Yajue magonjwa ya kuambukizwa kwa watoto

TANGU wanapotoka tumboni mwa mama zao, kama watu wengine, watoto wachanga huanza kushambuliwa na mazingira mbalimbali zikiwamo athari za kiuchumi na hata mabadiliko ya hali ya hewa.

Hali hii samba,mba na kukua kwa kawaida kwa mwanadamu yeyote pamoja na maambukizo mbalimbali, huwafanya watoto nao kushambuliwa na magonjwa mbalimbali. Kwa Msaada wa kitabu kitwacho Mahali Pasipo na Daktari, tunajaribu kutazama kwa kifupi tu, baadhi ya magonjwa ya maambukizo kwa watoto.

TETEKUWANGA:

Ugonjwa wa tetekuwanga husababishwa na vijidudu vidogo sana aina ya vijasumu. huanza wiki 2 hadi 3 baada ya mtoto kukaa na mtoto mwingine ambaye tayari anao ugonjwa huu.

Kwanza kabisa, madoadoa au vipele vidogo sana vyekundu na ambavyo huwasha, huanza kutokea.

Hivi, hubadilika na kuwa malengelenge na mwishowe, kufanya ganga vyote kwa wakati mmoja.

Kawaida huanza kwenye mwili na baadaye hutokea kwenye uso, mikono na miguu.

Kunaweza kukawa na vipele, malengelenge, na ganga vyote kwa wakati mmoja. Kwa kawaida homa ni kidogo tu.

Tiba:

Ugonjwa hupona baada ya wiki moja. Mkogeshe mtoto kila siku kwa sabuni na maji ya uvuguvugu ili kupunguza kuwasha. Tumia nguo baridi zilizoloweshwa kwenye maji yaliyotokana na shayiri iliyochemshwa na kukamuliwa.

Kata kucha za mikono ziwe fupi kabisa. Kama ganga zinapata ugonjwa, paka gentia violet (g.v) au mafuta ya kuua vijidudu.

SURUA

Ugonjwa huu mkali ambao husababishwa na vijasumu pia ni wa hatari sana kwa watoto wenye utapiamlo au kifua kikuu.

Huanza siku 10 baada ya kukaa karibu na mtu mwenye surua, kwa dalili za mafua homa, makamasi, macho mekundu na kikohozi.

Mtoto huzidi kuwa na hali mbaya. Mdomo unaweza kuwa na vidonda sana na anaweza akaanza hata kuharisha.

Baada ya siku mbili au tatu, madoadoa meupe kama chembe za chumvi hutokea mdomoni. Siku ya kwanza na ya pili baadaye, vipele hutokea. Kwanza kabisa, nyuma ya masikio kwenye shingo, halafu kwenye uso na kwenye mwili na mwisho kabisa, hutokea kwenye mikono na miguu.

Baada ya vipele kutokea, kwa kawaida mtoto huanza kupata nafuu. Vipele huchukua siku tano.

MATIBABU:

Mtoto ni lazima apumzishwe kitandani, apepeswe maji ya kutosha na chakula bora. Kama mtoto hawezi kunyonya kutoka kwa mama, basi mpe mtoto maziwa yaliyokamuliwa kutoka kwa mama kwa kijiko.

Kwa homa na maumivu, toa "asetominofeni" au asprini. Kama anapata ugonjwa wa sikio, toa dawa ya kuua vijidudu.

Kama dalili za kichomi, ugonjwa wa uti wa mgongo au maumivu makali ya sikio au tumbo yanatokea, tafuta msaada wa mganga haraka sana.

KINGA YA SURUA.

Watoto wenye surua ni lazima wakae mbali na watoto wazima. Hasa ni muhimu sana kujaribu kuwazuia watoto wenye utapiamlo au mwenye kifua kikuu au ugonjwa mwingine wa muda mrefu kuchanganyika na watoto wazima.

Watoto kutoka familia zingine wasiruhusiwe kwenda nyumba ambayo kuna surua.

Ikiwa watoto wengine kwenye familia ambayo kuna ugonjwa wa surua, bado hawajaugua surua, ingefaa wasiruhusiwe kwenda shuleni, sokoni au madukani kwa muda wa siku kumi.

Ili kuzuia surua isiwauwe watoto, hakikisha kuwa wanakula chakula bora na cha kutosha. Watoto wazindikwe kuzuia surua wakati wanapofikia umri wa miezi nane hadi kumi na nne.

SURUA YA KIJERUMANI (German measles or Rubella).

Surua ya Kijerumani si kali kama surua ya kawaida, huchukua siku tatu au nne. Vipele vichache mara nyingi tezi zilizo nyuma ya kichwa na shingo huvimba na kuuma.

Mtoto ni lazima apumzike kitandani na atumie asprini kama ni lazima.

Wanawake ambao huugua surua ya Kijerumani katika miezi mitatu ya kwanza ya mimba wanaweza wakajifungua watoto wenye hitilafu au kilema.

Kwa sababu hii, wanawake wenye mimba ambao hawajawahi kuugua surua ya Kijerumani au hawana uhakika ni lazima wakae mbali sana na watoto wenye aina hii ya surua.

MUMPS

Dalili ya kwanza huanza wiki mbili au tatu baada ya kukaa karibu na mtu ambaye ana mumps.

Mumps huanza kwa homa na maumivu wakati wa kufungua kinywa au kula, baada ya siku mbili uvimbe laini hutokea chini ya masikio kwenye pembe za taya. Kwanza, upande mmoja na baadaye upande mwingine.

TIBA:

Uvimbe hupona wenyewe baada ya siku 10 bila hata ya kutumia dawa.

Aspirini inaweza kutumiwa kwa sababu ya homa na maumivu, mpe mtoto chakula bora kilicho na maji maji na weka kinywa chake safi wakati wote.

HATARI:

Kwa watu wazima na watoto walio na umri zaidi ya miaka kumi na moja, huweza kukawa na maumivu ya tumbo au uvimbe unaouma kwenye makende(wanaume) au matiti (wanawake).

Watu wenye uvimbe huu ni lazima wapumzike kitandani kabisa na kuweka mabonge ya barafu au nguo baridi zilizolowanishwa kwenye sehemu zilizovimba ili kusaidia kupunguza maumivu na uvimbe.

Kama dalili za ugonjwa wa uti wa mgongo zinatokea jaribu kupata msaada wa mganga.

KIFADURO:

Kifaduro hutokea wiki moja au mbili baada ya kukaa karibu na mtu aliye nacho. Huanza kama mafua kwa homa, makamasi hutoka puani, na kikohozi.

Wiki mbili baadaye, kifaduro hutokea.

Ghafla, mtoto huanza kukohoa haraka haraka sana bila ya kuvuta pumzi mpaka kohozi linapovutika hutoka, na hewa huingia haraka kwenye mapafu yake kwa mlio wa ajabu unaoitwa kifaduro.

Baada ya hiki kifaduro, anaweza kutapika katikati ya nyakati hizi za kukohoa mtoto huwa mzima kabisa.

Kifaduro huchukua miezi 3 au zaidi.

Kifaduro ni cha hatari hasa kwa watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja kwa hiyo wazindikwe mapema.

Watoto wadogo hawapati kikohozi chenye kifaduro kamili kwa hiyo ni vigumu kuwa na uhakika kama wana kifaduro au hapana.

Ikiwa mtoto mchanga anazimia anapokohoa au macho yake yamevimba panapokuwepo wagonjwa wa kifaduro kwenye sehemu yake mtibu kama mgonjwa wa kifaduro mara moja.

TIBA:

Katika hatua za mwanzo za kifaduro, erythoromycin, tetracyline au ampisilini zinaweza kusaidia. Chroramphenicol husaidia pia lakini, ina hatari zaidi. Ni muhimu.

Kwa wagonjwa wa kifaduro ambao wamezidiwa sana, phenobarbital inaweza kusaidia hasa ikiwa kikohozi kinamzuia kulala au kinasababisha degedege.

Ili kuzuia kupungua kwa uzito na hatimaye utapiamlo, ni lazima mtoto apate chakula bora na ale mara baada ya kutapika.

Wakinge watoto wako wasipatwe na kifaduro hakikisha kuwa wanazindikwa kuzuia kifaduro wanapofikia umri kutokifunga.

DIPHTHERIA.

Ugonjwa huu huanza kama mafua na homa, kuumwa na kichwa na maumivu ya koo. Ganga lililo kama ngozi la rangi ya kijivujivu au njano huweza kutokea kwenye koo na mara nyingine kwenye pua au midomo. Pumzi hunuka sana.

Ikiwa unashuku kuwa mtoto ana Diphtheria:-

Mweke kitandani kwenye chumba tofauti na watu wengine.

Tafuta msaada wa mganga haraka sana. Kuna dawa maalum (antitoxin) kwa diphtheria.

Toa penisilini kidonge kimoja cha uniti 400,000 mara tatu kila siku kwa watoto wakubwa

asukutue mdomo kwa maji yenye chumvi kidogo, Avute mvuke wa maji moto mara kwa mara.

Kama mtoto anaanza kupaliwa au kugeuka rangi na kuwa bluu, jaribu kuondoa ganga kutoka kwenye koo ukitumia kitambaa cha nguo kwenye vidole vyako.

Diphtheria ni ugonjwa wa hatari unaoweza kuzuiliwa kwa urahisi kabisa kwa zindiko la DPT hakikisha kuwa watoto wako wamezindikwa.

POLIO (ugonjwa wa kupooza wa watoto):

Polio hutokea zaidi kwa watoto walio na umri chini ya miaka miwili.

Ugonjwa huu unaosababishwa na vijidudu vya virus, huanza kama mafua kwa homa, hutapika na maumivu ya misuli.

Mara nyingine, hizi ndizo dalili zinazoonekana tu.

Lakini, wakati mwingine sehemu fulani ya mwili hulegea au kupooza.

Mara nyingi hii hutokea kwenye mguu au mkono mmoja. Baada ya muda mguu au mkono uliopooza huwa mwembamba na haukui kwa haraka kama huo mwingine.

TIBA:

Ikiwa ugonjwa umekwishaanza hakuna dawa itakayoweza kuondoa kupooza. Dawa za kuua vijidudu hazisaidii. Tuliza maumivi kwa asprini au astaminofeni na kukanda misuli inayouma kwa maji moto.

KINGA:

Mweke mtoto mgonjwa kwenye chumba tofauti mbali na watoto wengine. Mama ni lazima anawe mikono kila mara baada ya kumgusa. Kinga iliyo nzuri kuliko zote kwa polio, ni zindiko la polio.

Hakikisha kuwa watoto wamezindikwa kuzuia polio kwa matone akiwa na umri wa miezi miwili, mitatu na minne.

Mtoto aliyelemazwa na polio ni lazima ale chakula bora na kufanya mazoezi ili kuipa nguvu misuli iliyobaki. Kwa mwaka wa kwanza, nguvu inaweza kurudi kidogo.

Msaidie mtoto ajifunze kutembea kwa jinsi anavyoweza. Weka nguzo mbili ili aweze kuegemea. Baadaye, mtengenezee magongo ya kutembelea.

Waimbaji, mnajua umuhimu wenu?

Na. Jenifer Aloicye

KADRI miaka inavyozidi kusonga mbele, ndivyo umuhimu wa kwaya (uimbaji), inavyozidi kuonekana na hata kushika nafasi ya malaika katika Kanisa.

Kwaya ni utume na uinjilishaji, ni utume wa walei unaokoleza na kuchangamsha ibada kwa njia ya nyimbo.

Wanakwaya wanahusiana sana na kazi za kimisionari kwa sababu wanajitoa na kuacha kazi zao nyingi, kwa ajili ya mazoezi na matayarisho muafaka ya huduma hiyo katika sehemu, ibada na nyakati mbalimbali.

Wanakwaya wanaingia katika wito huo wa kimisionari kwa kuwa wamekuwa wakitangaza Neno la Mungu kwa njia ya nyimbo.

Katika kuimarisha mahusiano na Mungu, kwaya(nyimbo) zinaweza kutumika kwa kuabudu, kuomba na hata kushukuru.

Kanisa Katoliki ni moja na lenye ushirikiano mkubwa. Ni kwa mantiki hiyo pia kanisa linasisitiza umoja usiovunjika hata katika vikundi vya nyimbo na hata waamini wasio waimbaji.

Ni ukweli ulio bayana kuwa endapo wana kwaya au vikundi mbalimbali vya kwaya katika kanisa vitaungana na kuwa na ushirikiano thabiti katika kuifanya kazi hii ya kumtumikia Mungu, zitakuwa zimechochea umoja, upendo na ushirikiano katika Kristo ndani ya kanisa zima.

Vikundi vya kwaya havina budi kukolezwa kwa hali na mali; kama chumvi katika mboga ili nazo, zipate nguvu ya kukoleza pale pasipo na ladha halisi ya ki-Mungu kwani mboga isiyokuwa na chumvi, asilani haina ladha.

Hapa hapana budi kujiuliza swali hili; hivi utakatifu wa wanakwaya ukoje? Wanakwaya waliotangazwa wanachama wa utumwa wa uimbaji ni wanakwaya wale walio Wamisionari na walio viungo vya Kristo; tena, walio hai katika imani yao moja ya Kikristo.

Hao wanapaswa kuwa ni wanakwaya wasio na majivuno, wala kizuizi kinachowawekea mto baina yao na mahusiano mema na Mungu. Kizuizi kinachowawekea mipaka ya kuunganika na Mungu kwa njia ya sakramenti.

Wanapaswa kuwa wale wasio na masengenyo, bali wawe ni wenye kujua kuwa kanisa ni mahali pa namna gani. Tena, wanakwaya wa Kanisa wasiwe ni wanakwaya wanaoshiriki kuimba na kucheza ndombolo na shamkwale kwenye Night Club.

Wanakwaya wa chama chochote cha kitume ndani ya Kristo, wanatakiwa wajirudi, wajikosoe na kujirekebisha kimawazo, kimaneno, kimatendo na kitabia kwa jumla.

Itakuwa kwaya haina maana endapo waimbaji(wanakwaya), wataimba huku wakiihimiza jamii kufanya au kuepuka vitu kadhaa ambavyo wao wenyewe, wako kinyume kabisa na hali wanayoisisitiza.

Mfano, utaimba wimbo unaomshauri mwenzio afunge ndoa wakati wewe bado upo kwenye maisha yasio na muelekeo wowote wa kufunga ndoa ; tena bila sababu yoyote ya msingi. Je, utakuwa umemuonesha mfano gani?

Mfano mzuri unaotakiwa kuigwa na wanakwaya wote, ni mfano wa maisha ya mwanakwaya Cecilia ambaye ni Msimamizi wa wanakwaya wote.

Mtakatifu Cecilia, aliishi Roma katika karne ya tatu. Alitungiwa kitabu chake kilichojulikana kama "Mateso ya Mtakatifu Cecilia", aliuawa kwa ajili ya kumpenda Kristo.

Wazazi wake wote walikuwa wapagani lakini yeye, alibatizwa na kuweka nadhiri ya kuishi maisha ya ubikira ingawa wazazi wake hawakupendezwa na nadhiri yake. wakamlazimisha aolewe na kijana mmoja aliyeitwa Valerian.

Lakini yeye aliendelea kumwomba Mungu mpaka siku ya harusi yake ilipofika, akaendelea kuomba, "Ee Mungu wangu! Uilinde roho na mwili wangu ili usitiwe aibu mbele za watu, na Mungu alisikia sauti yake."

Ulipofika usiku, alimwambia Valeliani usiniguse kwani pembeni yangu kuna Malaika na malaika huyu atakupenda kama ukiniacha Bikira.

Kijana huyo alikuwa hajabatizwa kwa hiyo Cecilia alimsihi akabatizwe kwanza. Akaenda kwa Mt. Albano akabatizwa na aliporudi kwa Cecilia alimkuta malaika pembeni ndipo akamwachia.

Mfalme baada ya kuona hivyo alimshurutisha Cecilia aikane dini yake na Cecilia baada ya kukataa aliamriwa auawe.

Cecilia alikuwa tayari kufa kwa ajili ya Kristo. Alikatwa kichwa mara tatu lakini, hakufa mpaka baada ya siku tatu huku akiendelea kuomba, "Ee Mungu! Ilinde roho yangu na mwili wangu usitiwe aibu mbele za watu."

Hiyo ndio sababu iliyofanya kwaya zote ziwe chini ya msimamizi wao, Mtakatifu Cecilia kwa kuwa alimpenda Mungu na akawa tayari kufa kwa ajili yake.

Vile vile, katika maisha yake, alijenga kanisa lililojulikana kama Kanisa la Mtakatifu Cecilia.

Kwa hiyo ni muhimu kwa wanakwaya wote kufuata nyayo za somo wao ili wayajenge makanisa kwa kutoa zaka, sadaka, na kuwa na uhusiano mwema na wengine.

Pia, kuwa na upendo wa Kanisa. Kinyume na hayo, watakuwa hawajengi kanisa bali wanabomoa.

Mnatakiwa kufunga na kusali kila baada ya muda fulani mkimuomba Mungu awasaidie katika matatizo yenu yanayojitokeza ndani ya kwaya zenu maana, ndani ya kwaya zenu kuna matatizo mbalimbali yanajitokeza na matatizo hayo yanazidi kukomaa kwa kuwa hayana wa kuyashughulikia na mengi yanatokana na walimu wa kwaya hizo pamoja na wanakwaya wenyewe.

Maandiko ya kitabu Kitakatifu cha 2Timotheo 3:2-5, kinasema, "Watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasio wapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,..."

Mnatakiwa kuwa tayari wakati wa furaha na huzuni mkiwapenda maskini mkiwaimbia nyimbo za kuwafariji ili wajisikie kuwa na wao ipo siku watakuja kuwa mstari wa mbele kutangaza Neno la Mungu na hata kuuona ufalme wa mbingu.

Ingawa wanakwaya wanatakiwa kuiga mfano halisi wa kuwa wafiadini kama somo wao, hivi sasa wengi wao wanamkana Kristo.

Mfano, Ni kwa vipi ifikie hatua ya Mkristo kuolewa na Muislamu? Au, inakuwaje hadi anaolewa na Mkristo mwenzake lakini asiyefuata vema mafundisho ya kanisa na badala yake sasa mwanamke huyo anakwenda kuwa mke wa tatu?

Sasa, hapo kama sio kumkana Kristo ni kufanya nini? Je, wanaofanya hivyo wanaonesha mfano gani kwa wengine?

Kwaya ni chombo cha Kanisa kwa ajili ya Kanisa na kuimba kuzuri, ni kusali mara mbili lakini, kuimba kubaya ni sawa na kutosali kabisa. Wanakwaya wawe mfano bora wa kuigwa kimawazo, maneno na vitendo.

Ubinafsishaji ni nini?

l