Yajue madhara ya vidonge vya majira

Watu wengi katika jamii,wamejenga dhana potofu kuwa njia bora na ya pekee ya kudhibiti ongezeko la idadi ya watu na mimba zisizotarajiwa kwa wakati, ni kutoa mimba na kutumia dawa za kisasa kuzizuia badala ya kutumia njia za asili zinazotegemea maumbile.

Katika makala haya, Mwenyekiti wa Shirika la Kutetea Uhai la Pro-Life Tanzania, Bw. Emil Hagam, anajaribu kuelezea madhara ya vitu hivyo ambayo jamii haijui kuwa yapo ingawa inahimizwa kutumia.

KIMSINGI vidonge vya majira hufanya kazi kwa kuzuia kupevuka yai. Lakini sio mara zote utendaji huu hufanikiwa. Ikitokea kuwa yai limepevuka, basi kazi ya pili huwa ni ile ya kuzuia mimba kujipandikiza. Kazi hii ya pili yaweza kutokea ama kabla, au baada ya kujipandikiza kwa mtoto.

Athari za baada ya kujipandikiza zinaweza kuleta matatizo makubwa kwa baadhi ya watu ambao wangetaka kujua uwezekano huu. Katika makala haya nitajaribu kutathimini ushahidi uliopo juu ya athari za vidonge baada ya kujipandikiza na kuunga mkono hoja kuwa uwezo wa vidonge vya majira hutegemea kwa kiasi kikubwa athari hizo baada ya kujipandikiza.

Pamoja na kukosa takwimu hizo, kanuni za uelewa wa watumiaji ni muhimu ili iwasaidie kufanya uamuzi wa busara katika kutumia vidonge vya majira.

Vidonge vya majira ni kati ya dawa zilizofanyiwa utafiti wa kina na zimetumika utafiti sana hapa duniani ingawa katika baadhi ya nchi matumizi yake yako katika kiwango cha chini.

Nchini Marekani, matumizi ya vidonge vya majira yamechangia katika kukubalika kama njia ya kudhibiti kizazi ingawa kwa baadhi ya wateja, maamuzi juu ya matumizi yake, bado yamegubikwa na vikwazo vya kimaadili na kiimani kwa watu ambao huamini kuwa uhai wa binadamu huanza katika muunganiko wa yai la mama na mbegu ya baba.

Njia yoyote ya uzazi wa mpango inayoharibu ukuaji wa mtoto (mimba), haiwezi kukubalika kamwe kutumika kama njia ya kudhibiti mimba zisizokusudiwa na kasi ya ongezeko la watu.

Hii ni pamoja na vidonge vinavyotumika baada ya mimba kutungwa na vile vya tahadhari (Emergence Contraceptives) ambavyo hutumika baada ya tendo la ndoa na kwa kuamini kuwa mimba imetungwa.

Vilevile, vidonge vya RU 486 na vitanzi, vinavyotumika kama viua mimba, zimekubaliwa kuwa na matokeo yasiyo ya msingi.

Ushahidi wa jambo hili haujathaminiwa vya kutosha. Lengo la makala haya, ni kuwawezesha watumiaji kujua athari hizo na hivyo kufanya uamuzi ufaao juu ya matumizi yake na maelezo yafuatayo yanatokana na taarifa zilizochapishwa tangu mwaka 1970.

UTENDAJI WA VIDONGE VYA MAJIRA.

Wakati kimsingi vidonge vinauzia yai kukomaa (kupevuka), kwa kukandamiza chembechembe katika tezi la "Pituitary gonadotropin", utendaji mwingine ni ule wa kubadilisha ute wa mwanamke na hivyo kuzuia kupita na pia kuleta mabadiliko katika ukuta wa mji wa mimba na mirija ya uzazi (fallopian tube) ambayo huzuia kupita kwa mbegu.

Kushindwa kufanya kazi kwa vidonge kunatofautiana kufuatana na aina na matumizi. Vidonge vya kiwango cha chini vinavyotumia "estrogen" na matumizi mabaya vinashindwa kuzuia yai kupevuka.

Matumizi mazuri ya vidonge (oral contraceptives), yana maana ya kumeza kila siku na kwa namna iliyo sahihi ( maana yake kwa mpangilio, kwa wakati wake kila siku bila kutumia madawa mengine ambayo yanaweza kupunguza nguvu zake).

Matumizi halisi humaanisha kiwango cha kawaida cha matumizi. Utafiti uliotathimini matumizi yake kwa wanawake umeonesha kiwango cha kushindwa kiasi cha asilimia 1.7 na 28.6 kwa kila mwandamo.

Kushindwa kwa vidonge vinavyotumia kemikali ya "progestin" (Progestin only Pills) ni kiwango cha asilimia 33 hadi 65.

Ni wazi kuwa kushindwa kwa vidonge kunasababisha kutungwa mimba isiyotarajiwa na kiwango chake hutofautiana na kiasi chake hudharauliwa.

Upembuzi wa kina unaonesha kuwa utungaji wa mimba zisizotarajiwa ni kwa kiwango cha asilimia 0.1 na 1.0 kwa kila wanawake 100 wanaoutumia vizuri na asilimia 3 kwa kila wanawake 100 wasiotumia vizuri katika mwaka wa kwanza wa matumizi. Takwimu fulani za kitaifa zilionesha kuwa kiwango cha kushindwa ukijumlisha na mimba zilizoharibiwa ni asilimia 4 kwa watumiaji wazuri na asilimia 8 hadi 29 kwa wale wasiotumia vizuri.

Viwango vya upatikanaji wa mimba ni vikubwa kwa watumiaji wa POP kuliko watumiaji wa OC’s. Viwango hivyo ni kati ya asilimia 3 hadi 7 kwa kila wanawake 100 wenye matumizi halisi (pamoja na wale wasiotumia vizuri).

Vidonge vya progestin vinaaminika kuharibu ute na ukuta laini ndani ya mji wa mimba. Hali hii imeleta hoja kuwa kazi ya vidonge hivi ni kuharibu mimba na kuharibu mazingira ya kusafirisha mbegu.

Kinadharia, athari ya vidonge vya majira zinaweza kuangukia katika makundi mawili:

1) Kabla ya kujipandikiza, itakuwa na athari za kupunguza uwezo wa kusafirisha mimba katika mirija ya uzazi (fallopian tube) na hivyo huzuia mimba kujipandikiza katika mji wa mimba na hali hii inaweza kusababisha kutotambulika kwa mimba hiyo ikiharibika au mimba hiyo kujipandikiza nje ya mirija hiyo.

2) Kuharibika kwa ngozi nyororo ya tumbo la uzazi kwa namna kwamba mimba hiyo baada ya kufikia mji wa mimba, inashindwa kujipandikiza katika ngozi nyororo.

3) Kutoa mimba kunakosababishwa na mimba hiyo kushindwa kukaa katika mji wa mimba; mimba inajipandikiza lakini baadaye ina kufa kutokana na mji huo kushindwa kuhifadhi mimba hiyo.

ATHARI ZA VIDONGE VYA MAJIRA ZITOKEAZO BAADA YA KUTUNGWA KWA MIMBA

1. Mabadiliko ya ngozi nyororo

Vidonge (Oral Contraceptives), huathiri moja kwa moja ngozi nyororo kwa kuifanya ngozi hiyo isiweze kupokea na kutunza mimba iliyotungwa. Hali hiyo hutokea kwa sababu vidonge hivyo huharibu ngozi nyororo ambayo hufanya kazi kama kitanda cha mtoto.

Ngozi hiyo inakuwa nyembamba iliyotanuliwa, iliyochoshwa na nyamanyama zake kubaduliwa kwa kuharibu chembechembe za ngozi nyororo na kwa kuharibu chakula cha mtoto kitengenezwacho katika ngozi hiyo.

2. Mabadiliko ya Chachu ziitwazo ‘Integrin’

Chachu za ‘intergrin’ ni muunganiko wa molekule ambazo hutengeneza mazingira ya upokeaji wa mimba katika ngozi nyororo ya tumbo la uzazi. Chachu hizi zikiharibiwa, mazingira ya upokeaji wa mimba huharibiwa pia yaani, kuifanya mimba isiweze kusafiri kutoka kwenye mirija ya uzazi kwenda kwenye mji wa mimba.

3 Kuongezeka kwa mimba nje ya mji wa mimba

Utafiti umeonesha kuwa wanawake wanaotumia vidonge (OC’s) wamo katika hatari kubwa ya kupata mimba nje ya tumbo la uzazi ukilinganisha na wanawake wasiotumia.

Utafiti uliofanywa katika nchi 17 zenye jumla ya vituo 33 na uliowahusu watu 2800 umethibitisha kuwa matumizi ya vidonge, yanaongeza uwezekano wa kupata mimba nje ya tumbo la uzazi.

Mimba hizi za nje ya tumbo la uzazi (ectopic pregnancy) huhatarisha sana uhai wa mama. Watumiao vidonge vya progestin (POP’s) Vilevile wamo katika hatari kubwa ya kupata mimba nje ya tumbo la uzazi.

KUTOA TAARIFA ZA KWELI

Wataalamu wengi wa afya ya kizazi wanatafsiri mimba kama vile ni ile itokeayo baada ya kujipandikiza. Hata hivyo tafsiri hii haiondoi ukweli kuwa wataalamu wengine na baadhi ya watu wanaamini kuwa mimba hutungwa wakati mbegu ya baba na yai la mama vinapoungana.

Kwa watu hawa, aina yoyote ya kuzuia uhai kunakosababisha uhai huo kuuawa haiubaliki. Bila kujali itikadi, imani, msimamo au mtazamo.

taarifa za kweli juu ya kazi, mwenendo na athari zitokanazo na matumizi ya vidonge lazima yawekwe wazi kwa watu ili kama wanaamua kutumia watumie wakiwa wanafahamu watu wapatiwe taarifa za kweli za uhakika na bila propaganda.

Imefupishwa toka makala ya "Post fertilization Effects of Oral Contraceptives and their Relationship to Informed Consent" katika jarida la ARCHIEVES OF FAMILY MEDICINE, Vol.9, No.2, February 2000

Ijue imani yetu

Imani yetu juu ya Msalaba

MARA kadhaa kumekuwapo maswali na mashaka mengi kuhusu suala la kuabudu msalaba, hasa siku ya Ijumaa Takatifu. Mashambulizi ya Wakristo wa madhehebu yasiyo ya kikatoliki na dini nyingine yamewafanya baadhi ya Wakatoliki kuingia mashaka kuhusu neno hilo. Katika makala haya, Katibu wa Idara ya Liturgia ya Baraza la Maaskofu, Padre Julian Kangarawe anajadili suala hili ili kuondoa uvumi na uzushi wa wasiojua maana na matumizi ya msalaba katika Kanisa Katoliki.

"Hata wengine wamefika kuomba tubadili neno hilo tuseme ‘kuheshimu msalaba’ badala ya kuabudu msalaba. Hata kitabu cha madhehebu ya Maaskofu, kwa kiingereza, kiitwacho ‘Veneration of Bishops’ kimepiga chenga kidogo na kusema ‘Ceremonies of the Cross’ badala ya ‘Adoration of the Cross’. Kama ilivyo katika kitabu hicho hicho kwa lugha ya kilatini (Adoratio Crucis).

Kuna umuhimu wa kutuoa mafundisho sahihi kuhusu suala hilo kwa yamkini hatuabudu ubao fulani udongo fulani au chuma kinachoitwa msalaba. Andiko lasema: ‘Watamtazama yule waliyemtoboa’ (Yn.19:37), yaani Yesu aliyetundikwa msalabani; au ‘kama vile Musa alivyomwinua juu nyoka wa shaba kule jangwani, naye mwana wa mtu atainuliwa juu vilivyo hivyo ili kila anayemwamini awe na uzima wa milele’ (Yn 3:14-15).

Atainuliwa juu ya msalaba. Msalaba hapa ni ishara hai ya Yesu anayetundikwa msalabani, anayekufa msalabani kwa ajili ya ukombozi wetu wanadamu. Msalaba ni Yesu mteswa. Ndiyo maana tunasema kwa makini kabisa: "Ee Bwana tunakuabudu na tunakuheshimu, kwa sababu umeikomboa dunia kwa msalaba wako mtakatifu". Msalaba unakuwa mtakatifu kwa sababu unatumika na Kristo, Mungu- Mtu kwa ajili ya kazi ya ukombozi. Na Ijumaa Takatifu tunaimba "Huu ndiyo mti wa msalaba ambamo wokovu wa dunia umetundikwa juu yake, njooni njooni tuabudu". Tunachoabudu wokovu wa dunia ni Yesu mwenyewe aliyetundikwa msalabani. Msalaba ni ishara yake mwenyewe ni yeye mwenyewe. Tunapotaja msalaba tunamtaja yeye Yesu anayewambwa katika mti huo, mti unapata hadhi hiyo ya nafasi ya Yesu mwenyewe mteswa. Tunapiga magoti mbele ya Yesu anayeteswa na kufa msalabani. Tunamwabudu Yesu mwenyewe siyo mti, au chuma au udongo wenye sura ya msalaba, bali nafasi ya Yesu mwenyewe.

Ni lazima tujilee na tufundishike kuvuka toka ishara ya msalaba tunayoiona hadi kumwona Yesu mwenyewe.

Tusipovuka hivyo tunafanya makosa, kama wanavyotulaumu wengine wa ishara, hilo lisingekuwa tatizo kwake kufahamu na kuona zaidi ya kile kinachoonekana kwa macho.

Ni kwa sababu hiyo ya ufahamu sahihi kanisa kwa makini linasema kwamba, hasa Ijumaa Takatifu, wakati wa ibada ya kuabudu msalaba, haifai kuitoa misalaba mingi kwa ajili ya kuabudu. Kufanya hviyo kunapoteza maana ya ishara, kunavuruga moja kwa moja maana ya ibada yote iliyofanyika ya kuuleta ule msalaba mmoja kuufunua kuuimbia na kuabudu.

"Huu ndio mti wa msalaba...." Na pengine ikaletwa hata misalaba ya chuma!!! Maana ya ishara inapotea na kupotoshwa.

Ingefaa tukafahamu vema nia ya mama Kanisa kuweka misalaba mingi siku ya Ijumaa Takatifu. Hapa si shauri la kutaka kumaliza kundi la watu mradi tu wanamalizika upesi kufanya tendo hilo la kuabudu msalaba. Hiyo si hoja ya kikatekesi wala ya kiteolojia wala Kiliturujia wala kichungaji wala mwongozo wa Mama Kanisa.

Kanisa limeelekeza kwamba kama watu ni wengi sana, basi mchungaji aeleze vizuri maana ya kuabudu msalaba na awaelekeze waabudu toka mahali walipo wakimwona Yesu mwenyewe akifa msalabani. Hisia za kudai Waafrika wanapenda kubusu msalaba kunapelekea kwenye hatari ya kosa la kuabudu sanamu, na ndiyo maana wengi kweli hupenda kubusu msalaba angalau Ijumaa Takatifu, lakini kwa bahati mbaya maadili yao hawako tayari kubadili na kumwongokea na kumgeukia Yesu wanayembusu akiteswa na kufa kwa ajili yao.

Ibada ambayo si sahihi inamwelekeo wa kuwaingiza watu katika ibada potofu kabisa. Kama hisia hizo ni za kweli, basi wakeshe kama tufanyavyo Alhamisi Takatifu! Kuabudu kwa namna hiyo mradi kubusu msalaba bila kuongoka hakufanani na ushirikina? Ni busara na salama kufuata mafundisho na maelekezo ya mama Kanisa, mwalimu pekee na mratibu wa imani Katoliki pamoja na utekelezaji wa imani hiyo katika ibada za liturujia.

Kwa namna hiyo hatuna haja ya kuhangaika kutaka kubadili maneno. Ni sahihi KUABUDU MSALABA kwa namna ya kumwabudu Yesu aliyewambwa mtini, anayeteswa mtini,anayekufa msalabani. Wala tusibabaishwe na wapinzani ambao wanaamini kujua zaidi maandiko ya Mungu.

  

Uchaguzi wa Kisiasa kwa nini tujali?

Y Mpenda amani

Y Mwaminifu

Inaeleweka kiongozi yeyote anaweza kukumbana na vishawishi.

Y Kutokana na silika, kiongozi ni mtu anayeshawishika kuongozwa na kutokana na tabia na silika za ubinadamu hujikuta amewaambia watu nini cha kufanya badala ya kuwapa fursa kutoa mawazo yao na kuyazingatia katika kufikia uamuzi wa utekelezaji.

Y Baadhi ya viongozi wanashawishika kuwa na kiburi au majivuno fulani na kufikia hali ya kujiamini kupita kiasi.. Wanafikiri wao wanajua kila kitu hawakubali kukosolewa na wala kupokea mawazo ya wengine wanashawishia kulazimsha maoni yao hata kama yanathibitika kuwa si sahihi.

Y Mara nyingi viongozi wanavutwa na tamaa ya madaraka. Baadhi yao wanafurahia kutawala wengine na wanapenda kuwa katika aina nyingi za vyombo vya kutolea maamuzi. wanapenda pia kuheshimiwa na kupewa nafasi nzuri na za kwanza kupewa usafiri bora kukiromiwa marupurupu mengi tu.

YViongozi hushawishika kutumia madaraka yao vibaya au kuwapa wengine rushwa ili wawafanikishe mambo yao na kutekeleza matakwa ya wale wanaowasaidia.

Vishawishi hivi kuwapata wanasiasa mmoja mmoja na hata katika makundi kama Chama cha siasa na hii ndiyo sababu uongozi wa kisiasa unahitaji udhibiti ili kufisha nguvu ya vishawishi hivyo na kuhakikisha kuwepo kwa uongozi bora na uadilifu hasa katika ngazi ya vyama vya siasa.

Kwa hiyo;

- Kama Chama cha Siasa siyo cha Kidemokrasia, ni wazi hakiwezi kuongoza kidemokrasia endapo kitapewa dhamana ya kuiongoza Serikali.

- Kama vyama vya Kisiasa haviamini wengine au haviko tayari kushirikiana na vyama huru vya wananchi au vikundi vya dini havitaweza kamwe kusikiliza na kutimiza matakwa ya watu.

- Kama wanasiasa na vyama vyao hawaheshimu maoni ya wengine na ya vyama vya upinzani ni wazi vitakuwa na asili fulani ya udikteta.

Ukweli unabaki pale pale kuwa watu hujipatia uongozi ambao ni stahili yao. viongozi wanaweza kutumia vibaya madaraka kwa sababu tu watu wanaowaongoza wanawaruhusu kuchezea madaraka. Viongozi wanaweza kushinikiza mambo yao kwa sababu watu hawawaulizi chochote na wala hawajajifunza namna ya kutoa changamoto dhidi ya maoni na utendaji wa viongozi wao. Mara nyingi watu huwa tayari kukubali na kupokea ahadi hizo mara nyingi pia watu hujisikia udhaifu fulani au wanapata woga kuuliza chochote wakati mtu mwenye madaraka anapowaeleza kitu hata kama wanajua sio sahihi.

Tunahitaji kujifunza kuwauliza wawakilishi wetu nini wametufanyia.

Lazima watoe taarifa kamili ya uwajibikaji. Hii ni katika ngazi zote kuanzia chini tunamoishi. Wanaotuwakilisha katika mikutano mbalimbali wanawajibika kutupatia taarifa.

Uongozi wa Chama cha Kidemokrasia unapaswa kuwa na;

- Taratibu zilizo wazi za uteuzi wa wagombea wake katika ngazi zote.

- Uteuzi wa wazi na halali wa wagombea wake na katika uongozi wa Chama.

- Mijadala na makubaliano ya wazi ya Sera za Chama

- Uwazi na Ukweli katika upatikanaji wa fedha na matumizi yake.

- Taarifa za fedha zilizo wazi kwa ukaguzi wa Wanachama.

Uongozi mzuri unaruhusu mawazo mapya na damu mpya ndani ya chama ili kuondoa kundi fulani linalotaka kujidumisha katika madaraka.

Hii si kwa nchi inayokabiliana na mabadiliko ama changamoto mbalimbali tu bali ni kwa nchi zote.

MASWALI:

i) Je, tunawezaje kupata viongozi wanaojitoa kupigania Haki na kulinda amani pamoja na kutekeleza wajibu wao kwa watu waliowapa kura zao.

ii) Unawezaje kumtambua kiongozi mwenye:

- Kiburi na majivuno

- Uchu wa mali na madaraka

- Moyo wa Kidemokrasia.

iii) Ni kwa nini vyama vinashindwa kuchagua wagombea wao kihali na kwa uwazi?

iv) Ni mambo gani yanawafanya wagombea kutokuwa tayari kupokea matokeo ya kushindwa katika uchaguzi.

v) Je, una maoni gani kuhusu fedha nyingi zinazotumika kuendeshea kesi za uchaguzi

vi) Kwa nini si rahisi vijana kupata nafasi ya uongozi wa Chama?

3. MIPANGO YA UCHUMI

Josephs na Cyril wameishi katika mji mkubwa kwa muda wa miaka minne na waliotaka kuoa na kuishi kijijini mwao. Ijapokuwa hawakujipatia fedha nyingi lakini wameona na kujifunza mengi.

Uzoefu wao mwingi wa uwajibikaji waliojifunza katika Kikundi cha Vijana kilichopo Parokia ya Manzese kimewasaidia kuelewa kuwa ni uwajibikaji na kufanya kazi pamoja ndiyo njia pekee inayofikisha katika mafanikio fulani. Kupanga mipango mizuri hakusaidii lolote mpaka mpango hiyo itakapowekwa katika utekelezaji.

Walitaka kuwashirikisha wenzao huko Kijijini uzoefu wao katika hitaji la kufanyia ukarabati shula fulani. Walijiuliza 'tutaweze na tutaanzia wapi?" Wanayo mikono miwili afya nzuri na msukumo mkubwa na nia nzuri ya kusadia wenzao hapo kijijini.

Joseph na Cyril wakaanza mipango mingi Ijapokuwa ilichukua muda wa mwaka mzima kukarabati darasa moja tu, mbali na muda mwingi na nguvu kutumika licha ya mikutano ya kukatisha tamaa kwingi hatimaye walifanikiwa.

Kupanga uchumi kunaanzia na kutambua mahitaji kupima uwezo wa watu na Rasilimali zilizopo kisha kutekeleza kwa msukumo wa pekee kwa kuweka mikakati ya utekelezaji.

Tukiangalia Historia yetu baada ya Uhuru Ukuaji wa uchumi ulitilwa maanani katika sera za maendeleo. Kuondoa umaskini maradhi na Ujinga vilizingatiwa katika kila Sera ya msingi ili kulifanya Taifa lianze maendeleo kiuchumi.

Sasa umepita muda takribani miaka 40 ya uhuruu ambapo tunaweza kusema tumepiga hatua kiasi fulani. tumejionea mambo mengi mazuri lakini bado pia tunaona

Maisha na Mikasa

ALIYETELEKEZWA JIJINI DAR ASIMULIA NA KUSEMA

Daktari aliyenileta Dar alinifukuza bila hata ya senti

lNiliokotwa na mchungaji

"BIASHARA ya kuwarubuni watoto wa maeneo ya vijijini eti wanakuja mijini kutafutiwa kazi, ama kujiriwa majumbani, imeshamiri mno siku hizi kwa watu wasio na utu wala huruma.

Wengi wao wanapofika mijini, huwageuza zana na vitega uchumi vya kuongeza kipato cha familia,aidha kwa kuwauza moja kwa moja kama bidhaa za sokoni ili wakawe wafanyakazi wa majumbani mwa watu wengine, au kuwafundisha na kuwasajili katika biashara haramu ya ukahaba na kucheza muziki kwenye kumbi za starehe.

Ingawa ni watoto wa kike wanaoathirika zaidi na tabia hii inayokwenda kinyume na maadili ya jamii na mapenzi ya Mungu, wapo pia watoto wa kiume wanaoangukia katika mitego hiyo. Hao ndio huishia kupiga debe wasijue kuandika hata "A", kuvuta bangi na kujihusisha na vitendo vya ujambazi, wizi na matumizi ya madawa ya kulevya.

Abass Kihanza, ni mvulana aliyejikuta akiangukia ndani ya shimo lenye adha na mateso ya namna hiyo. Yeye mwenyewe katika makala haya, anaelezea yaliyomkumba kama alivyozungumza na Mwandishi wetu NEEMA DAWSON.

"Nimeamini kuwa maisha ni kitendawili na ni mlima,kwani kuna kupanda na kushuka.

Hakuna ambaye anaweza kukitegua zaidi ya Mungu. Maishani mwangu sikuota wala kutegemea kuwa siku moja na mimi ningejua walau kusoma au kuandika angalau jina langu.

Hivi hapa nilipo, nani angenigharamia masomo ya hapa sekondari? Nakuapia asingekuwa huyu mchungaji; Mchungaji Michael Mugarura, kunichukua na kuniongoza sijui ningekuwa napita katika mapito ya dunia ya nani huku sijui hata kusoma!

Sijui sasa hivi ningekuwa nazungumzia wapi na ningekuwa katika hali gani ya kiafya na hata ya kiroho pia"

"Mimi nilikuwa nimejizoelea kuishi kwetu Iringa kwa wazazi wangu ingawa hali yetu ya kimaisha ilikuwa ngumu sana kutokana na wazazi wangu kuwa na uwezo duni na tulikuwa tunategemea kuishi kwa ajili ya kilimo peke yake na kutokana na wazazi wangu kuwa na afya zisizoridhisha kuna kipindi kushika jembe kulikuwa kunawashinda na msimu unapofika wa mavumo hapo ndipo tulipokuwa tunatoka kapa kwani kipindi cha kilimo hatukuweza kulima mazao mengi na pesa ya kuweka vibarua tulikuwa hatuna; kama unavyojua kijijini"

Ilipotokea bahati ya mimi kuchuliwa na Dokta Kaligita, kutoka Iringa kuja kufanya kazi za ndani hapa Dar es Salaam niliona ninapelekwa katika hali ya neema kimaisha na wazazi wangu walifurahi kwani walijua nikifanya kazi nitapata pesa na kuweza kuwatumia nyumbani Iringa. Walidhani hali yao kimaisha inaweza kubadilika. Matokeo yake mambo yalikuwa kinyume pale nilipofika Dar es Salaam na kufanya kazi ya kukata majani kwa ajili ya chakula cha ng’ombe na kufanya kazi nyingine za ndani kwa Dokta Kaligita, lakini sikuweza kupata hata pesa kidogo za kuwatumia wazazi wangu Iringa ingawa nilikuwa ninafanya kazi ngumu sana na kwa muda mrefu bila hata kupata nafasi ya kuweza kupumzika.

Niliteseka, niliteseka lakini ikanibidi nipige moyo konde nikitegemea ipo siku ambayo ninaweza kupata pesa lakini matokeo yake nilifanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja na matokeo yake nilifukuzwa bila kufanya kosa lolote lile. Sikupewa pesa hata Sh.1o; sikuwa na mahali pa kwenda wala pa kuweza kujihifadhi, sina ndugu hapa jijini.

Mambo niliyaona magumu na mazito. Nilijuta na kuona ni heri ningebaki huko huko nyumbani ingawa tulikuwa na maisha ya shida,lakini nilikuwa nafahamiana na majirani wengi ambao wasingesita kunisaidia. Nilijiuliza maswali mengi sana ambayo sikuweza kupata majibu:

Nifanyeje, niende wapi, nile wapi, nitafikaje Iringa sina nauli, hapa Dar es Salaam ni mgeni; sijui hata stendi panafananaje? Nimuombe nani msaada amabaye atanisaidia?

Hayo ni baadhi ya maswali ambayo nilijiuliza bila kupata majibu, hasa ukizingatia kuwa kipindi hicho nilikuwa na umri wa miaka 11. Katika hali hiyo nilihitaji msaada mkubwa sana kutoka kwa watu mbalimbali.

Niliamua kujichomoka kwa watoto yatima walio katika shirika la Feed and Tend Internatilanal (FTI) lililopo Kongowe, Temeke, ili niweze kupata angalau ugali na mahali pa kulaza ubavu.

Baada ya maelezo hayo mafupi, Mwandishi wetu alimtupia kijana huyo maswali.

Swali: Abbas, umesema kuwa ulipofukuzwa na tajiri yako uliamua kwenda kujihifadhi katika kituo cha kulelea watoto yatima. Unaweza kueleza kituo hicho kiko umbali gani na sehemu uliyokuwa unafanyia kazi?

Jibu:Sehemu niliyokuwa nafanyia kazi ni kwa Daktari wa hospitali ya shirika la Feed and Tend Internatianal na kituo hicho kinalea watoto yatima hivyo sikuona umbali wala ugumu wa kujiingiza katika kituo hicho ili niweze kupata hifadhi kwa kukosa sehemu ya kwenda.

Swali: Je watoto wa kituo hicho hawakukuona tofauti na wao kiumri?

Jibu: Nilionekena tofauti sana kwani hali niliyokuwa ilikuwa ni ya mzubao tofauti na walivyokuwa watoto wengine ambao wameishazoea kujumuika kwa pamoja hali ambayo mimi nilionekana mpweke sana.

Hata mwanzilishi wa kituo hicho alipofika alinishangaa kwa nini, mimi niko mpweke na kuniuliza maswali mengi.

Ukiwa uliokuwa umenitanda, uliomfanya mkuu wa kile kituo kunisogelea mpaka nilipokuwa akanishika mkono na kuniuliza maswali.

Maswali kati ya Mchungaji na Kijana yalikuwa ni kama ifuatavyo:-

Mchungaji: Wewe mtoto mbona huna furaha kama watoto wenzako, una matatizo gani? Na unaitwa nani? Mbona sura yako ni ngeni?, umekuja lini?

Kijana: Mimi ninaitwa Abbas Kihanza, (kilio...) Nimefukuzwa kwa tajiri yangu, sina pa kwenda kwetu Iringa. Sina pesa ndiyo maana sina furaha. Hiyo ndiyo sababu nimeamua kuja kujihifadhi hapa angalau nipate malazi na chakula. Sina ndugu mimi.. (kilio). Ndipo mchungaji (yule mkuu wa kituo)aliponichukua na kunifuta machozi na kunipeleka hadi nyumbani kwake na kuniambia kuwa nitakuwa naishi hapo kwake. Kwa kweli niliishi maisha mazuri ya upendo na kulishwa Neno la Mungu.

Tulikuwa tunasali kila asubuhi na usiku na pia kulikuwa na zamu za kushukuru wakati wa kula, kulala na tunapoamka. Nilipozoea walinipangia na mimi zamu ya kusalisha na mchungaji Michael aligundua kuwa sijui kusoma kwani nilishindwa kusoma hata kifungu kidogo cha Biblia.

Mchungaji hakupendezwa na hali hiyo. Alinitafutia mwalimu wa kunifundisha masomo ya Biblia na yale ya darasani baada ya kugundua kuwa sifahamu kusoma wala kuandika. Cha kushangaza, masomo ya darasani yalinichukua muda mrefu kuyafahamu tofauti na masomo ya Biblia ambayo niliyafahamu kwa muda mfupi sana.

Abbass anasema Mchungaji aliamua kumpeleka shule ya msingi Kongowe na kutokana na kuelewa kwake na umri hakusoma darasa la kwanza wala pili. "Nilianza moja kwa moja darasa la tatu kwa vile nilikuwa na umri wa miaka 12 na tayari nilijua mambo mengi ya masomo," alisema.

Gharama zote za kunisomesha zilitolewa na Mchungaji Michael, ambaye baada ya kumaliza darasa la saba aliamua kuniendeleza tena katika shule ya sekondari ya Dar es Salaam Christian Seminary (DCS) iliyopo Kongowe, hapa hapa jijini, ambayo ni ya binafsi. Mchungaji Michael ni mwanzilishi wa shule hiyo ambayo ni ya bweni na kutwa na ingawa ada ya bweni ni fedha nyingi lakini amejitolea kunilipia ada ya shilingi laki tatu kwa mwaka. Nashindwa nimlipe nini mchungaji kwa wema wake alionitendea na anaoendelea kunitendea hadi nitakapomaliza masomo yangu kwani kwa sasa bado niko kidato cha Pili.

Swali: Ukiwa kama kijana uliyesaidiwa na mchungaji katika kuyatengeneza maisha yako, je, unawashaurije vijana wenzako?

Jibu: Ninawashauri vijana wenzangu kote ulimwenguni wasijiingize katika mambo ya uhuni na wajishughulishe na kazi mbalimbali zilizo halali ili wakubalike katika jamii. Mimi binafsi kulingana na msingi niliojengewa na kulelewa na mchungaji na kupewa msaada na ukarimu nategemea na mimi kuwafanyia watu mema ambayo mimi nimetendewa bila kujali dini wala kabila. Ninaahidi kama mchungaji Michael Mugarura ambaye ni Mwanzilishi wa shirika la Feed and Tend International atawekwa hai nitajitahidi kumuomba ushauri zaidi katika maisha yangu na nitajitahidi siku moja nimpe shukurani yangu japo najua siwezi kumlipa.

Swali:Unategemea utakapomaliza masomo hayo utajishughulisha nini?

Jibu: Shughuli za kufanya ni nyingi sana lakini nategemea kufanya shughuli za kujiajiri hasa katika kilimo za biashara na nitajitahidi kuwasadia wale wote walio na matatizo mbalimbali kama mimi nilivyosaidiwa.