Uchaguzi wa Kisiasa kwa nini tujali?

makubwa yaliyojitokeza katika Sera za Uchumi na Siasa.

Mfumo wa kiuchumi ulibadilika ghafla kutoka Ujamaa kwenda Ubepari wa Soko huria na matokeo yake miundo mingi ilibidi ibadilishwe Benki au mfumo wa fedha, matumizi ya Serikali, ukusanyaji wa kodi.

Biashara zilizokuwa zinamilikiwa na Serikali zimefungwa ama kuuzwa ambapo ulipaji wa madeni ya nje umekuwa ukichukua sehemu kubwa sana ya mapato yatokanayo na mauzo ya nje. Maamuzi yote haya yalikuwa na athari katika maisha ya kawaida ya kila Mtanzania. Wengi wamekuwa wanalazimika kulipa zaidi ya hapo awali katika huduma za kawaida za elimu, afya, maji na usafiri. Lakini cha muhimu kujiuliza hapa ni kwa kiwango gani watu walieleweshwa sababu za mabadiliko katika sera hizo?

Wanasiasa wangapi na Ilani zipi za vyama ziliweza kuelezea wananchi kwa uwazi na ukweli sababu za mabadiliko hayo na hivyo kuwapa fursa wananchi kubainisha vipaumbele vya mahitaji yao ili kidogo kilichopo kitumike kwa kuzingatia umuhimu na mahitaji?

Wakati Vyama vya Kisiasa kupitia Ilani zao za Uchaguzi viliahidi kuboresha na kuanzisha Elimu ya Msingi, maji, barabara, mfuko wa ajira kwa vijana , ni kwa kiwango gani katika hali halisi tunaweza kusema matamko yao yalikuwa ya ukweli na ambayo wangeweza kuyatekeleza?

Ni wazi walioandaa Ilani hizo walijua kabisa kwamba ahadi hizo zisingeweza kutekelezeka. Wale waliokuwa wagombea katika vyama vilivyokuwa vinavuma na uwezo wa kuelewa ugumu wa mambo waliyokuwa wanayawasilisha na kuyaahidi kwa namna rahisi tu na kwa maneno matamu.

Kwa upande mwingine watu wengi waliokuwa wakisikiliza Kampeni za uchaguzi hawakuelewa mabadiliko makubwa yaliyokuwa yanafanyika kwao wenyewe, mabadilko ambayo yanaathiri maisha yao wala hawakujua vema namna ya kufikiri juu ya Kampeni hizo bali walibaki kufurahia tu maneno matamu na ahadi nzuri zilizokuwa zinatolewa.

Ni wazi kabisa kuwa wapo Watanzania waliojisikia uzito fulani katika kupokea maneno hayo na hawakujisikia kabisa kuwa ni watu huru na wenye haki ya kuwachagua Viongozi wao na kushiriki katika kuchangia mawazo katika uundwaji wa Sera. Kwa hakika walijisikia kuwa Sera zimetayarishwa kwa ajili yao pasipo wao kushirikishwa.

Katika uchunguzi wananchi walilazimika kuwapigia kura wagombea ambao waliteuliwa na kundi dogo ndani ya Chama na kuletwa kwa kundi kubwa la wananchi kwa uthibitisho tu.Na kwa kweli ingawa sasa tuko katika Mfumo wa vyama vingi bado hatuwezi kuridhika kuwa tuna demokrasia zaidi ya hapo awali tulipokuwa katika Mfumo wa Chama Kimoja na hii si ajabu kwamba wananchi wamekufa moyo kabla ya uchaguzi unaofuata kwa sababu tunachoona ni mapambano ya Kisiasa kama mchezo wa mieleka na masumbwi ambao hawaonekani kuwa na lengo lolote zaidi ya kupata ushindi na madaraka. Hata hivyo kinachotakiwa si kukata tamaa bali ni kuwa na mfumo utakaowarudishia watu kilicho chao, yaani uwezo wa;

w Kushiriki kwa dhati katika utengenezaji wa sera nchini kwa manufaa ya Watanzania wote.

w Kuchagua viongozi watakaofanya kazi kwa manufaa ya Watanzania na sio kwa manufaa ama yao binafsi au ya vikundi vyenye uwezo fulani.

wKuhimiza watu wote wenye mapenzi mema kuungana na kufanya kazi kwa manufaa ya wote bila kujali hisia za kikabila au kidini .

w Kuunda vikundi vya watu wanaowajibika na wenye msimamo kimaadili ili kwa pamoja waweze kusimama na kutetea haki za raia wote, kufanya kazi ya kutafuta haki kwa wote na kuchukua jukumu maalum la kuwasaidia walio maskini, wadhaifu au wale wanaoteseka kutokana na kutopata fursa na kuelekea kusahaulika.

Tunahitaji kuangalia upya maadili katika shughuli za Siasa hapa Tanzani.

Tunahitaji pia damu mpya mawazo mapya na uongozi wenye kujitoa kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Taifa na watu wake.

4. Kwa vipi tunaweza kuhamasisha watu waweze kutumia madaraka na uwezo wao?

Katika maandalizi ya uchaguzi tunapaswa kuwahamsisha watu waelewe kuwa kazi yao si kuzikilizza tu hotuba na propaganda za Kisiasa. Zipo habari na taarifa ambazo lazima watu washirikishwe ili wapate moyo na kuthubutu kuzungumza katika mkutano ya hadhara. Hapa twaweza kugusia mifano michache;

w Ilani za vyama vya siasa zilieleza nini katika uchaguzi wa 1995? Sasa mwaka 2000 Je, mangapi kati ya hayo yalikuwa na umuhimu kulingana na mahitaji ya eneo lako?

wNi ahadi zipi ambazo zimekwishatekelezwa.

wNi sababu zipi tunadhani ni za msingi zilizopelekea ahadi zilizowekwa zisitekelezwe.

wJe watu wa eneo lako tayari wameshatafakari juu ya mahitaji ya eneo wanalishi na kuyaweka mahitaji yao kipaumbele?

w Watu wanawezaje kupima upeo wa mgombea katika kuelewa masuala mbalimbali na uwezo wake katika kupendekeza njia za kuyashughulikia - mfano barabara upatikanaji wa maji dawa za kutosheleza katika zahanati, ada za shule. Je unadhani mbinu anazodai kuzitumia mgombea zitaleta mafanikio? zinatofautianaje na zile za 1995 ambazo hazikutekelezeka?

5. Mbinu za Uhamasishaji

Sehemu ya pili ya kijitabu hiki tumeandaa mada sita kwa tafakari hii ni kwa kumsaidia Mhamasishaji mada zinazotoa mawazo na tafakari juu ya namna ya kufanyia kazi suala fulani na kusaidia watu kutafakari na kujileza wenyewe. Mada hizo ni msaada tu.

Mhamasishaji anaweza akawa na mambo mengine ya kusaidia kutafakari ama mahitaji mengine ya msingi kwa wakazi wa eneo lake ambayo yanaweza kuwa bora au muhimu zaidi. Lengo kuu ni kuwafanya waelewe kuwa wao ndiyo nguvu ya kuchochea ukuaji wa siasa na maendeleo.

Kitu kingine cha muhimu katika kazi hii ya kuhamashisha ni kuangalia kwa makini makundi maalum katika jamii kulingana na mahitaji yao makundi ya mijini na vijijini, wakulima, wanafunzi, wanawake na vijana wasio na ajira. Makundi haya yana mahitaji, mapendeleo na matatizo yanayotofautia. Kama wahamasishaji tunapaswa kuangalia mahitaji ya makundi hayo na kuwasaidia kujieleza wenyewe na pia kuelewa vema kuwa wana haki na wajibu kwa jamii nzima.

Kwa kusaidia tafakari na mbinu za uhamasishaji mada sita zifuatazo zimechaguliwa;

v Utamaduni wa Kidemokrasia

v Uongozi

v Mipango ya uchumi

v Afya

v Elimu

v Masuala ya kijamii

Chini ya kila mada yameangaliwa masuala na maswali kadhaa.

Maisha na Mikasa

Nimeteseka miaka minane sijapona sasa nangojea uamuzi wa Mungu

lBaba alinisusa baada ya kuachana na mama

Na Dalphina Rubyema

ROBERT Leo, ni kijana mkazi wa Kinondoni Shamba, jijini Dar es Salaam.

Miaka minane iliyopita alikumbwa na ajali ambayo kwa maelezo yake imekuwa mwanzo wa mateso makubwa yanayomkosesha hamu ya kuishi.

Hata hivyo, Leo angali anayo matumaini ya kuwa mwenye furaha tena endapo atasaidiwa, ingawa matumaini hayo yanaonekana kuwa madogo unapoongea naye ana kwa ana. Fuatana naye akielezea mkasa huu uliompata akicheza mpira wa miguu.

"Kama ni mateso nimeyapata. Niliumia mwaka 1991 na kuwekewa vyuma gotini. Kwa vile haikupatikana pesa ya kutolewa vyuma hivyo nimesota navyo hadi Aprili, mwaka huu nililopata pesa kutoka kwa wasamaria wema na ndipo vyuma hivyo vilipotolewa"

Kisa chenyewe kiko hivi:

Mimi baada ya kumaliza darasa la saba katika shule ya Msingi ya Mbuyuni sikuweza kuendelea na Sekondari hivyo niliona bora nikuze kipaji changu cha kucheza mpira.

Hivyo nilijiunga na timu ya mtaani kwangu iliyokuwa ikijulikana kama Jamaica.

Ingawa nilikuwa na umri mdogo wa miaka 13, niliweza kucheza mpira mzuri sana na kuwa mchezaji ambaye nilikuwa nikitegemewa sana na timu yetu.

Mwaka 1991 mwishoni, wakati timu yetu iliposhindana na timu ya mtaa mwingine inayoitwa 11Killers ndiyo hiyo siku nilipopata mkasa huo mzito.

Siku hiyo mchezaji wa timu ya 11 Killer ambaye namkumbuka jina lake kuwa Maena, alinikanyaga kwenye goti langu la mguu wa kushoto goti hilo lilizunguka na kugeuka nyuma, palepale marafiki zangu baada ya kuona nimeanguka chini na kupoteza fahamu kwa muda walikimbia na kukodi taksi iliyonipeleka moja kwa moja katika hospitali ya Muhimbili.

Kwa kweli nilikuwa nasikia maumivu makali sana, nisingeweza kutembea kutoka kwenye uwanja wa shule ya Sekondari ya Kinondoni hadi kituoni ndio maana hata rafiki zangu waliona bora wakodi taksi.

Nilipofikishwa Muhimbili walinipeleka moja kwa moja kwenye wodi ya Kibasila.

Sikucheleshwa sana huko, nilipelekwa moja kwa moja chumba cha upasuaji ambapo nilifanyiwa operesheni.

Baada ya operesheni niliwekewa vyuma kwenye maungio ya goti ili lisiendelee kuchezacheza, na nilikaa Muhimbili kwa kipindi cha miezi mitano nikitibiwa.

Mwezi Machi mwaka 1992 ndipo nilipopewa ruhusa ya kurudi nyumbani ambapo nilivalishwa P.O.P kutoka kwenye paja hadi kwenye unyayo.

Baada ya kukaa nyumbani kwa kipindi cha siku sita saba hivi, hali ya mguu ambao sasa ulikuwa umepata nafuu, ilianza kubadilika tena, nilianza kusikia joto joto kwenye sehemu ya kidonda.

Mguu ulianza tena kuniuma na kutoa usaha uliolowanisha P.O.P, nilipoona hali imekuwa mbaya ilinibidi nimweleze baba yangu mzazi (Mzee Boniface Leo), kwamba hali yangu sio nzuri, hivyo anirudishe hospitali, Baba alikodi tena gari na kunirudisha Muhimbili.

Nilipofika Muhimbili kwenye wodi yangu ya Kibasila, wauguzi walipouangalia huu mguu wangu, ndipo wakabaini kuwa kumbe kuna makosa ya kiufundi yalifanyika.

Baada ya kugundua hilo muuguzi mmoja ambaye sikumbuki jina lake, akanifungua kidonda hicho kwa kulikata POP na hapo hapo uchafu mwingi ulitoka, ulikuwa sio wa kutazama maana ulikuwa umejaa usaha wenye halafu ya kutisha mno.

Baada ya kusafishwa kidonda, ilibidi nilazwe tena hospitalini hapo kwa kipindi cha wiki moja na nusu.

Baada ya hapo niliruhusiwa kurudi nyumbani kwa masharti kwamba niwe nafika hospitalini hapo mara kwa mara kufanyiwa "Check - Up."

Mara za mwanzo nilifanikiwa kufanya hivyo na hali ya mguu ilikuwa inaendelea vizuri pamoja na kwamba niliwekewa vyuma kwenye maungio ili goti langu lisicheze na kunisababishia maumivu.

Kwa wakati huo vyuma hivyo havikuniathiri.Kasheshe ilikuja wakati wa zile mvua za El-Nino kwani ni wakati huo ambapo vyeti vyangu vya hospitali vilipotea.

Mguu huu, kama vile ulisubiri kwanza vyeti vyangu vipotee ndipo unianzie matatizo, ulianza kuniuma kiasi kwamba hata kuunyoosha sasa nilikuwa siwezi tena.

Kwa vile sikuwa na vyeti vya kupeleka hospitali ili niweze kutibiwa bure, ilinibidi nikubali maumivu hayo kwani hata baba hakuonyesha dalili ya kunipa pesa kwa ajili ya matibabu. Alichoniambia ni kwamba nitajijua mimi mwenyewe. Sasa sijui baba alinifanyia hivyo kwa vile tayari alikuwa ameshatengana na mama au vipi!

Niliendelea hivyo hadi mwaka jana alipotokea msamaria mwema ambaye ni mwanajeshi anayeishi karibu na nyumbani,akaniambia nitafute daftari na kulitembeza kwa watu nikitafuta mchango kwa ajili ya kuanza matibabu upya.

Mungu bariki kwa kusaidiwa na rafiki yangu mkubwa aitwaye Thobias tulifanikiwa kupata sh 10,000 na hatukuchelewa. Thobias alikodi baiskeli na kunipeleka Muhimbili.

Kufika Muhimbili tuliambiwa kuwa kiutaratibu tulitakiwa kuanzia hospitali ya Wilaya ya Kinondoni-Mwananyamala, hivyo tukaambiwa hatuwezi kupokelewa hospitalini hapo.

Hatukukata tamaa. Tulienda tena Mwananyamala na huko daktari alitupatia kibali cha kwenda Muhimbili na huko sasa tulielekezwa kwenda wodi ya mifupa ya MOI.

Hapo MOI nilifanyiwa tena Check- Up na daktari aliniambia kuwa niende tena mwanzoni mwa Januari 2000, ambapo niliporudi nilitolewa vile vyuma. Pamoja na kutolewa vyuma hivyo, mguu wangu hauponi ndio kwanza unaendelea kuvimba na kutoa usaha na sasa sijui kwanini!

Kibaya zaidi ni kwamba madaktari wawili wa wodi ya MOI ambao siwafahamu majina yao walipouangalia mguu wangu walisema hata nisipokumbuka hauwezi kupona! sasa sijui kwa nini waliniambia hivyo. hadi hivi sasa mimi naishi kwa wasiwasi.

Hata hivyo, Daktari wangu Dk. Mboya, ameniambia kuwa niende katikati ya mwezi huu wa tano kwa ajili ya uchunguzi zaidi sasa sijui ataniambiaje?

Baada ya maelezo hayo Kiongozi ilihojiana na kijana Robert kama ifuatavyo:

Mwandishi: Unasema baada ya kuumwa goti rafiki zako walikukimbiza moja kwa moja hospitali. Je kabla ya kufanya hivyo walijaribu kwanza kukupa huduma ya kwanza kwa kujaribu kuligeuza geuza goti hilo?

Robert: Kusema kweli hawakujaribu kunipa huduma kama hivyo, pengine walinionea huruma maana nilikuwa nasikia maumivu makali sana.

Mwandishi: Umesema pia Baba yako alishindwa kukupa pesa pengine kwa vile katengana na mama yako.Je huyo mama yako mwenyewe kwanini ashindwe kukupatia pesa ili ukatibiwe?

Robert: Kwakweli mimi siyo kwamba namtetea mama yangu, lakini ukweli ni kwamba hakuwa na kipato cha kuweza kunisaidia kwa vile hata senti ya kumfanya apate chakula asife ni ya taabu.

Mwandishi: Je, baada ya kutoka hospitalini nami anakupatia huduma muhimu?

Robert: Shangazi yangu kanishauri nitafute kazi nyepesi nyepesi itakayo niwezesha kunipatia riziki yangu; hivyo hivi sasa pamoja na maumivu makali ninayoyapata najishughulisha na uuzaji wa chipsi.

Mwandishi: Unataka kuieleza nini jamii?

Robert: Ambacho naweza kuieleza jamii ni kwamba inisaidie na hasa mashirika ya dini yanayotoa misaada yanisaidie kwa vile Muhimbili hawajatoa uamuzi wa kimaandishi kueleza kwamba wameshindwa..Ikiwa huko Muhimbili watatamka kuwa wameshindwa basi naomba hao watu wadini na wahisani wengine wanisaidi kunipatia matibabu kwenye hospitali za nje ya nchi hii.