Kwa nini mpango wa Uzazi?(2)

Inatoka toleo lililopita

Baada ya muda wanandoa wanaanza kujisikia kutoridhishwa.

Mke anaanza kujisikia kuwa mume wake hampendi isipokuwa mwili wake tu kwa tamaa ya kuridhisha misukumo ya mwili. Mume vile vile anaanza kufikiri mke wake hapendi na hamlidhishi katika tendo la ndoa, kwa vile anaonekana ‘baridi’ na kumlazimu kila anapohitaji unyumba kuomba na kubembeleza.

Misuguano hii ya mitazamo,polepole huharibu uhusiano kati yao. Misuguano inapoendelea matatizo mengine huanza kisha kuishia kwenye talaka.

Nne: Sumu za ‘kupanga uzazi’ huwaona watoto kama ugonjwa kwa hiyo suluhisho tunaona nilazima tunywe dawa ‘sumu’ au tuwaue ili tuwazuie wasizaliwe.

Uja-uzito katika jamii ya leo huonekana ni jambo la huzuni badala ya kuliona kuwa jambo la furaha. Uja- Uzito baada ya mtoto mmoja au wawili kutendewa kama vile lingekuwa kosa la jinai, ambalo kila mmoja anachukua tahadhari kulikwepa baadaye. Kama wakristo tunajua kuwa mtazamo huu ni mbaya.

Biblia Takatifu inatufundisha kuwa watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu. Uwepo wa watoto wengi ni ishara ya upendeleo wa pekee wa Mungu. Je sisi binadamu tuna haki gani ya kuwakataa?.

Baada ya mtazamo wa dunia ya sasa ya kuwaona watoto kama bughudha inayotuzuia kufurahi kutumia utajiri.Lakini ikumbukwe kuwa huo utajiri hauwezi kuwa na maana bila watoto na kama kuna utajiri wa namna hiyo basi huo ni wa uchoyo, ubinafsi, ndani yake.Ipo chuki na ni ile ile ya Kain na Abeli (Mwa. 4:8-12).

Tano: Sumu ya uzazi wa mpango huwadhalilisha na kuwanyanyasa wanawake. Mwanamke anapotumia sumu hizo yeye na mume wake wanaukataa uzazi yaani ule uwezo wa mama kuwa mja- mzito. Uwezo pekee unaopasisha familia na jumuiya ya kitaifa na kimataifa unakataliwa na kuonekana ni mzigo.

Kwa vile sumu hizi zinatumiwa na wanawake tu zinaposhindwa kufanya kazi, na mwanawake akipata uja- uzito lawama yote anachiwa yeye na anatakiwa alishughulikie ‘kosa’ hilo kwa kwenda kumwua mtoto wake (kutoa mimba) mume katika hali ya namna hiyo hujitenga na lawama na yuko tayari kuwatelekeza wote. Ni binadamu anayekaa na wasiwasi. Ni mtu wa kuhurumiwa.

Anapoteseka kutokana na sumu hizo mwanaume huwaendelea wanawake wengine kwa ajili ya kurudhisha tamaa ya mwili wake. Wanamke huwa jami la starehe za wanaume kutokana na dawa za uzazi wa mpango.

Sita: Sumu za kupanga uzazi licha ya kuwadhalilisha watumiaji kisaikolojia, pia kuwadhalisha wanawake kwa kuwafanya wagonjwa daima.

Madhara/ magonjwa wayapatayo wanawake kutokana na sumu hizo ni mengi, baadhi yake ni magonjwa ya moyo, mvunjo wa damu ndani ya mishipa ya ubongo, shinikizo la damu kupofuka macho na maumivu makali ya kichwa kutoka damu ukeni, sarakani ya matiti, mlango wa tumbo la uzazi, kokwa, magonjwa ya maini, mimba nje ya miji wa mimba, kupata utasa wa muda au kudumu n.k.

Sumu hizi husababisha kupungua kwa uwezo wa taifa kuzalisha mali kwa ajili ya maendeleo na hivyo gurudumu la mzunguko wa umaskini huzikabili nchi maskini, ambazo hutumia sumu hizo ikiwemo Tanzania.

Ukweli ni kwamba nchi zilizotumia sumu hizi kwa muda mrefu, kama vile nchi nyingi za Ulaya, ikiwemo Italia, Ujerumani, Greece, Ufaransa, n.k zimeshuhudia idadi ya watu wao kupungua kwa kasi.

Ili kuweza kujizalisha, taifa lolote linatakiwa liwe na ongezeko la watu kwa mwaka na kwa wastani watoto 2.2 kwa kila familia.

Nchi nyingi za Ulaya uwezo wa kujizalisha kwa mwaka ni chini ya wastani huo.

Kwa kadiri ya taarifa iliyomo katika ‘hali ya uchumi wa Taifa katika mwaka 1998’ iliyotolewa na Tume ya Mipango,Tanzania