ZIJUE IMANI ZA WENIGINE

Changamoto ya madhehebu mengi kwa kanisa

Katoliki na Imani yetu (4)

hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu wangalikaa pamoja nasi Lakini walitoka ili

wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu" (1Yoh 2:19).Huenda ni kosa lenye heri hao wakaondoka kuliko kubaki ndani ya Kanisa wakiwa na ngozi ya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu wakali (Mt 7:15) wanaoleta uharibifu mkubwa vipo vikundi na watu nje na ndani ya kanisa vyenye sura hiyo na vinavyoharibu sura na sifa ya kanisa katoliki kwa jina la Kristo na Maria. Lazima kuviepuka vikundi hivyo.

19. Mtume Paulo akiandika kwa watu na nyakati mbalimbali amewaonya waamini dhidi ya waalimu wa uongo na kuwahimiza waizingatie imani waliyoipokea awali kiasi hata cha kulaani wapotoshaji (Gal 1:6-10). Kwa Wathesalonike kama vivyo hivyo kwetu Paulo mtume anasema 'Basi ndugu simameni imara myashike mapokeo mliyofundishwa ama kwa maneno ama kwa waraka wetu" ( 2Thes 2:15).

Yafaa kuzingatia hapa thamani ya mapokeo yaani jinsi mitume na wafuasi wa Yesu walivyoishi hapa thamani ya mapokeo yaani jinsi mitume na wafuasi wa Yesu walivyoishika imani. Ikumbukwe pia kwamba Biblia ilianza kuandikwa zaidi ya mika ishirini baada ya kifo cha Yesu; Lakini kanisa lilikwisha kuwapo likiishi Injili ya Kristo isiyoandikwa bado. Licha ya hayo Mt. Yohana anatueleza kuwa si yote aliyosema na kutenda Kristo yaliandikwa katika vitabu tulivyonavyo (Yn 2125) Hivyo ni ukaidi wa kibinadamu kukataa ukweli wa ushuhuda wa mitume na jumuia za kwanza za Kikristo kanisa lililoanza baada ya siku ya Pentekoste Mtume Paulo kwa maneno aliyowaandikia Wathesalonike anatuthibitishia kuwa Neno la Mungu twalipata toka Biblia Takatifu na mapokeo dhidi ya msimamo wa 'Sola Scriptura' (Biblia tu).

VI. Changamoto la Madhehebu lisitumike kuiishi imani na kuisoma Biblia Takatifu.

20. Agano la Kale na Agano jipya yote yanatuonyesha kuwa imani ndiyo ufunguo wa wokovu wa watu wote (Rum 1:5;3:29;Gal 3:8). Mungu amewatayarisha watu ili hatua kwa hatua wamfahamu wampende wamsadiki, wamtii na kumtegemea yeye.

Ametufunulia kwa uwazi zaidi ili tumwamini kwa njia ya Yesu Kristo ( Yh 3:11) na aonyeshe kweli anamnyenyekea na kumwungama wazi Yesu Kristu katika mawazo, maneno na zaidi sana kwa matendo mema (Rum 2:6;Yak2:14 -26).

21. Imani tuliyonayo ni zawadi toka kwa Mungu anayetupenda. Amependa kuturudisha kwake kwa njia ya mwana wake Yesu, mzao wa Bikira Maria. Huyu Yesu akawafundisha na kuagiza kwamba wote wanaomsadiki kuwa yeye ndiye njia,ya ukweli na uzima (Yn 14:6) wabatizwe (Mdo 2:37-41;Mk 16:15-16). Nao ubatizo unadai kuyageuza maisha yote yamwelekee Mungu; unadai mbatizwa aache maisha ya dhambi. Mt. Paulo anabainisha kuwa ubatizo ni kufa na kuishi upya na Kristo: "Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima " (Rum 6:2-4). Ubatizo unatutaka tusirudie kuwa watumwa wa dhambi bali tuwe watumwa wa Mungu (Rum 6:22).

22. Wakatoliki sasa wanatishwa na wahubiri wapya kuwa wamepotea na hawawezi kuingia mbinguni. Lakini mtu haendi mbinguni kwa kuwa tu mlokole au mwanachama wa kanisa fulani, ama kwa kuwa fulani kakwambia hivyo. Kufika kanisani kusoma Biblia na kuimba tu hakutoshi. Kigezo Kristo anachotupa cha kwenda mbinguni ni kumsadiki yeye na kutimiza mapenzi ya Baba wa Mbinguni (Mt 7:21). Hii inadai kuzingatia madai ya ufanisi wa Yesu yaani Upendo kwake unaodai kujikana nafsi zetu (Yn 13:34-3 5;Mt 20:37-39; 22:34-40;Lk 10:25-27), na kuacha dhambi (Lk 13:1-5)

Wengi wa waumini huasi dini baada ya kushindwa madai ya ufanisi wa Yesu na kuacha dhambi. Lakini kuingia dhehebu fulani kwa kuwa umeshindwa kuishi unavyotakiwa kwa mfano kuacha mitala ni kutafuta tu pango la kujificha ili ukatulize dhamiri inayokaidi kuishi mpango wa Mungu kuhusu ndoa kama alivyoumba tangu mwanzo (Mt 19:3-9), Mk 10:1.12). Ni kujaribu kujificha tatizo uendelee kuishi katika dhambi ukipozwa kidogo na kuwa kule kanisani usikoambiwa wazi kuacha mitala. Udhaifu wako unabaki palepale . Inashangaza kusikia kuwa watu wanatafuta makanisa ambako dhambi inaruhisiwa au kuhimizwa au ambako dhambi haionwi kuwa dhambi kwa kupidisha neno la Mungu kwa werevu (2Pet 2:1) Ukweli ni kuwa imani inaokana kwa unyenyekevu wa kukubali kuwa naishia katika dhambi na kuomba huruma ya Mungu ili anisaidie kuishinda dhambi maana mtu akiwa katika hali ya dhambi na huku anasema hana dhambi au hajatenda dhambi basi anajidanganya ukweli haumo ndani mwake na anamfanya Mungu awe mwongo (1Yoh 1:8-10).

  1. Chamgamoto la madhehebu mengi litutie

 

 

Uchaguzi wa Kisiasa kwa nini tujali?

Oktoba, mwaka huu kutakuwa na Uchaguzi Mkuu wa pili wa Rais na Wabungekatika mfumo wa vyama vingi vya siasa. Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini kwa kushirikiana na Chama cha Wanataaluma Wakatoliki wameona wanao wajibu kama vyombo vya kanisa kuwasaidia wananchi wazijue haki zao katika Uchaguzi huo na kutoka kitabu hiki ambacho tumeamua kukichapisha ili kuunga mkono hatua hiyo.

Lazima tusisahau kwamba Viongozi wanatokana na jamii. Namna Viongozi wanavyotumia madaraka na mamlaka yao inaonyesha namna ambavyo jamii ilivyo. Mambo watu wanayafikiria wanayoyasema na wanayotazamia viongozi wao wafanye ndiyo aina hiyo hiyo ya uongozi wanaoweza kujipatia.

Kama watu ni wakimya na wasiotaka kubainisha matakwa yao basi hawa watasubiri kuongozwa tu, na hivyo watachagua uongozi ambao utawaongoza kwa kuwaburuza hasa katika maamuzi na kuunda Sera. Daima hawana fursa ya kuka na watu na kujadiliana nao kwa makini. Watu ambao ni washiriki wazuri katika kuunda Sera na kuyawekea mahitaji yao kipaumbele basi watajipatia uongozi ulio tayari kuwasikiliza na kushirikiana nao katika matakwa yao.

Kama jamii ni ya watu wabinafsi ni wazi itakuwa na viongozi wabinafsi. Viongozi wanademokrasia ya kweli wanatokana na jamii ambayo ina moyo wa Kidemokrasia na inafikiria wengine pamoja na kujifikiria yenyewe.

Tunapaswa kuanzia kwetu wenyewe na kujiuliza:

Tunawezaje kuishi pamoja? Kama tunataka kuishi pamoja na kwa amani ndani ya jamii ambamo tunajaliana na kuhakikisha kuwa kila mmoja anapata nafasi halali basi tunapaswa kutafuta viongozi ambao watatusaidia kukamilisha nia hiyo. Mfano ni namna gani tunataka kuelimisha watoto wetu, kutibu na kutunza wagonjwa wetu au kusaidia maskini waliomo miongoni mwetu?

Ni sisi pekee tunaopaswa kujibu maswali hayo, kisha kutafuta watu wanaoweza kutuongoza na kutuunganisha kupanga mipango yetu kwa nia ya kufikia malengo yetu.

Lakini Je, nini kinatokea kila mara?

Huwa hatujisumbui kukaa pamoja kwa lengo la kutafakari kuona nini tunataka na kufikiri vipi tunaweza kufanikisha. Tunabaki tu kusema hiyo ni kazi ya Serikali. Lakini kwa vipi? Uzoefu unaonyesha kuwa ni kwa kiasi kidogo mno Serikali inaweza kupanga na kutekeleza kwa manufaa ya wananchi wa kawaida. Pengine mpaka ilazimishwe kufanya hivyo. Kwa hiyo ni muhimu kujiunga pamoja mapema na kutambua agenda yetu ya Maendeleo kabla ya Kampeni za uchaguzi kuanza. Bila kufanya hivyo tutaendelea kuwa na uongozi usiowajibika kwa wananchi wakiendelea kusingizia uhaba wa fedha. Huku ni kulikengeusha tatizo- kuliweka miguu juu na kichwa chini.

Lazima tuanze na sisi wenyewe. Baada ya hapo tunaweza kuangalia kwa namna gani Serikali au wawakilishi wa kisiasa wanaweza kutusaidia.

Kama tunajua mahitaji yetu, tutaweza pia kuelewa nani anaweza kutuwakilisha vema. Kama tunawajibika vema katika kusaidiana sisi kwa sisi tutaweza kwa urahisi nani tumpige kura awe kiongozi wetu.

Kama tunatafuta manufaa yetu binafsi na kushughulikia malengo ya kibinafsi hapo tutawapa kura wale ambao tunadhani watatunufaisha sisi binafsi na kushindwa kabisa kujali mahitaji ya wengine.Kuweza kuuliza uwajibikaji wa wengine sharti sisi wenyewe kwanza tuwajibike . Kutaka uaminifu wa wengine lazima kwanza sisi wenyewe tuwe waaminifu. Kutaka wema na uzuri wa wengine ni lazima tuanze kwanza kutendeana wema sisi kwa sisi.

Hivi leo tunashuhudia kuwepo kwa Rushwa kwa kiwango cha juu nchini Tanzania. Na hii ni kwa sababu watu wengi wanashiriki katika vitendo vya rushwa na kwa kufanya hivyo tunaruhusu rushwa iendelee kushamiri.

Kama sisi tusingekuwa wapenda rushwa tusingeruhusu wengine kuendeleza vitendo vya rushwa. Katika Tanzania tutaweza tu kujenga jamii nzuri kamaWatanzania walio wengi watataka na kujitahidi kuishi wema kwa matendo. Katika kufanikisha azma ya kujenga jamii njema wale wote wenye nia wanapaswa kuunganisha nguvu zao na kuzuia ubinafsi kupata nguvu na kujijenga. Na hii si kwa njia nyingine bali ni kwa njia ya kushiriki uchaguzi na katika kufikia maamuzi na uundwaji wa Sera.

Mtu binafsi kamwe hawezi kuwa mwanademokrasia kwa vile Demokrasia inapatikana katika kuwajali na kuwaheshimu wengine kwa kuwa fikra na dhamira ya kuishi pamoja vizuri, Mtu mbinafsi daima hutaka kuwatumia wengine kwa manufaa yake.

Yesu aliposema 'Mpende Mungu na Jirani yako' alitaka kutueleza na kusisitiza kuwa haya mawili yanakwenda pamoja. Hatuweza kumpenda Mungu kama hatumpeni Jirani yetu, na ni yule tu anayempenda kweli Mungu ndiye anayeweza kutenda matendo ya upendo ya jirani yake.

3 Tunawezaje kuishi dhamira hii kwa matendo?

Haya yote yanaweza kuonekana kama mahubiri safi lakini je twawezaje kuyafikia haya katika hali halisi hapa Tanzania? Wengi wetu tunaweza kucheka na kuthubutu kusema hii ni ndoto tu. utekelezaji wake hauwezekani kabisa.

Hii ni lugha ya kukata tamaa lakini tunahitaji kuliangalia jambo hili kwa makini zaidi hasa kwa sababu katika Tanzania ya leo wengi wetu hatuamini kabisa kuwepo uwezekano wa kuishi pamoja na vizuri. Hatuamini tena kama sisi ni watu walio na umoja, Tunachoamini ni kwamba tumegawanyika walio na mali pamoja na madaraka kwa upande mmoja na wale wasio na chochote kwa upande mwingine.

Lakini tunapaswa kusema sote kwa pamoja kwamba hatuhitaji jamii ya namna hiyo.Tunachotaka ni jamii ambamo kila mmoja anaheshimiwa na kupatiwa nafasi inayothaminiwa.

Jambo la pili ambalo tunapaswa kuliangalia ni namna ya kufanikisha azma hiyo. hii ndiyo hatua tunayoita uundwaji wa sera hatua ambayo tunafikiri kuwa ni muhimu kwa jamii kuweza kubainisha kipaumbele ili kujua lipi litekelezwe kwanza. Ni juu ya watu kueleza kwamba kwao kipaumbele ni jambo lipi na wataalamu wapo kuwasaidia kuweka mipango yao vizuri hivyo kwamba lengo linafikiwa.

Mara nyingi Vyama vya Kisiasa kueleza na kuandika vizuri kabla ya uchaguzi kuwa watatoa kipaumbele katika mambo gani ikiwa kama ndiyo ilani ya Chama chao. Wanachojaribu hapa ni kuteka mawazo ya watu ili waweze kupata kura zao.

Kama watu wanapigia kura Chama ambacho wanaona Ilani yake inaeleza vizuri mahitaji yao, basi ilani hiyo inapaswa kuheshimiwa na kuwa programu ya kutekelezwa na wale wanaowekwa katika Uongozi Kisiasa. Hii ni sawa kwa Chama kinachopata wingi wa kura na wawakilishi lakini vile vile kwa vyama vile vilivyopata kura chache. Wote wanapaswa kuheshimu matakwa ya wapiga kura.

Je, tunayoshuhudia yanatokea katika utendaji ndio hayo? Mfano tukichukulia uchaguzi wa 1995 na Ilani za vyama mbalimbali, je Ilani zimekuwa ndio mwongozo wa wawakilishi wa Kisiasa? au wamedharau mengi katika hayo na kutilia maanani matakwa yao binafsi na ya watu wachache au ya makundi fulani.

Mwaka 1995 nchi ilikumbwa na mambo halisi ambayo yaliletwa na matukio au hali ya kushindwa kutekeleza malengo yetu ya awali au pengine hata kwa sababu ya mabadil

Yasiyo ya Kawaida

Pamoja na kupooza mwili mzima anaendesha gari na kuendelea na shughuli za kila siku

lHutumia kitanda cha machela anapolala kifudifudi

lAnayo gari maalum isiyotumia usukani, anaye mke asiye kilema

Na Masha Otieno Nguru JR

PENGINE kama atatafutwa mtu duniani anayeishi na kufanya kazi na shughuli zake kimiujiza basi hatakuwa mwingine bali ni Kenneth Lawrance wa huko Grand Rapidan Michigan nchini Marekani.

Lawrance ambaye amepooza mwili wote mzima hawezi kusimama, kuketi wala kujisogeza hapa na pale isipokuwa kwa kutumia kitanda maalum cha Machela.

Kitanda hiki maalum ambacho Lawrance amekuwa akikitumia kwa takribani miaka 10 sasa kimerahisisha shughuli zake na kumpelekea kufanya shughuli zake kwa urahisi kana kwamba yeye ni mtu wa kawaida ambaye hana hitilafu yoyote mwilini.

Mikono na vidole vya Lawrence vinavyoweza kufanya kazi kwa kiasi fulani ndivyo humsaidia kusukuma gia ndogo zilizoko kwenye Machela yake ambavyo hatimaye hupelekea magurudumu ya machela hiyo kuzunguka.

Jarida la ‘News Week’ la Marekani lililochapisha habari za Lawrance kwenye kurasa zake linaelezea ni kwa namna gani ‘kilema’ huyu humudu kushughulika sawa na mtu awaye yeyote mwingine wa kawaida awapo juu ya machela.

Anapotaka kuendesha gari machela yake hubebwa na kupakuliwa humo. Kisha yeye mwenyewe akabebwa na kulazwa humo ‘kifudifudi’ hapo kwa kutumia mikono yake Lawrance huwasha gari lake lisilo na usukani ambalo linaendeshwa tu kwa kutumia ‘Remoter controler maalum’.

Anapofika mahala alipotaka kwenda anashushwa na machela yake yenye magurudumu halafu kwa kutumia mikono yake huiendesha hadi mahali anapotaka kuingia kama ni ofisini, dukani ama ni sokoni. Hufanya vivyohivyo hata aingiapo Kanisani.

Kwa baadhi ya watu wasiomjua Lawrance kushituka sana wamwonapo kwa mara ya kwanza akisafiri na kuvinjari mitaani mchana huku kalala kifudifudi juu ya machela.

Nchini Marekani mpaka sasa Lawrance ameamsha gumzo kuwa kumbe mlemavu hata awe wa aina gani upo uwezekano wa yeye kuendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa na maendeleo yake binafsi na kinachotakiwa tu ni atengenezewe mazingira na vifaa vinavyoweza kumrahisishia utendaji wake wa kazi kama Lawarance alivyotengenezea gari maalumu na vifaa maalum.

Mkewe Bw. Lawrance ni mama mpole wa kawaida asiye mlemavu kama mumewe. Bi. Maryilin Lawrance kitaaalumani mwalimu wa Elementary School huko Grand Rapidan Michigan tofauti na mumewe ambaye siku zote kabla na baada ya kupooza ni mtaalamu wa kompyuta.

Umri wao umeisha kuwa mkubwa, Lawrance anayo miaka 45 wakati mkewe Marylin ametimiza miaka 40 sasa. Lakini watu hawa katika umri huo wa makamo wangali wakiendelea kuishi pamoja kwa kushirikiana katika maisha yaliyojaa furaha lakini ya miujiza.

Wamezaaa watoto watatu Tanya, Clarkson na Twan. Binti yao Tanya ameisha olewa na watoto wao wawili wa kiume tayari wamemaliza chuo kikuu na wanafanya kazi.

Mkewe Lawrance anasema kuwa yeye haoni mzigo wala uzito wowote kuishi na mume aliyepooza mwili wote.

"Ni binadamu wa kawaida sawa na wengine hanipi shida na anachuma pato kubwa kuliko mimi mkewe"

Wamefanikiwa kujenga jumba la kifahari huko Michigan Lawrance pamoja na kazi zake za ofisini pia ni mtetezi wa haki za watu, ameanzisha chama cha kuhakikisha jamii inawawekea mazingira yanayowawezesha kumudu maisha kama watu wengine pamoja na masaibu waliyo nayo.

Maisha na Mikasa

KIJANA WA MLANDIZI AKUMBANA NA KASHESHE DAR NA KUSEMA:

Aliyetaka kunisaidia ndiye aliyesema nikipiga kelele wataniua

lMwenzake akanisogezea kisu shingoni

Dar Es Salaam ni jiji kubwa na lenye wakazi toka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi. Kila mmoja akiwa na tabia yake. Wapo wanaoonekana wa kutisha lakini sivyo walivyo.

Wapo pia wanaovaa ngozi ya kondoo kumbe ni mafisi wenye uchu wanaosema kufa kufaana. Wote hao wanastahili kuogopwa "kama ukoma". Mwandishi Josephs Sabinus, alikutana na kijana toka Mlandizi, aliyeangukia mikononi mwa "mafisi" hao na alipokuwa akitafuta msaada wa maelekezo kutokana na ugeni wake jijini. Mwanamke aliyemnusuru anaeleza alivyokutana naye:

"Alipofika, alisimama; akawa ananiangalia toka kule juu, nikasema huyu anayeniangalia hivi ni nani. Akanisalimia na mimi nikaitika.

Akasema, "mama, naomba chakula chochote kilichopo ninakufa kwa njaa. Nikashangaa; nikamuuliza wewe unayeniomba chakula hapa Dar es Salaam umetoka wapi?"

Anaelezea Mama Mary, mkazi wa Keko-machungwa jijini Dar es Salaam na kuendelea, "Nilipozidi kumuuliza zaidi akanieleza aliyokutana nayo; nikaamua kumpa kilichopo. Hivi vyakula ni vitu vya kupita tu, si vya kumnyima mwenye shida."

Baadhi ya watu waliomshuhudia kijana huyo anayeitwa Faraja Mshamu (18),ambaye hivi karibuni alitoka Mlandizi, Mkoani Pwani, kumtafuta kaka yake aende kumsaidia mdogo wao aliyekuwa amepelekwa katika hospitali ya Tumbi, mkoani hapo na kisha akakumbwa na masaibu mengine mengi, wakamtaka aeleze yaliyomkumba.

Yeye mwenyewe akasimulia aliyokumbana nayo katika jiji la Dar es Salaam lililojaa kila aina ya unyama pasipo utu wala huruma; akasema:

"Siku hiyo, usiku, mdogo wangu Saida aliugua ghafla usiku, tena usiku mzima hatukulala, sijui alikuwa na malaria, hata mimi sijui vizuri; niliacha wanampeleka hospitalini pale Tumbi, Kibaha".

"Baba na mama wakaniambia nije Dar es Salaam kumuita kaka yetu... anaitwa Saidi Mshamu. Nilipofika Keko-makugurumbasi ambapo alikuwa anaishi, wakasema eti alisha hama," akasema kwa sauti ya huzuni huku akionesha hofu.

Watu walipomuuliza kuwa huyo kaka yake anafanya kazi gani, kijana huyo wa kabila la Wangido aliyehitimu elimu yake ya msingi katika shule ya Mtongani huko Kibaha Mkoani Pwani, mwaka 1998, akasema,

"Alikuwa anauzauza vitu mikononi, nguo, pasi,na vyombo vya ndani; huwa anatembeza tembeza tu.( Mmachinga)"

Akaendelea kusimulia huku mara kwa mara machozi yanamlengalenga na wakati mwingine kushindwa kuyazuia yasitiririke. Akazidi kusema, "Nilipomkosa pale nyumbani, nikaanza kuulizia kwenye miji kuanzia kule juu.

Nilizidi kuulizia tu, maana wengine waliniambia eti labda nijaribu inawezekana amehamia huku Keko-machungwa.

Wakati nilipokuwa ninaelekea kule barabarani, nikakutana na kijana mmoja.

Akaniuliza ninatatufa nini nikamwambia nimetokea Mlandizi namtafuta kaka."

Nilipomuelezea jina lake, akasema anamfahamu, hivyo nimsubiri amuage mwenzake anipeleke anapoishi kaka yangu Saidi."

Huku tena sauti yake ikawa na kigugumizi kilichoashiria kulia wakati wowote, akawaangalia kwa woga watu waliokuwa wakiongezeka pale kumshuhudia huku ameketi ukutani kwa Mama Mary, baada ya kula chakula alichopewa na Msamaria huyo.

Faraja aliendelea kusimulia,

"Tukaenda, tukaenda tulipokaribia kule bondeni, mwingine akatokea mbele yetu.

Alipofika kwetu(walipokutana), akatoa kisu na yule ambaye tulikuwa naye akaniambia eti nikipiga kelele wananiua hapo hapo.

Wakati huo yule mwingine ananisogezea kisu shingoni.

Yule tuliyekuwa naye akaanza kuingiza mikono mifukoni akachukua shilingi 2000/= ambazo nilikuwa nazo za nauli yetu mimi na Saidi, maana baba alisema eti hata nikimkuta Saidi tuondoke haraka na hata kama hana hela nimlipie, twende haraka nyumbani.

Kisha yule mwingine naye akanitishia kuwa nikipiga kelele wananiua, wakanivua viatu nilivyokuwa nimevaa na mkanda wangu wakanivua."

Alipoulizwa kuwa mbona hawakumchukulia nguo alizovaa ingawa zilikuwa nzuri na mpya, kwa uchungu Faraja akasema, "walitaka kunivua hata hii suruali(anaonesha suruali yake aina ya jeans), lakini wakaona watu wanakuja njiani wakakimbia".

Akaendelea kusimulia kisa hicho kilichowahuzunisha watu wale waliosikiliza. Huku wakiwalaani wahuni wa jiji hili

Akasema, "Nilipotoka hapo nikaenda kwenye mji mwingine kuwauliza wanioneshe polisi ilipo, niende kuwaomba msaada kulala kwa kuwa sikuwa na hela nyingine na sijui niende kulala kwa nani.

Wakaniambia niende kwenye kile kituo barabarani pale wanapochonga vinyago (anamanisha kituo kidogo cha polisi cha Mivinjeni).

Nikawakuta polisi wawili nilipowaelezea wakasema eti nitajua mwenyewe. Wakasema Eti mtu haruhusiwi kulala pale, nitoke pale nitajua mwenyewe.

Nikaogopa kwenda pengine wakawa wananifukuza mimi nimenyamaza tu, mpaka wakaniacha nikalala kwa kulazimisha lazimisha tu. Nililala pale mbele mpaka asubuhi"

Kijana huyo anayeishi na wazazi wake Bwana na Bi. Mshamu Mohamed ambao ni wakulima hapo Mlandizi anasema ingawa hajui dada mdogo wake aliugua nini ghafla namna hiyo akaacha wakimpeleka katika Hospitali ya Tumbi huko Kibaha, anawaomba wote wenye mapenzi mema wamuombee ndugu yake apone na kwa hali yoyote na mali.

"Ingawa sijui kama nitamkuta lakini ..."

"Huku machozi yakimlengalenga, Faraja akasema, "Jamani kama mtu atasikia alipo naomba amwambie awahi nyumbani."

Gazeti hili lilimshuhudia msamaria mwema huyo licha, ya kumfadhili kwa chakula kama alivyoomba, Mama Mary akampa sh. 900/= kwa ajili ya kumrudisha nyumbani kwao Kibaha maeneo ya Mlandizi huku mama huyo akisema,"Kama anadanganya, shauri zake, ninafanya kumfurahisha Mungu" Moyo wa mama huyo Mwenyeji wa Musoma hauna budi kuigwa.