Ijue michango na vimelea wengine wa tumboni

KUNA aina nyingi za minyoo na wanyama wengine wadogo mno (vimelea) wanaoishi kwenye matumbo ya watu na kusababisha magonjwa. Wale ambao ni wakubwa zaidi, huonekana katika choo.

Baadhi ya wanyama hao ambao huathiri hata afya za wanadamu ni pamoja na

minyoo(Roundworm au Ascaris, mchango mdogo wa tumboni,(threadworm or pin work),

whipworm (tricuris) na tegu.

Minyoo ambao huonekana kwenye choo mara kwa mara ni michango midogo ya tumboni na tegu. Safura na Whilpworms, wanaweza kuwa wengi sana tumboni lakini, wasionekane kwenye choo.

KUMBUKA:

Dawa za minyoo zinazopendwa sana zina "piperazine". Hizi zinafaa kwa minyoo na michango midogo ya tumboni tu. Wadudu wengine ni lazima watibiwe na dawa nyingine.

Minyoo au michango (ascaris)

Hii ina urefu wa mpaka sentimita 30 na ina rangi nyeupe au nyekundu(pinki)

Jinsi minyoo inavyoenezwa

KINYESI MPAKA MDOMONI:

Kwa utovu wa usafi mayai ya minyoo husafirishwa kutoka choo cha mtu hadi kwenye mdomo wa mtu mwingine.

Athari kwa afya:

Mara tu mayai yanapomezwa, huanguliwa na minyoo wachanga hutoka na kuingia katika damu. Hii, husababisha kuwashwa mwili mzima. Michango hii michanga husafiri na damu hadi kwenye mapafu, ambako mara nyingine husababisha kikohozi au kichomi.

Pia husababisha kukohoa damu. Wakati wa kukohoa, minyoo hii michanga huja juu pamoja na kohozi halafu, humezwa na kufikia tumboni ambako hukua na kuanza kutaga mayai.

Minyoo mingi tumboni husababisha tumbo kuchafuka na mtu kulegea. Watoto wenye minyoo mingi huwa na matumbo yaliyovimba.

Mara chache minyoo husababisha pumu, degedege au kuziba kwa utumbo.

Wakati mtoto ana homa, minyoo hutoka nje pamoja na choo au kutambaa kwenye mdomo au pua. Mara nyingine, inaweza kutembea kwenye njia ya hewa na kuziba.

Kinga:

Ili kuepukana na maambukizo ya minyoo, jamii inashauriwa sana kuzingatia matumizi ya vyoo. Kila mtu hana budi kunawa mikono kila kabla na baada ya kula au kushika chakula chochote. Ni muhimu sana kulinda chakula kisiingiliwe wala kukaliwa na mainzi.

Ni muhimu sana kufuata masharti ya usafi kama yanavyoelzwa na wataalamu wa mambo ya afya.

Tiba:

Kipimo kimoja cha piperazine(antepar), kitaondoa minyoo yote.

Mchango mdogo wa tumboni (thread worm, pinworm, enterobius, vermicularis):

Hawa wana urefu wa sentimita moja na rangi yao ni nyeupe. Mnyoo huu ni mwembamba sana na uko kama uzi.

Jinsi inavyoenezwa:

Minyoo hii hutaga mayai maelfu kwa maelfu kwenye matako nje ya njia ya choo kikubwa. Hii husababisha kuwasha, hasa usiku.

Wakati mtoto anapojikuna, mayai haya yanaingia chini ya kucha na yanachukuliwa hadi kwenye chakula na vitu vingine. Kwa njia hii, yanafikia mdomo wake au midomo ya wengine na kusababisha maambukizo mapya ya minyoo hii.

Hatari kwa afya:

Hawa si hatari. Kuwashwa kunaweza kukamsumbua mtoto na kumfanya asipate usinginzi ipasavyo. Basi.

Tiba na Kinga:

Mtoto mwenye aina hii ya michango, ni lazima avae chupi au suruali iliyokaza wakati wa kulala ili kumzuia asijikune.

Mnawishe mikono na matako(eneo la njia ya choo) ya mtoto wakati anapoamka usingizini na baada ya kwenda choo. Kila mara, mnawishe mkono yake kabla ya kula.

Njia nyingine zinazotumika kama kinga ya michango hii ni kukata kucha za mtoto ili ziwe fupi kabisa na kubadilisha nguo zake. Muoshe mtoto mara kwa mara na kumsafisha matako na kucha vizuri.

Paka vaseline kwenye njia yake ya choo na eneo linalozunguka wakati wa kwenda kulala ili kusaidia kuondoa kuwashwa.

Mpe dawa ya wadudu yenye piperazine kwa kipimo. Wakati mtoto mmoja anatibiwa kwa ajili ya wadudu hawa, ni busara kutibu familia nzima kwa wakati mmoja.

Ni muhimu kuzingatia kuwa usafi ni kinga nzuri kuliko zote.

Hata kama unawaondoa wadudu hawa, wataokotwa tena kama mtu si mwangalifu na usafi wa mwili wake. Hii michango midogo huishi kwa kiasi cha wiki sita. Kwa kufuata vizuri kanuni za afya, wengi kati ya wadudu hawa watakuwa wametoweka kabisa baada ya majuma machache hata bila ya kutumia dawa.

Whipwarm (Trichuria, Trichiura, Trichocephalus)

Wana urefu wasentimeta 3 mpaka 5 rangi nyeupe au kujivujivu.

Minyoo hawa kama michango, husafirishwa kutoka kinyesi cha mtu mmoja hadi kwenye mdomo wa mtu mwingine.

Kwa kawaida, huleta madhara kidogo sana, ingawaje mara chache husababisha kuharisha.

Kwa mtoto, wanaweza kusababisha sehemu ya utumbo kutoka nje ya njia ya choo (prolapse of the rectum)

Kinga yake ni sawa na minyoo(michango)

Tiba:

Kama minyoo inaleta matatizo, toa "thiabendazole(mintezol)" au "mebendazole" kwa kipimo. Kama utumbo huo umetoka nje, mgeuze mtoto miguu juu halafu, umwagie utumbo huo maji baridi. Hii itaufanya urudi ndani.

Safura

Urefu wake ni sentimita moja na wana rangi nyekundu.

Kwa kawaida minyoo ya safura haiwezi kuonekana kwenye choo. Kipimo ni kitu cha lazima ili kuhakikisha kama wapo.

Jinsi safura inavyoenezwa:

Safura wachanga humwingia mtu kwa kutoboa kwenye nyayo za miguu isiyokuwa na viatu. Hii inaweza kusababisha kuwashwa.

w Baada ya siku chache, hufika kwenye mapafu kwa kupitia kwenye damu, wanaweza kusababisha kikohozi kikavu na kwa mara chache, husabaisha kukohoa damu.

wMtu hukohoa hawa safura wachanga na kuwameza. Siku chache baadaye, mtu anaweza kuharisha au kuumwa tumbo.

wSafura hujishikiza kwenye kuta za utumbo. Safura wengi husababisha ulegevu na upungufu mkubwa wa damu.

wMayai ya safura hutoka mwilini yakiwa yamechanganyikana kwenye choo cha mgonjwa. Mayai hayo huanguliwa yakiwa kwenye udongo wenye majimaji.

wUgonjwa wa safura unaweza kuwa mojawapo ya magonjwa ya watoto yaliyo maharibifu zaidi.

wMtoto yeyote mwenye upungufu wa damu, mweupe sana na anayekula uchafu anaweza kuwa na safura. Ikiwezekana choo chake lazima kipimwe.

Tiba

Tumia Thiabendazole(mintezol) mebendazole, tetracholoroethylene(TCE), au bephenium (alcopar) kwa kipimo na tahadhari.

Tibu upungufu wa damu kwa kula vyakula vyenye chuma kwa wingi na meza vidonge vyenye chuma ikiwa ni lazima.

Njia bora ziadi ya kuzuia safura, ni kuchimba na tumia choo. Usiache watoto watembee miguu mitupu bila kuvaa viatu.

Tegu

Tegu hukua mita kadhaa kwa urefu katika utumbo lakini, vipande vidogo laini na vyeupe vianavyopatikana kwenye choo ni kiasi cha sentimita moja tu kwa urefu. Wakati mwingine, kipande kinaweza kutoka nje na kutambaa chenyewe na kupatikana kwenye nguo za ndani.

Watu hupata tegu kwa kula nyama ya nguruwe, nyama ya ng’ombe au nyama nyingine ambayo haikuiva vizuri.

Hakikisha kuwa nyama zote hasa ya nguruwe, zimeiva vizuri. Hakikisha kuwa hakuna sehemu mbichi katika nyama ya kuchoma.

Nguruwe hula mayai kwenye kinyesi cha mgonjwa wa tegu. Mayai ya cyst hutokea kwenye nyama ya nguruwe aliyekula mayai kwenye kinyesi cha mgonjwa wa tegu.

Wakati mtu anapokula nyama iliyopikwa vibaya, "cyst" hubadilika kuwa tegu tumboni mwake.

Cyst zinaweza zikasababisha kuumwa na kichwa, degedege au kifo.

Mayai ambayo huingia mdomo wa mtu kutoka kwenye choo chake mwenyewe kutokana na utovu wa usafi zinaweza kutokea cyst katika ubongo wake mwenyewe.

Athari kwa Afya:

Mara nyingine tegu husababisha maumivu kidogo ya tumbo, lakini shida nyingine ni chache.

Kuna hatari kubwa iwapo cyst(vifuko vidogo vyeupe tegu wachanga), zitaingia kwenye ubongo wa mtu. Hii hutokea wakati mayai yanapoingia mdomoni kutoka kwenye choo chake.

Kwa sababu hii, mtu mwenye tegu ni lazima afuate mashauri ya afya kwa uangalifu sana na apate matibabu haraka iwezekanavyo.

Tiba:

Tumia "niclosamida(yomesan), dichlorophen(antiphen)" au "quinacrine(mepacrine, atebrine)" fuata maagizo kwa uangalifu.

Trichinosis

Wadudu hawa hawaonekani kwenye choo kamwe. Wanatoboa kwenye kingo za utumbo wa mtu na kufika kwenye misuli. Watu hupata wadudu hawa kwa kula nguruwe au nyama nyingine isiyopikwa vizuri kama ilivyo kwa tegu.

Athari kwa afya

Kutegemea kiasi cha nyama iliyovamiwa na minyoo hii, mtu anaweza asisikie lolote au anaweza kuwa mgonjwa sana au hata kufa kutoka dakika chache hadi siku 5 tangu kumeza nyama iliyoambukizwa na minyoo hii mtu, huanza kuharisha au kusikia maumivu ya tumbo.

Ikiwa hali ni mbaya mtu anaweza pia kuwa na homa pamoja, kutetemeka pamoja na maumivu ya misuli.

Hali nyingine zinzoweza kujitokeza ni kuvimba kwenye macho na wakati mwingine miguuni, michubuko midogo(madoa meusi au mekundu) kwenye ngozi na kutokwa na damu katika sehemu nyeupe ya macho.

Hali mbaya huchukua majuma 3 au 4

Tiba

Tafuta msaada wa mganga mara moja "thibendazo (mintezol)" inaweza kusadia kidogo kwa kipimo, "corticostreroids" zinaweza kusaidia pia lakini, lazima zitolewe na mganga au daktari.

MUHIMU:

Kama watu kadhaa waliokula nyama ya nguruwe mmoja wanaugua baadaye, basi shuku ugonjwa huu wa trichoinosis

Kinga ya Trichinossisi

Kula tu, nguruwe au nyama nyininge ambayo imeiva vizuri.

Usiwape nguruwe makombo ya nyama au mabaki kutoka machinjoni mpaka yawe yamepikwa vizuri.

Narejea Tanzania kumshabikia mnyonge

HIVI karibuni mwandishi wetu John P. Mbonde alipata nafasi ya kukutana na Padre Joseph Healey, Mmisionari wa Shirika la Maryknoll na kufanya mazungumzo naye. Mmisionari huyu licha ya mambo mengi aliyogusia, alizungumza juu ya wajibu wa kuwatetea wanyonge.

Aidha alisisitiza masuala ya utamadunisho wa Uinjilshaji nchini Tanzania, pia aliwahimiza Wakristo wote kuwajibika na kushabikia katika uenezaji wa Habari njema kwani sisi sote ni Wamisionari.

Mbonde katika makala haya anajadili,

Kila baada ya miaka mitatu huwa naenda Marekani kwa likizo ya kawaida nyumbani. Mwishoni mwa likizo, kila mara huwa naulizwa swali lile lile na jamaa zangu wanaponiona nafungafunga tayari kwa safari ya kurejea Tanzania.

"Kwa nini unapenda kurudi tena Tanzania?" na kisha wanaongeza kutoa maoni yao mbalimbali.

Kwa mfano, "Tunakuhitaji hapa! na kwamba, "Unakimbilia nini wakati katika parokia nyingi za hapa hapa Marekani kuna kazi tele za kichungaji?"

Kwa muda wa miaka mingi, nimekuwa nikijitahidi kuwaelezea ni kwa nini nilipenda na bado napenda kurejea Afrika Mashariki ili kuendelea na kazi ya umisionari. Lakini, waling’ang’ania kutetea hoja zao. Yaelekea hawakutosheka na maelezo yangu hadi siku moja...

Binamu yangu Barbara alikuwa anaendesha kunipeleka uwanja wa ndege wa Kimataifa wa New-York ili nikapande ndege kwenda Dar-Es-Salaam, Tanzania.

Aghalabu, wanafamilia yangu ni washabiki wakubwa wa vilabu vya mpira wa miguu. Jioni ya siku iliyotangulia tulipozungumzia juu ya timu mbili zishabikiwazo kwamba zitacheza "Jumatatu usiku wa kandanda," Barbara akatamba, "Mimi nashabikia zile zinazofungwa. Daima nashabikia zile zenye unyonge ambazo ni dhaifu."

Kwa hiyo tulipokuwa garini kuelekea uwanja wa ndege aliponiuliza, "Joseph kwa nini unapenda kurudi tena Tanzania? Kumbe mwishowe, sasa nilikuwa na jibu. Barbara, kwa yamkini uyakumbuke yale uliyoyasema jana jioni kuhusu timu za mpira unazoshabikia.

Nilimwambia dhahiri kuwa, majibu yangu siyo tofauti na ule msimamo wako na mimi ninakwenda Tanzania kwa sababu ninashabikia Wanyonge. Ni dhahiri kwamba kuna mahitaji mengi na kila aina ya changamoto hapa Marekani.

Iwapo unataka kujua unyonge uliokubuhu, basi ni Tanzania.

Kufuatia takwimu za kiuchumi za hivi karibuni, Tanzania ni nchi ya tatu maskini duniani miongoni mwa nchi fukara baada ya Msumbiji na Ethiopia.

UKIMWI, janga la njaa, wakimbizi, malaria, imani za uchawi, ufukara, uchumi duni, rushwa, barabara mbaya na madhara mengine mengi, ni miongoni mwa kero zinazodunisha maisha ya watu. Tanzania imesongwa na kubanwa mno na hali hizo.

Kwa mantiki hiyo, sisi wamisionari tunakiri kuwa tumeitwa kuungana na wananchi hao katika matatizo hayo yote na kila inapowezekana, tunasaidia kuleta mafanikio angalau kidogo.

Baada ya maelezo hayo, Barbara akashusha pumzi na kusema, "Ala! Kumbe sasa naelewa! Ni kweli nafahamu kwa nini unapenda kwenda tena Afrika".

Ndipo nikaendelea kufafanua; "Tafadhali usiwe na mawazo kwamba mambo yote ya Afrika ni mabaya tu, na ya kukatisha tamaa.

Rais wa Kwanza wa Tanzania, Hayati Julius Kambarage Nyerere alisema, "Tuna matatizo mengi lakini tunabaki wachangamfu." Kusema kweli Waafrika ni miongoni mwa watu wenye furaha na wachangamfu kuliko watu wengine ambao nimepata kukutana nao licha ya ufukara mkali unaowakabili.

Ili kusisitiza juu ya maisha yangu ya umisionari nchini Tanzania, niliongeza kusema, "Hebu kitafakari kile kifungu katika Injili ya Mtakatifu Luka, wakati Yesu alipowaambia wafuasi wake, "Natangaza Habari Njema za Ufalme wa Mungu kwa miji mingine pia kwani nilitumwa kwa lengo hili."

Kifungu hiki, kwangu kinanigusa kikiwa na maana ya kwenda pia kwenye miji mingine ya Tanzania kama vile Arusha, Mwanza na Rulenge.

Hiyo ina maana ya kufuata nyayo za Kikristo ili kueneza habari njema kwa maskini, dhaifu waliotengwa na jamii, wapotelewao, na hasa kwa wanyonge.

Umisionari maana yake ni kusafiri bega kwa bega na hata Watanzania. Siku hizi tunaongelea sana juu ya "utamadunisho" wenye mtazamo wa kushabikia waenezaji Habari Njema za Yesu Kristo kwenye ardhi ya Afrika.

Ipo kanda ya video ya kupendeza sana juu ya maadhimisho ya kiliturujia katika bara zima la Afrika inayoitwa KANISA LA NGOMA(The Dancing Church).

Hili ni jina lenye sifa kubwa litangazalo moyo na shauku ya Kanisa katika Afrika.

Hayo yalikuwa ndiyo mazungumzo baina yangu na Barbara, binamu yangu ana hekima kushabikia wanyonge nchini Tanzania, ina maana kupambana na magumu na dhiki fulani fulani.

Mmisionari kutoka nje daima anaonja ugeni fulani, Wakristo wengi wa kijadi na tunu za Kiafrika hushambuliwa na shinikizo la malimwengu hasa katika miji mikubwa kama Dar-Es-Salaam na Nairobi.

Mtu anaweza kuchoshwa na mfululizo wa migogoro iibukayo barani Afrika. Siku za karibuni tuligubikwa na wasiwasi dhidi ya majanga makubwa ya asili kama tungeweza kuepukana nayo kama vile mafuriko makubwa yaliyoikumba Msumbuji na ukame mkali huko Ethiopia.

Kero za kila siku maishani, magonjwa na mikasa na maafa mengine mengi yametoa changamoto za kila namna lakini, kama alivyo mpwa wangu Sarah ambaye ni mwanamichezo aliniambia, "Mjomba Joseph, wakati mwingine utapaswa kucheza mchezo wa hatari."

Kwa kupitia hayo yote, nahisi kwamba zawadi kubwa kabisa ya umisionari niliyopewa na Mungu imekuwa na mapendo yasiyo na kifani kwa Waafrika.

Wao ni kaka na dada zangu kwani, Waafrika kwa upande wao wamenipatia upendo mkubwa na urafiki wa pete na kidole. Ninawiwa shukrani nyingi kwa zawadi hii ya thamani kubwa na neema.

Isije wazo hili wanyonge likawa zito kupita kiasi, napenda kuongeza kwamba kwa vile natoka Baltimore, Maryland na timu kipenzi wa kabumbu ni Baltimore Ravens (Raven ni ndege kubwa mweusi afananaye na kunguru).

Kamwe, nisingependelea wao kuwa wanyonge (wanaoshambuliwa au dhaifu). Yamkini, ninapenda wanapokuwa na vipenzi kabambe wa kuwashabikia.

Makala Maalumu

Kujibu mapigo ya Katoliki

Nani Askofu Halali?

Na Francis W. Rutaiwa, PhD

MASWALI nyeti yamejitokeza katika gazeti la MSEMA KWELI kuhusu msimamo wa Katoliki na uhalali wa Kanisa na Uaskofu. Maswali ya imani za Kikristo wakati mwingine, yanakuwa magumu kuyaongelea kwa utulivu hasa yanapogusa misimamo ya madhehebu ambayo sasa yanaongezeka kila kunapokucha kwa njia ya kumegukameguka yenyewe.

Kuna wengine, tena Wakristo "safi" wanaoamini kwamba kumeguka huku ni mpango wa Mungu ukisukumwa na nguvu za Roho Mtakatifu. Lakini, wengine wanahisi ndani ya tabia hiyo mna ishara za kuvuruga mpango huo huo kwa visingizio mbalimbali.

Sasa Maaskofu wa KKKT (nchini Tanzania) wamejaribu kujibu mapigo ya Katoliki au tuseme kauli ya Askofu Kilaini kutamka kuwa Kanisa ni moja. Ruksa kutoa upinzani kwa hilo lakini, isiwe kwa jazba kama ilivyojitokeza kwa kusema eti Askofu Kilaini ni Askofu ‘mchanga’ na asingetoa kauli hiyo, ila Papa mwenyewe.

Hapo KKKT wamesahau kwamba msimamo Katoliki kudai Kanisa ni moja, sio tu kitu kipya, na viongozi wa Kilutheri dunia nzima wanafahamu kwamba hoja hii imeisha zungumzwa katika vikao mbalimbali na viongozi Katoliki huko Vatican.

Isitoshe Katekisimu ya Kanisa Katoliki yenye mafundisho katoliki yenye kuaminika, inafafanua hoja hii kwa kina zaidi.

Aidha, Askofu Kilaini alichofanya ni kurudia kwa kifupi mafundisho yanayojulikana kwamba Kanisa la Kristo ni moja, Takatifu, Katoliki na la kitume.

Kwa maana ya fumbo Kanisa ni "Mwili Mmoja" wa Kristo, hali hizo nne zilizoungana bila kugawanyika kati yao, zinaonesha sifa za lazima za Kanisa na za utume wake.

Labda kuna sifa pia za kimadhehebu. Askofu Kilaini hakuingilia hoja hiyo. Kanisa lake kuwa Moja, Takatifu, Katolili na la Kitume na bado yeye anayeliita kuitekeleza kila moja ya sifa hizo.

Na kama kuna yeyote mwenye ubishi kwa hilo na anashikilia tu, mtizamo wa ki-madhehebu, au madhehebu yake, hiyo itakuwa ni imani yake binafsi lakini isiyo na ufunuo wa ki-Mungu.

Hapa hakuna dharau kwa madhehebu ya Kiprotestanti, ila ni kukumbushana na kushauriana tu ya kuwa, kipo kiini na msingi wa umoja katika makanisa yanayojihesabu katika kundi la Kristo.

Tusipuuze hilo kama mzaha pale Yesu anapotuagiza sisi(Wakristo)tuwe wamoja kama yeye na Baba walivyo. Utitiri wa madhehebu umeathiri maendeleo katika kuunganisha Kanisa la Kristo; na tatizo kubwa huenda linatokana na mamlaka kuwa nyingi mno kuwafanya Wakatoliki washindwe kufuatilia misimamo yote inayojitokeza.

Ingawa Bwana Joseph B. Lukindo, aliandika katika MSEMA KWELI, anategemea Biblia kuwa ndio mwongozo wa maswali yote ya kuwapata maaskofu.

Ningeshauri huyu ndugu angeangalia msimamo wa Kanisa kabla hajakimbilia tafsiri binafsi za Biblia. Kwani hata Mtakatifu Paulo mwenyewe, anaeleza kuwa nguzo na msingi wa kupata ukweli, ni Kanisa na wala si Biblia (1Tm 3:15).

Pia Mtakatifu Petro, aliyepewa mamlaka na Yesu Kristo juu ya Kanisa, anatuonya kwamba "Hakuna unabii katika Maandiko, upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu," (2pt 1:20).

Kumbuka pia ni Kanisa lililotunga Biblia likiongozwa na Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, BIBLIA NI MALI YA KANISA na sio kama KANISA NI MALI YA BIBLIA. Tena sio mambo yote ya Yesu(Kanisa) yaliandikwa katika Biblia.(Yn 21:25).

Bw. Lukindo, kuchunguza sifa za kumpata Askofu ni vyema kabisa. Lakini, je, unafikiri maaskofu tu, ndio wenye sifa hizo? Au anapendekeza iwe ni haki ya kila mmoja mwenye sifa hizo kuwa askofu?

Si wazi mtizamo kama huo unaashiria vurugu ya kujinadi mbele za Mungu kwa sifa, watu kadhaa wakidai kuwa nazo? Mtazamo unaomfurahisha sana adui wa Kristo.

Wanachojaribu Wakatoliki kuwaambia Wapotestanti ni kwamba, U-MADHEHEBU UMEPITWA NA WAKATI, na kwamba sasa, Wakatoliki na Wakristo wengine wote, wanastahili kuwa kitu kimoja, kwa sifa na utukufu wa Kristo wao aliyeomba hali ya umoja itimizwe.

Kwa jambo la Kanisa moja, Yesu aliomba akisema, "Baba Mtakatifu kwa jina lako ulilonipa, uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo,"(Yn 17:11b). akarudia: "Wote wawe na umoja kama wewe, Baba ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma." (Yn 17:21.) Kumbe kupinga umoja ni kikwazo kwa ulimwengu kumsadiki Kristo ipasavyo.

Sio siri, Yesu alikabidhi Kanisa lake kwa viumbe wanadamu dhaifu. Wakati mwingine vinazidiwa na mzigo huu wa Kimungu. Lakini, hii isiwe kisingizio cha kujimegua kuunda vidhehebu tu, ambavyo tukivitafutia uhalali katika Biblia, basi Kanisa litaendelea kumeguka bila mwisho. Huu sio mpango wa Mungu.

Hakuna ufunuo wowote wa Ki- mungu unaotoa kibali cha namna hiyo. Kujitenga na Kanisa asilia kama njia tu ya kuboresha mpango wa Mungu ni maarifa tu, ya kibinadamu yanaposhindwa kumtegemea Mungu mwenyewe kusafisha Kanisa lake.

Uwezo anao, hata kukiwamo na wadhamini na wadhaifu wa kiasi gani ndani ya Kanisa. Yesu anatualika tuwe wamoja katika Ufalme wake. Yaani, Kanisa lenye wadhambi na watakatifu pamoja, na vipaji tele jinsi inavyompendeza kuvitoa.

Kanisa tena ni shamba lake Kristo. Tusiharakishe kuunda madhehebu, jinsi ya kutoa magugu kabla ya mavuno. Si Yesu alifundisha tuache ngano ikue pamoja na magugu?(Mt. 13:30).

Sasa hii hoja ya kupata uaskofu halali au Daraja nyingine katika Kanisa sio jambo geni kwa wale walio makini kwa historia ya Kanisa. Tangu karne za kwanza za Kanisa, aina mbali mbali za huduma zikifanyika ndani ya kanisa.

Mapokeo yashuhudia kuwa cheo cha wale ambao wameingizwa katika uaskofu, hushika mahali pa kwanza, kwa mfululizo unaorudi hadi mwanzoni, waangaliwa kama wapitishaji wa mbegu ya kitume.

Ili waweze kutimiliza utume wao wa hali ya juu, mitume walijaliwa na Bwana mmimino wa pekee wa Roho Mtakatifu, ukiwashukia nao kwa kuwekea mikono waliwagawia karama hiyo ya kiroho wasaidizi wao, inayodumu mpaka siku hizi kwa njia ya wakfu wa kiaskofu(Mdo 1:8;2:4, Yoh 2:22-23; 1Tim 4:12-14).

Mmoja hufanywa mshiriki wa kiaskofu kwa nguvu ya utakaso wa kisakramenti na kwa ushirika wa kihierarkia pamoja na kichwa cha urika na viungo vyake. Mazoea ya zamani sana ya Kanisa yanataka maaskofu wengi washiriki katika ibada ya utakaso wa askofu mpya.

Haya yote yana asili yake katika Kanisa Katoliki. Siku hizi kwa ajili ya kutoa daraja halali la askofu, hutakiwa uamuzi wa pekee wa Askofu wa Roma, mintarafu ubora wake wa kuwa kiungo cha juu kabisa kinachoonekana cha umoja wa Makanisa ya pekee katika Kanisa moja, na mdhamini wa uhuru wa makanisa hayo. Lakini, Kristo anaendelea kutenda kwa nia ya maaskofu (Efe4:11).

Maaskofu waliopewa daraja ya halali ni wale walio katika mstari wa mfululizo wa kitume na ndio hao wanakubalika kutoa ngazi tatu halali za Sakramenti ya Daraja.

Maaskofu huchaguliwa miongoni mwa waamini wanaume wanaoishi useja na walio na nia ya kudumu useja "Kwa njia ya Ufalme wa mbinguni"(Mt 19:12). Mhudumu wa Kanisa anawekwa wakfu; akipokea useja kwa moyo wa furaha anatangaza ufalme wa Mungu kwa namna iliyo angavu (1Kor. 7:32).

Hakuna aliye na haki ya kupokea Sakramenti ya Daraja. Kwa kweli hakuna anayeweza kudai kazi hii au kuigombea kwa ajili yake mwenyewe. Kwa ajili ya kazi hiyo mmoja huitwa na Mungu, na anapaswa kwa unyenyekevu kuweka tamaa yake chini ya mamlaka ya Kanisa ambalo lina wajibu na haki ya kumwita yeyote kupokea Daraja. Kama zilivyo neema zote, sakramenti hii hupokelewa tu kama paji ambalo mmoja hastahili.

Yule aliyepewa daraja halali aweza, kwa sababu kubwa, kuruhusiwa kuacha wajibu na kazi zinazohusiana na daraja au anaweza kuzuiliwa asizitekeleze. Lakini hawezi kurudia katika hali ya mlei kwa maana halisi kwa sababu alama aliyochapwa kwa kupewa Daraja yadumu daima.

Kwa kuwa mwishowe ni Kristo mwenyewe anayetenda na kuleta wokovu kwa njia ya mhudumu huyu wa Daraja, kutofaa kwake mhudumu huyu hakumzuii Kristo kutenda. Ni sawa na wale wanaofukuza mapepo kwa JINA LA YESU. Mungu anawaruhusu kufukuza pepo kwa mamlaka iliyomo ndani ya JINA lake, hata kama wao binafsi hawastahili. (Lk. 10:17-20).