 200.

Wanasema wamefanikiwa kununua vifaa mbalimbali kutokana na kazi hiyo ambapo Abdalah amefanikiwa kununua baiskeli na Likasu anatumia pesa hiyo kulipia kodi ya nyumba na kununua chakula na mavazi.

"Mimi bwana hela yangu kwanza navaa na kula pamoja na kulipia kodi,mambo ya kujenga ama kununua kiwanja ama kitu kingine cha namna hiyo siyo sasa hivi hizi,isitoshe hata pesa ninayoipata ni ndogo sana," anasema Likasu.

Hata hivyo watoto hao wanasema kuwa wamekuja kufahamiana hapa jijini Dar-Es-Salaam.

Wakielezea jinsi walivyoweza kufahamiana,watoto hao wanaelezea kama ifuatavyo:-

"Mimi nilitokea kwetu Lindi kuja kutafuta maisha hapa Da-Es-Salaam,nilifikia eneo la Mtoni Mtongani kwa Baba yangu mkubwa. Baada ya kuona maisha ya hapo hayaeleweki, niliamua kuingia mitaani nikijishibisha kwa kuimba nyimbo" anasimlia Likasu.

Katika zunguka zunguka yangu, nilifanikiwa kukutana na huyu Abdalah na ndivyo hivyo tukaamua kuwa marafiki. nakufanya wote kazi pamoja"anaongeza.

"Abdalah aliniambia kuwa yeye anaishi na shangazi yake na eti wazazi wake wote wawili walisha kufa".

Abdalah anasema kuwa, baada ya wazazi wake kufariki, aliamua kuja jijini na kufika kwa shangazi yake aliyemtaja kwa jina la bibi Mambo-B ado anayeishi Mbagala Charambe ambako ndiko alikokutana na rafiki yake, Mbuta Likasu.

Akisimulia jinsi alivyo kutana na Likasu,Abdalah anasema " Huyu Likasu alinikuta hapa kwa shangazi yangu".

"Nikawa ninaongozanaongozana naye.

Akawa akiimba na kupata pesa, ananipa na mimi. Baada ya siku chache, nikamuambia shangazi kuwa Likasu anataka sehemu ya kuishi hapa nyumbani".

Abdalah anaendelea kusema kuwa Bibi Mambo-Bado alimpangisha Mbuta katika nyumba yake huko Mbagala ambapo alimpa chumba na kitanda kwa malipo ya shilingi 1500/= kwa mwezi kama kodi ya chumba hicho.

Anaongeza kuwa kwa sasa wanaishi wote katika chumba hicho.

Vile vile watoto hawa walisema kuwa wateja wao wengi wanapatikana katika kumbi za burudani yakiwemo mabaa na sehemu za mikusanyiko ya watu kama vile vituo vya mabasi na hata katika masoko.

Watoto hawa pia wamewataka wananchi wenye moyo wa kutoa msaada kuwa, wasisite na kwamba wao watapokea msaada wa aina yoyote ile pasipokujali ukubwa au udogo wa misaada hiyo.

Ramdhani na Abdalah wamesema kuwa wanapatikana Mbagala Charambe Nzasa kwa Balozi Monga karibu kabisa na Lupango Bar, nyumbani kwa Bibi Mambo-Bado.

Katika mahojiano hayo yaliyomfanyika katika ofisi za chama cha wafanyabiashara wa eneo la Manzese (CHAWAMATA), watoto hao walisema kuwa watu watakaposhindwa kuwafikia huko Mbagala wanaweza kuiacha misaada hiyo kwa uongozi wa chama hicho ambapo mmoja kati ya maafisa wa chama hicho Bwana Ally Makopo, alisema uongozi wa CHAWAMATA utaifikisha misada kwa wahusika.

Wametoa wito kwa watoto wenzao kuwa siyo vizuri kukaa barabarani kuombaomba wapita njia na badala yake, watumie vipaji walivyonavyo kukidhi mahitaji yao.

Wanasema kama ni msaada, watasaidiwa wakishaonesha bidii yao.