Kuwaelimisha watoto wapende kufanya kazi za nyumbani

WATOTO wadogo wanapoona wazazi wanasafisha nyumba, kufua nguo na kupika chakula, hupata shauku kubwa sana ya kuwaiga wazazi wao kufanya kazi hiyo, Lakini wazazi wengi zaidi hawafahamu mahitajio yao . Wanadhani watoto hawana haja ya kufanya kazi, baadhi yao wanahofia watoto wataharibu vitu au kuchafuaa nguo zao. Kwa hivyo wakati wanapofanya kazi huwakataza watoto au kuwaambia watoke nje kucheza. Katika hali ya namna hii watoto hushindwa kufanya kazi za nyumbani bila idhini ya wazazi wao. kama wakishindwa kufanya vizuri kazi fulani watakaripiwa au kushutumiwa na wazazi . Kufanya hivyo kutadhoofisha juhudi ya watoto. Watoto wanapokuwa wakubwa ingawa wana uwezo wa kufanya kazi hizo za nyumbani lakini wanakosa hamu tena. Sababu ni kwamba kwa kadiri ya umri wa watoto unavyozidi kuwa mkubwa ndivyo shughuli zao zinavyozidi kupanuka, wanapata hamu nyingine mpya na kupenda kushirikiana na watoto wa rika lao. Wazazi baada ya kurudi nyumbani kutoka kazini hufikia baada ya kurudi nyumbani kutoka kazini hufikia kazi ya kusafisha mboga na kupika chakula. Kama wazazi wanawataka watoto wao ambao wanarandaranda chumbani wafaye kazi hii au ile hawaoni furaha hata kidogo, hivyo wazazi hupandwa na hamaki, pengine huweza kusababisha kukosana baina ya wazazi na watoto. Kwa watoto wenye desturi ya kufanya kazi tangu utotoni wanapokuwa huwa wamekwisha jenga tabia ya kupenda kufanya kazi kwa furaha bila ya usununu. Ukikosa fursa hii ya kuwaelimisha watoto kufanya kazi tangu utotoni, basi ni shida sana kwao kuweza kufanya hivyo baadaye. Kwa kupitia kujiamulia kufanya kazi za nyumbani mtoto huweza kuishi na kusoma katika mazingira mazuri na kujua kwamba kufanya kazi ni jambo la kufurahisha. Tunatoa mapendekezo kama yafuatayo ili kuwapa wazazi mwangaza wa njia ya kuelimisha watoto wapende kufanya kazi za nyumbani.

A. Wazazi hawana budi kutosheleza mahitajio ya kisaikolojia ya watoto na kuwafundisha kufanya kazi za nyumbani hatua kwa hatua kuanzia kazi rahisi hadi kazi ngumu ili kuwajengea tabia ya kufanya kazi.

B: Watoto wakishughulikia kazi za nyumbani mapema zaidi, huleta mafanikio makubwa zaidi katika kujenga tabia ya kufanya kazi.

C. Kuwaelimisha watoto kufanya kazi za nyumbani kunaweza kuanza kutoka kazi za kujihudumia hadi kazi za nyumbani. Kutokana na kazi hizo watafahamu kuwa kazi ni mahitajio ya maisha na kwamba ni jukumu la lazima kwa kila mtu katika familia.

D Tunapowaelimisha watoto wafanye kazi tusiangalie tu matokeo ya kazi yenyewe bali ni kutilia mkazo juu ya maana ya kazi. Maana yake ni kwamba pengine kazi zenyewe hazitokusaidia chochote, lakini zinaleta faida kwa kujenga tabia nzuri ya watoto.

E. Wazazi wanapowapangia watoto kazi hawana budi kutilia maanani namna ya kuchangamsha hamu ya watoto na kuwahimiza watoto watumia akili ya kufanya juhudi ili wafanye kazi vizuri. Tukigundua uvumbuzi wa watoto itatubidi tuwasifu kwa wakati.

F. Ongeza aina za kazi kwa kufuata umri wa watoto, himiza watoto wafanye kazi kwa ajili ya wengine ili watoto wawe na tabia nzuri.

G. Mafundisho ya kazi na uadilifu yanatakiwa kuanza kwa pamoja ili watoto wafahamu vilivyo maisha mazuri ya watu yanategemea mchango wa watu kwa jamii na wafahamu namna ya kushirikiana vizuri na watu wengine katika kazi za pamoja.

 

ZIJUE IMANI ZA WENGINE

Changamoto ya madhehebu mengi kwa kanisa Katoliki na Imani yetu (3)

kichungaji wa Petro na mitume wengine huunda moja ya misingi ya Kanisa. Kazi ya Petro na mitume ilipaswa kuendelea daima bila kukatishwa hadi atakaporudi Bwana. Kazi hiyo inaendelea kwa njia ya daraja ya uaskofu kwa mfululizo usiokatika (LG 20) tangu mitume wa kwanza. Kwa bahati mbaya wapo waliovunja na wanaovunja urika huo na umoja huo kwa kujitenga na kuanzisha vikundi vinavyoitwa kwa majina ya waliovianzisha au mengineyo.

iv Maonyo ya Kristo

15. Ni wajibu wetu kuwakumbusha waamini hasa wale wafuasi wa Kristo ambao wamekwisha naswa na udanganyifu au na kishawishi cha kupotolewa katika imani juu ya maonyo ya Kristo. Tumeuvunja mwili wa fumbo wa Kristo na kuunda miili mingine na mazizi mengi kwa sababu ya kutozingatia maneno ya Kristo. Na ili kutuliza dhamiri kwa kosa la kuvunja umoja wa ZIZI la Kristo (Kanisa) wengine husisitiza zaidi kuwaita Wakatoliki 'Waroma' ili kanisa Katoliki lionekane sawa na madhehebu mengine. Hiyo ni tafsiri potovu ya kuleta ulinganisho usio sahihi pia. Kanisa Katoliki siyo 'dhehebu' la Kilatini kwa Wakatoliki walio chini ya Askofu Mkuu wa Roma, au la mashariki kwa Wakatoliki walio chini ya Mapatriaka. Hatuna budi Wakristo kumwomba msamaha Kristo na kutafuta kurudisha umoja alioutaka tukizingatia maonyo aliyowapa watangulizi wetu.

Maandiko Matakatifu yanatupa maonyo hayo ya Bwana wetu Yesu Kristo yafaa kurejea mifano michache. Wanafunzi wake walipomuuliza ni lini Yerusalemu na Mahekalu vingevunjwa na dalili gani zitatuonyesha kuja kwake mara ya pili na mwisho wa dunia, Yesu alimwambia 'Angalieni mtu asiwadanganye kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu wakisema 'mimi ni Kristo' nao watadanganya wengi. Na manabii wengi wa uongo watatokea na kudanganya wengi. Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho ndiye atakayeokoka" (Mt 24:4 -13).

Na akiwatahadharisha juu ya taabu kubwa ambazo zitakuwapo nyakati za mwisho alisema "Wakati huo mtu akiwaambia Tazama Kristo yupo hapa" au 'Yupo Kule' msisadiki kwa maana watatokea wakristo wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu wapate kuwapoteza , kama yamkini hata walio wateule. Tazama nimekwisha kuwaonya mbele"(Mt 24:23-25). Maonyo hayo ya Kristo yanakutwa pia katika Injili za Marko (13:5-6,21 -23) na Luka (17:20 -23). Na kwa hao wanaosababisha upotovu wa wale waliokwishaipokea imani iliyojengwa juu ya mitume Kristu anatutangaza mwisho wao kwa maneno haya: "Si kila mtu aniambiaye Bwana Bwana atakayeingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ili 'Bwana Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako, kwa jina lako kutoa pepo, kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri si kuwajua ninyi kamwe ondokeni mwangu ninyi mtendao maovu" (Mt 7:21-23)

V. Maonyo ya Mitume

16. Baada ya Kristo, kazi ya kuutangaza ujumbe wa Kristo iliendelezwa na Mitume na baada ya mahalifa wao. Hatari ya uzushi wa uasi imekuwepo tangu nyakati hizo ndio mwanzo wa mitaguso kama ule wa Yerusalemu (Mdo 15:1 -29) na yote iliyofuata, ikiwaleta, ikiwakusanya pamoja 'Mitume na wazee' wa kanisa ili kwa pamoja watafakari juu ya matatizo yanayowagusa waamini na kutoa mafundisho sahihi ya imani kama walivyopokea toka kwa Kristo.

17. Kanisa kadiri lilivyokua uzushi na mafarakano vilijitokeza. Hivyo imepelekea wenye dhamana ya kulinda imani waendelee kutoa maonyo na kusahihisha upotovu . Yafaa kurejea kwa mifano ya mitume tunayoikuta katika Agano Jipya. Petro mtume na mkuu wa mitume hakukawia kuwausia wakristo wote wajue kigezo cha usahihi wa mafundisho akisema: "hakuna unabii katika maandiko upato kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu bali wanadamu walinena yatokayo kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu " (2Pet1:20-21)

Hapo ndipo tunatambua nafasi na thamani ya UALIMU WA KANISA (Mamlakafunzi); tunaelewa kwa nini walifanya mtaguso wa Yerusalemu na mitaguso mingine kama ya Efaso,Trento na Vatkanina ndiyo maana tunaonywa na Mt. Yohana kuwa tusimsadiki kila anayeamka na kudai anaye Roho Mtakatifu .Anasema "wapenzi msiiamini kila roho bali zijaribuni hizo roho kwamba zimetokana na Mungu kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani hao ni wa dunia kwa hiyo wanena ya dunia na dunia huwasikia" (1Yoh 4:4,5).

  1. Mtume Petro alituonya dhidi ya waalimu wa

Uchaguzi wa Kisiasa kwa nini tujali?

Oktoba, mwaka huu kutakuwa na Uchaguzi Mkuu wa pili wa Rais na Wabungekatika mfumo wa vyama vingi vya siasa. Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini kwa kushirikiana na Chama cha Wanataaluma Wakatoliki wameona wanao wajibu kama vyombo vya kanisa kuwasaidia wananchi wazijue haki zao katika Uchaguzi huo na kutoka kitabu hiki ambacho tumeamua kukichapisha ili kuunga mkono hatua hiyo.

UTANGULIZI:

Chaguzi za kisiasa ni muhimu sana katika ujenzi wa Demokrasia

Mwaka 1995 Tanzania tuliingia hali mpya ya Kisiasa kwa kufanya uchaguzi wa kwanza katika mfumo wa Siasa ya Vyama vingi. Kulikuwa na hamasa na matamanio makubwa kufuatia mabadiliko hayo. Hata hivyo matokeo na matukio kadhaa yaliyotokea baadaye nchini na katika vyama vya Siasa yamefanya watu wakate tamaa. Sasa watu wanajisikia kwamba Vyama na Viongozi waliochaguliwa wameshindwa kutekeleza ahadi zao, hivyo Ilani za uchaguzi zilitumika tu kama njia ya kuwavuta watu kuwapigia kura. Heshima na Umaarufu wa Viongozi wa Kisiasa umeshuka kwa kiasi kikubwa. Haya sio maendeleo mazuri, Kwa hakika hali ya kukata tamaa na kutoaminiana ndiyo msingi mkuu wa kuwepo uongozi uliojaa Rushwa.

Kama jamii ya Kikristu hatuwezi kukubali hali hiyo na kuridhika nayo. Tumeitwa na Mungu kushiriki kujenga Ufalme wake hapa Duniani kwa kuimarisha na kuendeleza yaliyo mema na kuyapiga vita maovu yote.

Tumeitwa kushiriki kuendeleza uumbaji pamoja na Mungu ili kuifanya nchi yetu iwe mahali pazuri pa kuishi. Kwa hiyo tuna wajibu wa kushiriki kikamilifu katika maisha ya Taifa letu- Kisiasa na Kijamii pia. Ushiriki huo haukomei katika uchaguzi tu bali ni muhimu pia katika kufikia maamuzi juu ya sera na mfumo wa namna gani nchi yetu iongozwe.

Kijitabu hiki kinalenga kuwasaidia wale walio tayari kujitoa kuwa wahamasishaji na waelekezaji katika jumuiya mbalimbali ndani ya jamii yetu.

Tunahitaji watu wanaovutwa na kushawishika wakiongozwa na imani yao ya Ukristu kujitoa mstari wa mbele, kuwa tayari kujiwajibisha wenyewe katika kazi hii ya kuwaamsha watu watambue jukumu hili muhimu la kushiriki kikamilifu katika shughuli za Kisiasa ndani ya nchi yetu. Hivyo sote kwa pamoja tuweze kusaidia kulinda amani na kuhakikisha fursa za maendeleo zinapatikana kwa wote.

Nachukua nafasi hii kuwashukuru wana-CPT (Christian Professionals of Tanzania) na wale wote ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakijitahidi kushughulikia mambo haya.

Mh. Askofu Paul Ruzoka

Askofu wa Kigoma

na

Mwenyekiti wa Tume ya Haki na Amani-TEC

Februari,2000

SEHEMU YA 1-MAELEZO YA JUMLA

1. Kwa nini tujali Uchaguzi wa Kisiasa?

Uchaguzi wa 1995 ulitegemewa uwe wa aina yake kwa vile ulikuwa unatoa fursa kwa vyama vingi kupigiwa kura. Watu wengi wa kawaida walishiriki uchaguzi wakitarajia kujipatia Viongozi waliowataka. Mara tu baada ya uchaguzi watu wakabaini kwamba hakuna mabadiliko makubwa yaliyotokea. Wanasiasa waliochaguliwa wanaonekana kushughulikia matakwa yao binafsi au sanasana maelekezo ya vyama vyao badala ya kutilia maanani na kuweka mikakati ya kutekeleza mahitaji ya watu katika maeneo/majimbo yao. Hawana nafasi ya kutembelea Majimbo yao na kukutana na watu wao mara kwa mara kuweza kupata maoni yao na wala hawana nafasi ya kusikiliza malalamiko na matarajio ya watu wao.

Baadhi ya watu sasa wanaanza kuwachoka wanasiasa na vyama vya Kisiasa. zaidi na zaidi watu wanaelekea kuamini kuwa Siasa ni mchezo mchafu na hivyo wale wanaojihusisha na uchaguzi na hasa wagombea hufanya hivyo kwa manufaa yao binafsi.

Hii siyo tabia ya Kikristu kwa sababu kuwa Mfuasi wa Kristu ni kushiriki kazi ya kubomoa kwa kumsaidia binadamu aweze kupambana na uovu pamoja na ubinafsi.

Sote tunaelewa kuwa wakati mwingine Siasa huambatana na matumizi mabaya ya madaraka kutokana na uovu na mvuto wa kutimiza malengo yao binafsi. Lakini Mamlaka na Uongozi vyaweza pia kuwa fursa ya kutumikia wengine na kuleta manufaa kwa wote na hivyo kusaidia kujenga jamii kuwa mahali bora pa kuishi kwa pamoja na vizuri kama Wakristu tumeitwa na Mungu kushirikiana naye kuifanya dunia na nchi yetu kuwa mahali ambamo jamii inajaribu kuishi kadri ya matakwa na mpango wake.

Sisi ni sehemu ya jamii ya Tanzania kwa hivyo hatuwezi kuikimbia hali halisi kwa kujificha makanisani tukisali kuomba maovu yaondoke.

Mungu ametufanya tuwe washirika na wadhamini wake katika kuwashirikisha wanadamu kazi ya uumbaji na kuifanya dunia iwe na utu hivyo kwamba panakuwa mahali pazuri pa kuishi.

Kwa hiyo basi hatuwezi kufumbia macho mambo yanayoendelea katika Siasa, hatuwezi kukaa pembeni wakati huu na maandalizi ya uchaguzi wa Oktoba 2000. Tunatakiwa kuwa watoto wa Mwanga ili tuweze kuona yapi ni mema na yapi ni maovu.

Tunaitwa kushiriki katika chaguzi hizo, sio tu kama wapiga kura bali pia katika kulinganisha na kubainisha mambo ya kupewa kipaumbele na wanasiasa wetu katika miaka ijayo. Hatupaswi kupiga kura na kuishia hapo tu bali tunapaswa pia kuwambia wanasiasa ni namna gani tunawataka waongoze nchi yetu.

Demokrasia inamaanisha madaraka yamo mikononi mwa watu na hii sio katika kupigia kura viongozi tu, bali pia katika kuwaambia viongozi hao nini cha kufanya na namna gani yafanyike ili kuleta manufaa na ustawi wa jamii nzima.Wanasiasa ni watumishi wa watu. Kama hawatumikii watu, inabidi wapigiwe kura ya kutokuwa na imani nao na waondolewe madarakani.

Kama Wakristu tunaitwa kuathiri shughuli za Kisiasa hivyo kwamba ziweze kuhudumia jamii kulingana na matakwa na mpango wa Mungu. Huku ndiko tunakoita kujenga Ufalme wa Mungu ikimaanisha kwamba kuishi na kuridhishwa nayo.

2. Tunawezaje kutekeleza hayo?

Tatizo kubwa la Watanzania ni kulalamika juu ya wengine kila mara wengine ndio wa kulaumiwa yaani Serikali Chama Tawala, Vyama vya Upinzani, Magazeti, redio, Kanisa Wafadhili na Benki ya Dunia. Na hii inaelekea kuwa tabia-Kila mara lawama kwa wengine.

Kama tukiendelea hivi kamwe hatutafanikiwa kujenga Demokrasia. Demokrasia ya kweli inaanzia na mimi, Demokrasia ya kweli inaanzia na sisi.

Demokrasia ya kweli kwanza kabisa huanzia kwa kujengwa ndani ya mioyo na akili za watu. Ni fikra zetu na msukumo wetu wenyewe ndivyo vinavyoweza kujenga Moyo na Utamaduni wa Kidemokrasia.

Bila Moyo na utamaduni wa Kidemokrasia, ni kazi bure kuwa na vyama vingi vya Kisiasa ama watu wanaogombea uchaguzi. Hawa hawatasaidia jamii wala hawatahudumia kwa manufaa ya wote hatuwezi kamwe kuwa na demokrasia ya kweli, tutakachobaki kuwa nacho ni siasa za kutafuta na kugombea madaraka yaani kuwa na uongozi wenye ubinafsi wa fedha na madaraka.

Yasiyo ya Kawaida

Machimbo ya Farao kufunguliwa baada ya kufungwa kwa miaka 6000 sasa

lSehumu kubwa ya dhahabu imefukiwa na mchanga jangwani

lHuenda yakatoa dhahabu kupita machimbo mengine yote duniani

Na Masha Otieno Nguru JR

KWAKO wewe waweza kuona miaka 6000 ni mingi sana. lakini hivyo sivyo ilivyo kwa Sami El - Raghy Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni moja ya Australia ya kutafuta na kuchimba madini.

Katika hali ya kushangaza na inayochukuliwa na wengi kuwa haiwezekani kutokea kampuni hiyo imejitosa jangwani huko Misri ili kutafuta yaliyokuwa machimbo ya dhahabu ya aliyekuwa mtawala wa Misri kwa miaka mingi Farao.

Jambo hili bado linaonekana kama ndoto machoni pa walimwengu kwa sababu ni miaka mingi toka machimbo hayo ya mfalme Farao yalipofungwa na Mchanga mzito wa Jangwani tayari umefunika sehemu iliyokuwepo machimbo hayo huko Jangwani kiasi cha kupelekea isiwe rahisi kuyatambua yalipo tena.

Machimbo hayo ya dhahabu inasimuliwa kuwa yamesheheni hazina kubwa ya thamani ambayo pengine hata 'Mto Nile' haujapatia Misri kwa kiasi hicho.

Dhahabu iliyolala humo jangwani kwa miaka mingi inaelezwa na wataalamu wa mambo ya kale kuwa ni ile ya daraja la Kwanza na haiwezi kufananishwa na inayotoka katika machimbo yoyote yale duniani kwa sasa.

Hii ni kumaanisha kuwa hata yale machimbo ya dhahabu ya Afrika Kusini kule Witwatersrand dhahabu yake haifui dafu kwa hii iliyofichwa na Farao kwa miaka mingi.

Zama za utawala wa Farao vitu vingi vya thamani na mapambo ya dhahabu aliyotumia yalitokana na machimbo hayo ambayo baadaye aliyafunga na kuyaficha.

Hakika Mafarao waliopata kutawala Misri walikuwa wengi na walifanya hivyo kwa vipindi tofauti.

Pengine utajiuliza kuwa ni Farao yupi aliyeyafunga machimbo haya basi huyo alikuwa ni yule Fharao Menes ambaye ndiye aliziunganisha Misri mbili 'LowerEgypt' na 'Upper Egypt' kuwa kitu kimoja.

Kwa miaka mingi toka wakati huo suala la dhahabu nyingine kuwepo Misri lilichukuliwa kama ni hekaya tu, hadi hivi karibuni kampuni hii ya Australia ilipoama kubadili dhana hiyo na kutangaza rasmi kuamua kuisaka Dhahabu ya Farao kwa udi na uvumba kisha kuichimba.

Kihoja ni kuwa hata kampuni hiyo ya Australia inayojigamba kuwa itafukua dhahabu iliyofichwa na Farao mpaka sasa bado haijui kabisa ni sehamu gani hasa katika jangwa hazina hiyo imesetirika.

Kulingana na jarida mashuhuri la The Wall Street Journal Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya madini Bw. Sami El- Raghy ameeleza kuwa Serikali ya Misri imetoa kibali kwa kampuni yake kuanzia kazi hiyo Mashariki mwa jangwa karibu kabisa na bahari ya Red Sea ambako baadhi ya wazee wa kali waliohojiwa wamesimulia kuwa huenda ndiko machimbo hayo yapatayo 16 ya Farao yalikuwepo.

Lakini Ramani ya kale kabisa yenye umri wa miaka 2900 iliyogunduliwa na wataalam wa mambo ya kale huko 'Luxor' (Jhebes ya Kale) imeonyesha kuwa yapo machimbo mengine ya ziada 104 ya Farao ambayo pia hayajulikani yalikopotelea.