Manufaa ya kazi za nyumbani kwa mtoto

BAADHI ya wazazi wanatia mkazo juu ya masomo ya watoto, lakini hawajali umuhimu wa kazi za watoto wao, hawataki watoto wao kugusa kazi za nyumbani hata kidogo, hasa watoto wanaosoma katika darasa la kwanza na la pili bado wanalishwa chakula na kusaidiwa kuvaa nguo. Wazazi hao wanaona kwamba kazi za nyumbani zinaweza kukawiza masomo ya watoto. Lakini hawajui kwamba kazi za nyumbani zinaweza kusaidia hodari zaidi.

A. Kazi za nyumbani zinaweza kuwafundisha watoto uwezo wa kuhesabu na kupanga vitu taratibu.

Mawazo ya watoto wenye umri wa miaka 4-5 hivi hupatikana kwa kupitia kusikia na kuona na kazi ya nyumbani husaidia kujenga msingi wa ukuaji wa mawazo ya watoto. kwa mfano kabla ya kula chakula wazazi wanaweza kumwambia mtoto aende jikoni kuchukua mabakuli na vijiko kwa mujibu wa idadi ya watu, kisha awagawie. Kutokana na kazi hiyo mtoto anaweza kujifunza hesabu. Baada ya kula chakula mtoto anaweza kusaidia watu wazima kusafisha meza, mabakuli na vijiko. Kazi hii inafundisha mtoto kupanga vitu vya aina mbalimbali kwa utaratibu. katika kazi hiyo ya kawaida, ukuaji wa uwezo wa akili wa mtoto unakuwa umepata maendeleo vya kutosha.

B. Kazi za nyumbani zinasaidia watoto kukuza uwezo wa mawazo.

Watoto wakiwa wakubwa kidogo, wanaweza kufanya kazi ngumu kidogo ili kuinua uwezo wao wa mawazo. kwa mfano kazi ya kupika ni ngumu kidogo kwa mtoto. Inaanzia kusafisha kukata, kutumia mafuta, kuwasha moto..inawabidi wajue namna ya kupika vizuri katika muda mfupi. Kazi hiyo inahitaji kujua taratibu ya kazi na utumiaji wa moto. Katika kazi hiyo mawazo ya ubongo na matendo ya mikono yanashirikiana na kupelekeana taarifa ili kufanya kazi vizuri, na wakati huo uwezo wa kuleza mambo. Watoto wanapofanya kazi za nyumbani kwa kutumia akili na mikono wanapanua upeo wa macho, wanapata ujuzi na maarifa. Ikiwa wazazi wanazingatia jinsi ya kuwafundisha watoto kusema, wanaweza kumtaka mtoto aeleze kidogo juu ya kazi, basi mtoto haoni shida ya kusema.

Imedhihirika kwamba kazi za nyumbani zinaweza kuwafanya watoto wawe hodari zaidi. Mtaalamu maarufu wa elimu wa Urusi alifichua siri katika upande wa saikolojia: "Kwenye ubongo wa binadamu kuna maneno maalum yenye juhudi na uvumbuzi ambayo yanaweza kuchochewa na kuchangamka kwa juhudi na uvumbuzi ambavyo wanaweza kuchochewa na kuchangamka kwa juhudi kwa kutegemea ushirikiano wa mawazo na matendo ya mikono, hivyo watoto wanaweza kuwa hodari katika kufikiri" Zaidi ya hayo, kutokana na kazi za nyumbani, watoto wanapata tabia nzuri ya bidii, juhudi, makini na kutoogopa shida. Tabia hizo zinanufaisha masomo ya watoto.

Kazi za nyumbani pia zina maana kubwa katika kufundisha hisia za watoto. Mtaalamu mmoja wa filosofia wa Ugiriki aliwahi kusema kwamba ikiwa watoto hawataki kufanya kazi,basi hawatoweza kujifunza vizuri lugha, muziki, sanaa na michezo , Wazazi tuwaache watoto wafanye kazi za nyumbani.!

 

 

ZIJUE IMANI ZA WENGINE

Changamoto ya madhehebu mengi kwa kanisa Katoliki na Imani yetu (2)

Mtakatifu Mungu mmoja kadiri ya mafundisho ya Mitaguso yote Mikuu kamwe haabudiwi kama Mungu bali anatukuzwa kwa heshima ya pekee anayostahili (LG 52) kwa kujali nafasi yake katika mpango mzima wa wokovu kama alivyoupanga na kuutekeleza Mungu mwenyewe.

11 Tunaamini pia kwamba Roho Mtakatifu ni Mungu na Mungu hawezi kufungwa na mtu kiumbe! Na Kristo mwenyewe ametuthibitishia kuwa wote wanaomsadiki wakazaliwa mara ya pili kwa maji na Roho (Yn 3:8) wanaye Roho Mtakatifu. Mtume Paulo pia anadhibitisha kuwa wote waliomwongokea Kristo miili yao ni mahekalu ya Roho Mtakatifu (1kor 6:19). Na wale wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio wana wana wa Mungu (Rum 8:14). Lakini haitoshi kudai unaye Roho Mtakatifu yule anayeongozwa na Roho maisha yake huonyesha matunda haya. Upendo, Uaminifu, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, Upole, Kiasi (Gal 5:22-23). Mtu yeyote asijisifu bure kuwa anaye Roho Mtakatifu kama haongozwi naye Roho.

12 Ni ukweli dhahiri kuwa Ukristo siyo dini ya miujiza. Ni wale ambao hakuwa na imani ndiyo walimdai daima Kristo awaonyeshe ishara na miujiza (Yn 6:30) Yesu alisikitishwa sana na utovu huo wa imani kwani hata miujiza ilipotendeka na ishara bado baadhi hawakuamini NENO lake (Mt 11:20-24; Lk 10:13;Yn 12:37). Hivyo alama mojawapo ya kuonyesha upungufu au ukosefu wa imani ni mtu kutangatanga toka kanisa moja kwenda jingine kufuata miujiza au ya uponyaji au mingineyo. Kristo ametupa kipimo cha imani 'yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka una uzima wa milele' (Yn 5:24). Na mtu akiyasikia maneno ya Kristo na asiyashike, neno Kristo ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho (Yn 12:48). Mtakatifu Yohana anatufundisha kuwa "Yeye asemaye " nimemjua wala hazishiki amri zake ni mwongo wala haimo ndani yake .

Lakini yeye alishikaye neno lake katika huyo upendo wa Mungu amekamilika kweli kweli" (1Yoh2:4-5).

13. Hakuna chembe hata ndogo ya ukweli kuhusu kumwabudu Baba Mtakatifu. Hakuna tendo hata moja alifanyalo mtu yeyote la kumwabudu. hivyo ni dhihaka ya chuki kwa Wakatoliki kusema Papa anaabudiwa. Ni pia kumkosea haki na kumdhihaki Baba Mtakatifu kumwita mnyama kwa kisingizio cha tafsiri ya ufunuo wa Yohana sura ya 13. Tafsiri hiyo potofu inalenga kumkashifu yeye binafsi na pia kuikashifu nafai ya halifa wa Mtume Petro. Inalenga pia kuwafanya wakristo wanaomtii na kumheshimu Baba Mtakatifu kwa kufuata miongozo ya imani na maadili anayowapa wamdharau na wamchukuie na kuacha kufuata miongozo hiyo. Kanisa huwaagiza waamini wakristo kuwatii na kuwaheshimu Papa na maaskofu (Kan . 212 na 273 - sheria ya Kanisa) kwa sababu ya nafasi yao katika kanisa. Wakatoliki wanaokuwa waaminifu kwa kuwatii mahalifa wa wale "Thenashara" (mitume) wanachukiwa na kutukanwa. Lakini kumbukeni alivyowaambia hao mitume "Iwapo ulimwengu ukiwachukia mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu" (Yn 15:18-20).

  1. Katekisimu ya Kanisa inaeleza kuwa Simoni peke yake ambaye Bwana amempa jina la Petro amefanywa mwamba wa kanisa lake. Alimkabidhi yeye funguo (Lk 6:13; Yn 21:15-17), akamfanya mchungaji wa kundi lake. Lakini uwezo wa kufunga na kufungua uliotolewa kwa Petro umetolewa pia kwa URIKA (kikundi cha kudumu) wa mitume (maaskofu walio mahalifa wao) wakiungana na kichwa chao (LG22). Petro ndiye kiini cha kudumu cha chenye kuonekana na msingi wa umoja unaounganisha kati ayo maaskofu na umati wa waamini. Uwezo

Yasiyo ya Kawaida

Ndege anayejenga kwa wenzake huku kwake kwaporomoka

lJamii inamuhusisha na uchawi

lWatafiti wameshindwa kugundua kwa nini anawajengea wengine

Na Masha Otieno Nguru JR

"FUNDI CHUMA" ni mmoja kati ya ndege waliojizolea sifa kubwa sana katika mapori ya Afrika kutokana na na makuu anayofanya.

Pamoja na kuwa ni ndege mdogo tu ametokea kujenga viota ambavyo mpaka sasa binadamu wameshindwa kuamini ikiwa ni kweli vimejengwa naye.

Cha ajabu ni kuwa viota hivi vikubwa anavyojenga ndege huyu wa ajabu baada ya kuvikamilisha huishia kuvihama na kuachia ndege na wanyama wengine wavivu wa kujenga ndio wakae ndani yake na yeye kuhama kwenda kujenga kiota kingine tena.

Tabia hii ya Fundi chuma kujenga kiota na kukitelekeza kabla ya kuishi ndani yake mpaka sasa imebakia kuwa fumbo kwa watafiti wanasayansi wanaoshindwa kugundua ni kwa nini Fundi Chuma afanye hivyo.

Kiota cha Fundi chuma huwa ni kikubwa sana kiasi cha kwamba hata wanyama kama nyoka, Panya, Sungura, Pimbi na Ndezi wanaweza kuishi humo bila taabu.

"Mimi siku zote za utoto wangu nikitembelea mapori ya kwetu 'Ujaluoni' tulizoea kuona Bundi wakiishi kwenye viota vikubwa vya Fundi Chuma juu ya mti, hali hii ilitupelekea wajaluo kuamini kuwa kwa vile Bundi ni mkubwa ndiye amejenga kile kiota.

Nilikuja kugundua baadaye kupitia utafiti uliofanywa na Mtaalam wa picha za wanyama Mwingereza anayeishi Kenya. Bw. Allan Root kuwa kile kiota kikubwa Bundi alichokuwa akijivunia hakikujengwa naye bali na Fundi Chuma ndege ambaye Bundi anamzidi kwa ukubwa."

Kwa ujumla vifaa anavyotumia Fundi Chuma katika ujenzi wake pia huzidi kuchochea watu kumuogopa na kuamini kuwa ni kweli kwa kiasi fulani anahusiana na uchawi.

Zana anazotumia Fundi Chuma kwenye ujenzi wake zimekuwa ni pamoja na mifupa ya wanyama, vijiti, manyoya ya wanyama , Nywele za binadamu, nguo, nyasi, matope kidogo, kinyesi chake, na mikia ya wanyama.

Kuhusu nu wapi Fundi Chuma hutoa vitu vyote hivi bado watu wanashangazwa hali hiyo ndiyo huchangia kupelekea watu wanaopita karibu na kiota chake kumhisi kuwa ni mchawi. Pia hali hii imepelekea watu kam amimi ambao hatukujua siri hii tunapomkuta Bundi akiyatamia mayai yake kwenye kiota cha Fundi Chuma kuhisi kuwa Bundi ni Mchawi komesha.

Fundi Chuma wanapatikana katika mapori ya sehemu zilizo nyingi za Afrika. Lakini ndege hawa sana sana wanapendelea mapori ya Afrika Mashariki, Afrika ya Kati na hata Afrika ya Kusini. Hapa Afrika Mashariki Fundi Chuma wapo kwa wingi sana kwenye Mbuga za wanyama za Serengeti, Ziwa Manyara nan Kamageta.

Kiota kimoja kilichotelekezwa na Fundi Chuma chaweza kudumu kuwepo kikisaidia wanyama ndege wengine kama Maskani hata kwa miaka zaidi ya mitatu.

Kiota hiki hujengwa imara mithili ya nyumba ya binadamu kiasi kwamba mvua, jua kali na dhoruba haviwezi kuifanya lolote mahala ilikojengewa juu ya mti.

Fundi Chuma amefikia hatua ya kupewa na wataalamu jina la Mfalme wa Ndege hii inatokana na yeye kuwa shujaa kiasi cha kuwajengea ndege wengine wavivu viota vya kuishi. Undani na siri ya Fundi Chuma kufanya haya yote yaelekea anajua yeye mwenyewe na Mungu wake aliyemuumba.

Maisha na Mikasa

Mwanamke asema nilichoambulia kwenye ndoa ni kilema cha maisha na talaka nne

lPamoja na Talaka zote hizo ndoa ilidumu kwa miezi tisa tu, Mume adai mkewe hakufundwa

Na Dalphina Rubyema

Hidaya Saidi, mwanamke mwenye ujauzito amejikuta akiwa na ujauzito wa mumewa Bw. Saidi Abdallah, ambaye alishamwacha kwa talaka nne kwa mujibu wa imani ya dini ya Kiislamu. Wakati alipoachwa katika ndoa yao hiyo ambayo hata mwaka mmoja ilikuwa haijamaliza hakujua kama alikuwa mjamzito.

Akiwa ameshakaa kwa wazazi wake kwa miezi mitatu anaamua kuwasiliana na aliyekuwa mumewe ili waelewane wataifanyaje mimba "yao" hiyo.

Sambamba na hayo anaibuka na hoja ya kutaka mumewe amlipe madeni yake ya fedha alizowahi kumkopa. Si hivyo tu, mwanamke huyo anaibuka na hoja mpya kwamba wakati wa ndoa yao mumewe alikuwa akimwingilia kinyume cha maumbile na kwamba anahitaji matibabu.

Anadai alikuwa akiingiliwa hivyo na mumewe huyo ambaye ni Mfanyakazi wa NSSF, Temeke, jijini baada ya kuleweshwa pombe na alipogundua alibembelezwa kwa vijizawadi. Mumewe amejitetea kupitia gazeti hili kwamba mkewe amechanganyikiwa na ameshamchafulia jina vya kutosha, hivyo asingependa kuzungumza chochote. "Akitaka nitaongea mbele ya vyombo vya sheria," alisema mume huyo mwishoni mwa wiki.

Bi. Hidaya anaelezea mikasa mbalimbali aliyopata kutoka kwa mmewe ukiwemo ule wa kuchomwa kisu katika mkono wake wa kushoto.

"Mimi naitwa Hidaya Said, nilizaliwa mnamo mwaka 1974 mtaa wa Uhuru na Kongo hapa hapa Dar es Salaam. Lakini nimekulia Zanzibar ambapo nilikuwa nakaa na dada yangu katika sehemu ya Jang’ombe.

Nilikaa Zanzibar ambapo nilisoma shule hadi darasa la tano, darasa la sita na la saba nilikuja kumalizia huhu huku Dar es Salaam katika shule ya Msingi ya Hanannasif na hivyo darasa la saba nimemaleza 1997.

Kwa kweli nilichelewa kumaliza shule na hii ilitokana na kurudia rudia madarasa.

Baada ya kumaliza la saba sikupata bahati ya kuendelea na Sekondari , hivyo nilianza kazi ya kufuma mashuka ambayo ilinipatia pesa na kuweza kupanga chumba changu mwenyewe katika eneo la Moscow - Mzambarauni (Kinondoni).

Kwa kweli mashuka yangu yalinilipa na nilionekana msichana wa kuvutia na tarehe 10 Mwezi wa Pili mwaka 1999 kwa mara ya kwanza nilikutana na Bw. Saidi Abdalah Mambya ambaye alinieleza kuwa anataka kunioa.

Sikumkatisha tamaa, hivyo nilimshauri kuwa tuchunguzane kwanza na yeye akaniambia anataka kuoa haraka maana tayari alikuwa ameishaweka uamuzi juu la suala hilo.

Sikuona sababu ya kuendelea kumkatalia hivyo nilimpa ruhusa ya kuleta barua ya posa nyumbani kwa wazazi wangu.

Haikuchukua muda mshenga alitafutwa yaani mzee Shahibu Mzambe ambaye alileta barua nyumbani na kukubaliwa.

Sasa kabla ya kuanza kutoa mahari nilimuuliza mbona anataka kunioa haraka hivyo? alinijibu kuwa yeye anakaa bondeni kwa hiyo anataka kufanya harusi kabla ya mvua ambayo alihofia kuwa italeta tope.

Mahari ilitolewa tarehe 26 na mwezi wa 3 mwaka 1999 tukafunga ndoa ya Kiislamu. Harusi yetu ilifana sana.

Mwezi mmoja wa mwanzo wa ndoa yetu maisha yalikuwa mazuri sana lakini mwezi uliofuata, maisha yalianza kubadilika.

Bwana haachi hela ya chakula wala nini, kurudi ni taimu za usiku sana na nilipokuwa nikimuuliza ananiambia kuwa kazi ni nyingi sana.

Nilipoona hivyo nikaamua kuanza kazi yangu ya kufuma mashuka. Niliuza na kupata vijipesa kidogo lakini hapo hapo mume wangu naye akapata mkopo wa gari kazini hivyo ikabidi akope kwangu vihela hivyo vya mashuka ili aweze kumalizia mkopo wake.

Nikaendelea hivyo kumvumilia hapo tukawa tumefanikiwa kununua viwanja viwili, magari mawili na kuweka bomba la maji pamoja na kununua fenicha za ndani.

Bibi wewe! kuvuta bomba ndiyo ikaleta balaa maana hapo sasa hela ya chakula haikuachwa kabisa. Nikimuuliza mbona haachi pesa ananiambia niuze maji, mimi hili suala ikanibidi nilifikishe kwa wazazi wangu nao wakanishauri nivumilie kwani ndoa ni uvumilivu, nikakubali.

Tarehe 12 Novemba, mwaka jana tuliwaalika wageni nyumbani ambao ni marafiki zetu, tulishinda nao hadi jioni, baada ya hapo tuliwasindikiza.

Tukiwa njiani tunawasindikiza wageni hao siku hiyo ya Jumapili, mume wangu aliniambia nirudi nyumbani na nijiandae kusudi tukutane Maridadi Bar ambayo haiko mbali na nyumba yetu hapa Hanannasif.

Nilifanya hivyo na yeye akaendelea kuwasindikiza wageni nilipo fika nyumbani nilimwambia rafiki yangu Fatuma aliyekuwa ananisaidia kazi siku hiyo ya wageni ajiandae twende wote Maridad Bar kama alivyoniambia mme wangu ingawa niliambiwa niende peke yangu lakini sikuona sababu ya kumwacha rafiki yangu Fatuma ambaye kutwa nzima alishinda akinisadia kazi.

Tulipomaliza kujiandaa mimi na Fatuma tukaenda pale Bar; tulipofika hatukumkuta mume wangu lakini kwa vile nilikuwa na pesa kidogo tuliagiza kinywaji na baada ya muda mume wangu alifika.

Alipofika aliagiza soda na kunywa na sisi akaendelea kutununulia. Tulikuwa tunakunywa bia. Baada ya kukaa muda si mrefu sana mume wangu aliniaga kuwa anaenda nyumbani kupumzika na kuniruhusu mimi niendelee kupata kinywaji na aliniambia nisiondoke yeye mwenyewe atakuja kunichukua na gari. Aliniachia Sh.3,000 na kuondoka.

Kwa kuwa nilikuwa na rafiki yangu Fatuma, niliona uamuzi wa mume wangu siyo mbaya, hivyo tuliendelea kupata kinywaji huku nikimsubiri mume wangu aje kunichukua kama alivyoahidi.

Tulisubiri hadi saa sita usiku bila kumuona ilibidi tuondoke na nilipofika nyumbani niligonga mlango kwa muda mrefu bila kufunguliwa. Hatimaye alifungua mlango na mimi nikaingia ndani ambapo nilipokelewa na kipigo cha jiko la mkaa lililotengenezwa kwa udongo likanipasua mdomo wa chini.

Kwa vile nilishaweka pombe kichwani sikukubali siku hiyo kupigwa, hivyo tulianza kupigana na katika vurugu hizo tuliangusha taa ambayo ilikuwa inawaka na bahati mbaya kuanguka kwake kulisababisha kuungua baadhi ya vitu humo ndani.

Kuona hivyo mume wangu aliondoka na kwenda kutoa taarifa kwa mjomba wangu ambaye anaishi karibu na nyumba yetu na mjomba alikuja mbio na aliponiona hali yangu jinsi nilivyokuwa natokwa na damu alinishauri nitoe taarifa katika kituo cha polisi Mzambarauni ambao nao walinielekeza niende kituo cha polisi Oysterbay ambao walinipatia PF3.

Kwa vile siku hiyo ilishakuwa usiku sana na sikuwa na hela niliona bora niende kwa wazazi wangu nikalale na mambo ya matibabu niyashughulikie kesho yake.

Hiyo kesho yake najiandaa kutoka nyumbani kwenda hospitali, mume wangu alifika na ndugu zake na kuniomba tuyamalize na muafaka ulifikiwa. Tukawa tumeyasawazisha lakini yeye mwenyewe alinipeleka katika zahanati ya Mkwajuni na kupatiwa matibabu ya mdomo wangu, kisha akanipeleka kwa wazazi wangu nikapumzike.

Baada ya kukaa nyumbani kwa wazazi wangu nikiuguza mdomo wangu muda wa wiki nilirudi tena kwa mume wangu ambapo sasa wimbo wa kuninyanyasa ulibadilika kwani nilipomwambia anipe pesa ama kitu kingine alinijibu kuwa hana hela, hela yote anaitumia kununua vifaa vilivyoungua.

Nilivumilia, tarehe 31Desemba 1999 nakumbuka siku hiyo mume wangu aliniambia nimuandalie chai na mihogo ya kuchemsha. Alipomaliza kunywa hiyo chai na mihogo yake aliaga kuwa anaondoka, nami nikamuuliza ataondoka vipi bila kuniachia hela ya kula? Alinijibu kuwa hana pesa. Hali hii ya kila siku ya kilio cha kutokuwa na pesa niliona imezidi.

Nikatoka nikaingia chumbani nikachukua shati lake alilokuwa amevaa jana yake kuangalia angalau kama kuna pesa iliyobaki. Mungu bariki kufungua na kuingiza tu mkono ndani ya mfuko wa shati hilo nikakuta barua iliyokuwa imeandikwa "Vipi Bosi! Ile nyumba uliyoniambia niitafute tayari nimeishaipata ila unasubiriwa wewe tu, kabla hujaondoka nisubiri saa 10 tuongozane ili uende ukaione- Wako Emma."

Niliingiwa na kiwewe baada ya kusoma barua hii nikajua kumbe ndio maana mume wangu ananinyanyasa kumbe ana mtu mwingine. Niliona sasa dawa yake ni moja tu, ni bora niombe talaka. Nilirudi tena sebuleni na kuanza kumwambia huyo Saidi anipe talaka yangu.

Tukajibizana kwa muda akitaka kuninyang’anya hiyo barua yake lakini hakufanikiwa, hatimaye alifanikiwa kukimbia na alipofika mbali kidogo nilimsikia akisema ‘fungasha uondoke na mimi naenda kukuchukulia gari!’

Niliona kukimbia kwake sio dawa kwani nilimfuata kazini kwake anipe talaka yangu na huko kazini mzozo ulianza upya hadi wafanyakazi wenzake wakaanza kunibembeleza niache tukayamalizie nyumbani. Lakini mimi nilikataa na kuwaambia hatua aliyofikia mume wangu ya kuniletea wanawake nyumbani nikimuuliza anadai ni wafanyakazi wenzake haivumiliki!.

Hatimaye niliona hakuna sababu ya kuendeleza mzozo pale ofisini, hivyo tuliondoka wote hadi nyumbani na huko aliniandikia talaka tatu kwani siku za nyuma alikuwa kisha nipa talaka moja, jumla zikawa nne.

Siku hiyo nilifungasha vitu vyangu hadi nyumbani nikiwa sina akili timamu kwa vituko alivyonifanyia mume wangu. Baada ya kutulia akili yangu niliona sina msingi wa kuanzia maisha kwani hela yangu yote ya mashuka nilikuwa nimeisha mpa yeye kukomboa gari lake la mkopo hivyo niliona bora nitafute wazee wanipe ushauri.

Wazee hao walinishauri niende BAKWATA na huko BAKWATA niliwasimulia mkasa mzima na wakamwandikia barua ambayo nilimpatia mshenga na nasikia baada ya Said kuisoma alisonya na kuichanachana.

Nilipopata taarifa hiyo niliona sasa huyu mtu anataka kunichezea, hivyo nilichukua hatua ya kwenda Polisi Oysterbay kufungua faili la mshitaka. Pale polisi nilieleza kuwa nahitaji mume wangu anipatie pesa yangu ya mashuka na kunipatia pesa ya matibabu kwani nilikuwa najisikia maumivu makali kufuatia vitendo vya kunilawiti alivyokuwa ananifanyia baada ya kunilewesha kwa pombe.

Niliongozana na polisi hadi nyumbani kwa mume wangu kwa nia ya kumkamata na tulipofika pale askari nilioongozana nao walifanya ustarabu kwani walimwambia ajipeleke mwenyewe kituoni nasi tukawa tumeondoka zetu. Nilirudi nyumbani kwa wazazi wangu.

Muda mfupi tu baada ya kufika nyumbani nikamwona huyo bwana ameongozana Sheikh aliyetuozesha eti wamekuja nyumbani tuyamalize; mimi nilikataa. Kaitka kikao hicho tulichokaa na wazazi wangu na huyo bwana na Sheikh niliona siyo vizuri kuwaelezea mambo ya kulawitiwa,lakini nilishikilia kuwa suala hilo ni bora libaki kwenye vyombo vya sheria.

Kumbe siku hiyo aliyochana barua ya BAKWATA alikariri tarehe aliyoandikiwa kuwa twende kutafuta suluhu. Huko BAKWATA Sheikh Gorogosi alimwambia mume wangu anipe pesa ya chumba na deni langu la pesa ya mashuka ambapo alinikabidhi sh,110,000/= na Sheikh alimwambia kuwa ni lazima huyo bwana anipe vitu vingine tulivyochuma wote.

Vile vile Sheikh sikumwambia suala la kulawitiwa, hivyo niliongozana na mume wangu hadi polisi Osterbay ambapo alinikabidhi sh.45,000 kwa ajili ya matibabu nikafuta kesi.

Niliendelea kukaa nyumbani lakini niliona imepita miezi mitatu tangu nipewe talaka na mume wangu bila kupata siku zangu za hedhi hivyo nilijua sasa kuna uwezekano kuwa nina mimba.

Kwa vile tangu niachane na huyo mme wangu nilikuwa bado sijakutana na mwanaume mwingine kimwili niliona bora nimtaarifu juu ya hali hii ili akatae ama akubali nijue moja.

Hivyo tarehe 19 Desemba mwaka jana nilikutana naye barabarani na kumwambia afike nyumbani wazazi wangu na ndugu zake kwani kuna maongezi muhimu nataka yafanyike; na kweli siku hiyo jioni alifika nyumbani pasipokuwa na ndugu zake. Mimi baada ya kumuona niliwaita mama na dada yangu pamoja na yeye mume wangu na kuwajulisha juu ya hali niliyokuwa nayo, kwa kweli mume wangu hakubisha; alikubali kuwa kweli kama mimba ipo ni yake. Alichosema ni kuwa kesho yake asubuhi nifike kwake jioni kwa ajili ya kupata pesa ili niende hospitali kupima kama kweli nina mimba.

Nami sikufanya hiyana kesho yake saa mbili usiku nikaenda kwake. Kufika nikagonga mlango, akanifunulia na nikaingia ndani. Hapo alifunga mlango kwa ndani na kuanza kunitupia maneno. ‘"Wewe mwanamke usiyekuwa na haya... unasema una mimba yangu! mimi nitakupaje mimba na wakati uliniaibisha polisi kuwa nilikuwa nakulawiti?’.

Hapo hapo alinyanyuka na kuanza kunipiga na kwendea kisu alichokuwa tayari kaishatayarisha na kunichoma nacho mkono wangu huu wa kushoto (anaonyesha mkono huo na kuanza kulia) hapo hapo alinikamata hadi nikazimia.Alitoka mbio na kwenda kwa mjomba wangu na kumwambia kuwa nimemfuata kwake kumfanyia fujo.

Mjomba alifika nyumbani hapo na kunikuta nimezirai hivyo aliwataarifu ndugu zangu wengine na kunikimbiza hospitali. Huko Muhimbili nilikaa zaidi ya mwezi mmoja nikipatiwa matibabu.

Walinishona nyuzi mkononi na kunitibu koo ingawa hadi naruhusiwa kuondoka hospitalini hapo koo langu lilikuwa bado halijaanza kuongea vuzuri.

Nilienda kuomba msaada kwa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) ambapo walipoona siwezi kuongea vizuri kufuatia maumivu ya koo waliona bora kwanza kabla ya kushughulikia suala langu ni bora nipate msaada wa matibabu zaidi, wakanisaidia na bado wameahidi kunisaidia kisheria.

Mwandishi alitaka kupata ufafanuzi wa tuhuma nzito ya ulawiti.

Mwandishi: Unasema mumeo anakuingilia kinyume na maumbile bila ridhaa yako je kuna mahali popote ulikuwa umekwisha mfungulia mashtaka kabla ya kupewa talaka?

Hidaya: Hapana nilikuwa sijamfungulia mashtaka kwani alikuwa kesho yake ananiomba msamaha na kunipa vijizawadi vya kuniliwaza alidai alikuwa anapitiwa.

Mwandishi: Je kakufanyia hivyo mara ngapi?

Hidaya: Ni mara nyingi, siwezi kukumbuka ni mara ngapi maana huyu Bwana siku akisikia kufanya unyama wake huo, uwa ananinywesha pombe na kunionyesha upendo wa hali ya juu na nikisha lewa ndipo unapata nafasi ya kufanya atakavyo.

Mwandishi: Je hapa unapoishi ni kwa wazazi wako ama ni chumba chako mwenyewe?

Hidaya:Hapa nimepanga chumba changu

Mwandishi: Si unasema hauna pesa sasa hela ya kulipia kodi unatoa wapi? au umepata bwana mwingine wa kukusaidia?

Hidaya:Mmm! Nimpate wapi bwana mwingine! Hiyo hela sh. 110,000 aliyonipa Saidi huko BAKWATA ndiyo hiyo hiyo nalipa kodi.

Mwandishi: Iwapo suluhu itapatikana utakuwa tayari kurudi kwa mume wako ama hapana?

Hidaya: Sitakubali kurudiana naye ingawa yeye anasema talaka alizonipa si halali. Eti mtu hawezi kupewa talaka na mimba mimi siko tayari sitaki kabisa kurudi kwake maana akumlikaye mchana, usiku ukuchoma.

Gazeti hili lilipoongea na Bw. Said Abdalah Mambya, Ijumaa iliyopita kwenye ofisi za Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) zilizopo Temeke jijini Dar-Es-Salaam ambako yeye anafanyia kazi, alikuwa na haya ya kusema:

"Ni kweli huyu mwanamke alikuwa mke wangu lakini kuhusu yaliyotokea mimi bwana nimefundwa maneno ya kuongea hadharani tofauti na huyo mwenzangu anayeropoka hovyo. Hivyo siwezi kusema lolote kuhusiana na tuhuma hizo na nitafanya hivyo mbele ya chombo ambacho kitaweza kutoa uamuzi.

Nikiitwa kwenye vyombo vya Sheria nitoe maelezo yangu juu ya huyu mwanamke niko tayari kufanya hivyo na maelezo yake nitayagawa kwenye sura tatu ambazo siwezi kufafanua kwa hivi sasa.

"Kama ni kunidhalilisha huyu mwanamke kanidhalilisha sana, sasa kama anaona kuna haki nimemnyima ninamruhusu aende kwenye vyombo vya sheria kudai hizo haki siyo kukaa kuninyanyasa katika vyombo vya habari."

Kuhusu TAMWA mimi ni kwamba bado sijapokea barua yao ya kunitaka niende huko isitoshe naona hao TAMWA hawamjui huyo Hidaya na ndio maana wakajikuta wanatoa machozi siku alipodai mbele ya Makamba eti nimemfanyia mambo ya ajabu!

Mimi hapa ni bosi mkubwa tu, hapa NSSF Temeke kuna wasichana wengi sana kwanini nisiwatendee hao unyama na badala yake nimfanyie yeye?