SERA YA ONGEZEKO LA WATU: Zimwi katili lisilojulikana Afrika

UNAPOLIMA shamba na ukaotesha mahindi, baada ya muda itakupasa kupalilia ili kuondoa magugu ambayo kwa kawaida huota humohumo na mara nyingi kustawi kuliko ile miche ya iliyokusudiwa. Hilo ni jambo la busara. Lakini je, unaweza kuamini kuwa wapo wanadamu wanaoamini kuwa baadhi ya wanadamu wenzao ni magugu miongoni mwao na kwamba wanastahili kuuawa ili wale wanaowaita 'watu halisi' wastawi? Je, unaamini kuwa yapo mashirika ulimwenguni ambayo yana heshima kubwa katika jamii na yapo hata hapa Tanzania ambayo yalianza juu ya msingi wa itikadi hiyo na bado yangali yakiitekeleza kwa siri? Je, ungependa siri zilizofichwa ndani yake? Mwl. GABRIEL MWAKAVELA wa CPT , Ifakara, Morogoro, anaeleza.

Kuna tofauti kati ya ‘Mpango wa uzazi kwa majira’ na ‘sera ya ongezeko la watu’. Mpango wa uzazi kwa majira ni nafasi kwa wazazi kuamua wenyewe na kwa uhuru juu ya idadi ya watoto wanayotaka kadiri ya mazingira yao.

Wanaamua muda wanaotaka wenyewe kupata watoto kadiri ya afya ya mama na watoto. Wanaelewa kuzaa ni kazi ya ndoa tu, na ndoa ni mwito mtakatifu kwa hiyo wazazi hawa wanafanya bidii kuwajibika katika familia zao.

Lakini lengo la sera ya ongezeko la watu ni kupunguza idadi ya watu kwa njia yoyote kama vile kulazimisha watu kufungwa uzazi na kuharibu mimba kwa njia mbalimbali za kisasa.

Tuangalie nchi ambazo watu wao walilazimishwa kuzuia uzazi au kutumia kemikali za kuua mimba.

India walilazimisha wananchi hasa wanaume kwenda kwenye makambi maalum (sterilization camps) na kufungwa kizazi na kupewa zawadi.

Huko India walitia dawa ya utasa katika tanki la maji ya kunywa. Hii ilisababisha Indira Ghandi kuangushwa wakati wa uchaguzi kwa sababu ya kukubali kuanzishwa kwa sterilizaion camps.

Nchini Indonesia, wanajeshi waliwalazimisha wanawake kupelekwa kwenye sterilization camps kuwafunga kizazi. Watu wanaopigia debe sera ya kupunguza ongezeko la watu (population politians) wanaonyesha jinsi wanavyodharau utamaduni, maadili na dini. Sera hii imeenezwa pote duniani, Marekani ya kusini, Asia,Ulaya na Afrika, lakini ukweli unabaki kwamba tunaoathiriwa zaidi ni sisi Waafrika.

HISTORIA YA SERA YA KUPUNGUZA ONGEZEKO LA WATU

Hoja za idadi kubwa ya ongezeko la watu zilianzishwa miaka 200 iliyopita na Thomas Robert Malthus ambaye alikuwa mtu wa dini na mchumi. Aliishi kati ya mwaka 1766-1834. Mtu huyu alifikiri mambo mawili:

Kwanza: Alifikiri kuwa jinsi watu wanavyoongezeka na mahitaji ya chakula yanahitajika maradufu zaidi ya idadi ile. Kwa hiyo akaamini kuwa jinsi wanavyoongezeka ndivyo kiwango cha uhaba wa chakula kitakavyokuwa kikubwa.

Pili: Malthus, aliona kuwa watu wenye mafukara sana hawana haki ya kuishi wala kupata msaada, hivyo njia ifaayo ni kuwaacha wafe tu ili idadi ya wanaohitaji chakula ipungue. Hata hivyo Thomas Robert Malthus hakuanzisha shirika la lolote la kufunga Uzazi.

SERA YA ONGEZEKO LA WATU YA MARGARET SANGER

Margaret Sanger ni mtu muhimu sana kuzungumziwa katika suala hili la sera ya kupunguza ongezeko la watu. Alikuwa Mmarekani mwenye asili ya Ki- Irish. Alikuwa mpinzani mkubwa wa maadili (radical anarchist). Yeye alimwacha mumewe na watoto watatu huko Marekani akaungana na mwasherati (sexualogist) Ellis Havelock huko London, Uingereza.

Lengo kuu la kumwacha mumewe na watoto lilikuwa kuwa huru katika tendo la ndoa.

Alitaka ndoa ambayo inaweza kuvunjwa kiurahisi tena bila kupata watoto.

Margaret Sanger, ni mwanzilishi wa itikadi ya Udhibiti wa Uzazi (Birth control). Aliweka malengo yake katika kuanzisha hiyo ‘birth control’ ambayo ilikuwa:

(a) Kupata watoto wengi kutoka watu wenye nguvu (fit)na wenye majukumu muhimu katika jamii, lakini wapunguzwe watoto kutoka kwa watu wenye udhaifu na wanaoonekana kuwa "hawana umuhimu mkubwa".

(b) Kupata watoto au watu wa pekee kwa kuwaondoa watu wenye udhaifu na wenye kukosa umuhimu.

Je, njia ya kuwaondoa ni ipi? Margareti Sanger, alihamasisha kuwafunga uzazi watu wengi wasioonekana kuwa muhimu. Mpango huu ukaitwa ‘polite genocide’ yaani mauaji ya kistaarabu.

Kwa Margaret Sanger, watu wenye udhaifu na wenye kukosa umuhimu ni watu wa namna wale ambao anawaita ‘human weeds’ akiwa na maana kuwa ni magugu ya kibinadamu. Magugu hayo kulingana na mawazo yake ni watu weusi, wayahudi, wahindi, watu mafukara, wasioweza kuandika, walemavu na watu wenye makosa ya jinai.

MWANZO WA MASHIRIKA YA ONGEZEKO LA WATU

Ili kutimiza azma yake, Margaret Sanger, alianzisha mashirika yafuatayo:

National Birth Control 1913. National Birth control League (Chama cha kitaifa cha kudhibiti uzazi)ilibadilisha jina baadaye na kuitwa Race Betterment League (Chama cha mpango wa kuboresha jamii ya binadamu). Siku hizi inaitwa ‘Planned Parenthood (Uzazi uliopangwa).

Margaret Sanger, alipendekeza kwa Serikali itoe zawadi yaani fedha, kwa wale wenye udhaifu (unfit) wanaokubali kufungwa kizazi.

Tutambue kuwa Margaret Sanger alitaka kuwaondoa watu si kwa sababu nyingine yoyote bali kwa sababu hawa ni ‘magugu.’

Yeye pamoja na wengine walianzisha IPPF (International Planned Parenthood Federation mwaka 1952.

Adolf Hitler

Mtu mwingine katika ‘unyama’ huu wa utamaduni wa kifo ambao wao walisema una nia ya kustawisha watu (Eugenics and polite) alikuwa Adolf Hilter. Yeye alitoa amri ya mpango wa kufunga kizazi kwa watu ambao alifikiri ni magugu kama vile vilema, Wayahudi na wengine.

Lengo la msukosuko wa kusitawisha wanadamu baada ya Adolf Hitler lilikuwa wazi mno.

Mwamko wa harakati za ongezeko la watu.

Baada ya Adolf Hitler waliupa mpango huo haramu jina la wazi kabisa wakiuita wa kupambana na ‘overpopulation’ (Idadi kubwa mno ya watu). Waumini wa sera ya ongezeko la watu (popupation politicians) sasa walianza kubadilisha maneno mawili: Ufukara na idadi kubwa mno ya watu (over population).

Walifikiria kuwa wakisema kuwa, Nchi ni fukara watu wake wangelazimika kufanya bidii kupata maendeleo katika uchumi. Na wakisema, ‘Idadi ya watu ni kubwa mno watafikiria kuwa idadi ya watu wenyewe ni matatizo na wanaweza kupunguza watu kwa njia yoyote kama, kufunga uzazi, kuharibu mimba na mpango wa kifo kisicho na maumivu kama vile:

Kuua wazee, wasiojiweza, wagonjwa wenye saratani(Cancer),walemavu na kadhalika ni mambo yanayopendwa na wanaharakati hawa.

Hitler alifanya kazi sana ya Euthanasia (kuua wazee, wasiojiweza, walemavu n.k)

Waliofanya jitihada ya kupunguza watu.

William Vogt, Makamu wa Rais wa Planned Parenthood wa Amerika kwa muda aliandika:

FAO (Shirika la chakula na kilimo duniani) likipeleka msaada wa chakula kwa nchi yenye idadi kubwa ya watu (over population) lipeleke pia vifaa vinavyohusu upunguzaji wa watu. Mtu huyo pia alipendekeza kutoa zawadi (fedha) kwa wale wanaokubali kufungwa uzazi.

Huge Moore aliamua kufanya bidii kupunguza watu. Aliandika kijitabu "The Population Bomb (ongezeko kubwa la watu) na kukipeleka kwa viongozi wa Amerika.

Viongozi hao walianza kutoa dola maelfu na maelfu baadaye mamilioni na mamilioni ili kuhakikisha kuwapo IPPF na mashirika yake.

Serikali ya Amerika ikahalalisha kitu inachokiita "Mercy Killing" (kuua kwa ‘nia njema’ ya kuhurumia) itumike nchini mwao na ichochewe kwenda sehemu nyingine duniani.

Mwaka 1969 Berson Memorandum inasema: Lazima kupunguza watu kwa kila njia mpaka kulazimisha na kutia dawa ya utasa katika maji na chakula.

Prof. Julian Simon, siku hizi alieleza kuwa ongezeko la uchumi linahitaji ongezeko la watu. Alitoa mfano wa nchi kama Taiwan, Hongkong, Korea Kusini na Japan. Nchi hizi zilionyesha ukweli wa Julian Simon.

Ulaya ambayo ina idadi kubwa ya watu tukichukulia mfano wa Ujerumani ambayo ina watu 245 kwa kila kilomita ya mraba ina maendeleo makubwa ya kiuchumi wakati Tanzania ambayo ina watu 22 kwa kila kilomita ya mraba ina shida ya chakula.

Inabidi tujiulize je, ni kweli ongezeko la watu lina uhusiano na kupungua kwa uchumi ( hasa kwa maana ya chakula)? Kwa nini fedha zinazotumiwa na mashirika kama UNEPA- United National Fund for Population Activities,USAID - United State Agency for International Development, IPPF- International Planned Parents hood Federation, WHO the World Health Organisation, IMF-International Monetary Fund na mengine hazitumiki katika kuinua kilimo?

Kwa nini wamekazania katika kupunguza idadi ya watu? Je, si vita dhidi ya nchi maskini?.

Sababu kubwa ya watu wa sera ya ongezeko la watu ni kupunguza Waafrika.

Kwanza kushusha idadi ya watu hasa upande wa kaskazini ambao ongezeko lao ni asilimia 95. Nchi za Magharibu zinahofu sana.

mwaka 1950 barani Ulaya ongezeko la watu lilikuwa asilimia 15.6, mwaka 1990 ongezeko lilishuka hadi asilimia 9.4. Na hadi kufikia mwaka 2050 inatarajiwa kuwa idadi hiyo itakuwa imeshuka hadi asilimia 4.9 kutokana na sera hiyo mbovu.

Hivi sasa Afrika ina watu milioni 750. Mwaka 1950 ongezeko lilikuwa asilimia 8.8, mwaka 1990 ongezeko lilikuwa asilimia 12.1 katika mwaka 2050 ongezeko litakuwa asilimia 22.6.

Ongezeko hili linazitia kiwewe nchi za Magharibi kwa sababu nchi za Kiafrika au Bara la Afrika litakuwa na:

w Uchumi ulioinuka au kupanda juu

w Afrika ya Kaskazini na Kusini watakuwa na nguvu kijeshi.

w Muungano wa Waafrika na Idadi kubwa ya watu itawaimarisha Waafrika

wna Utamaduni wa Ulaya utafifia.

Biashara ya madawa na vyombo vya majira

Watu wa Ulaya na Marekani wametumia madawa navyombo vya uzazi wa majira kwa muda wa miaka ishirini (20) iliyopita. Siku hizi wametambua madhara yake na kuacha kabisa. Wameanza kutumia au kufuata njia ya asili ya kupumzika kuzaa.

Biashara imepungua huko Ulaya na Amerika, kwa hiyo wanatafuta masoko mapya (New Market) sehemu nyingine. Madawa na vyombo ambavyo havitumiki Ulaya wala Marekani kwa sababu ya madhara yake vinapelekwa Afrika.

Kwa mfano Vitanzi vimesababisha matatizo mengi Marekani na Uingereza ambavyo yamesababisha wanawake kwenda mahakamani kulalamika na viwanda wamelipa fedha nyingi kwa wanawake kama adhabu.

Vyombo na madawa vinaletwa Afrika kwa sababu wanafahamu kuwa watu wa Afrika watashindwa kwenda Ulaya au Marekani kushtaki mahakamani.

Kwa kupata fedha zaidi watu kama hawa wanatoa dawa na vyombo vya majira kwa vijana ili kuwaamsha kufanya tendo la ndoa na kupata magonjwa ya zinaa na Ukimwi ili wafe wapungue.

 

 

Uchaguzi wa Kisiasa kwa nini tujali?

Oktoba, mwaka huu kutakuwa na Uchaguzi Mkuu wa pili wa Rais na Wabunge katika mfumo wa vyama vingi vya siasa. Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini kwa kushirikiana na Chama cha Wanataaluma Wakatoliki (CPT) wameona wanao wajibu kama vyombo vya kanisa kuwasaidia wananchi wazijue haki zao katika Uchaguzi huo na kutoka kitabu hiki ambacho tumeamua kukichapisha ili kuunga mkono hatua hiyo. Endelea na toleo hili.

Lengo la kutafuta cheo lisiwe ni kutafuta madaraka na mamlaka makubwa kupita kiasi, bali liwe ni kusaidia usimamizi mzuri wa madaraka na matumizi yake kiasi cha kuleta manufaa kwa Taifa zima.

Demokrasia haiwezi kukua kamwe kama wananchi wenyewe hawashiriki kikamilifu katika maisha ya kisiasa ama ya umma. watu hawapaswi kulalamika dhidi ya matumizi mabaya ya madaraka miongoni mwa viongozi kama wao wenyewe hawatashiriki katika shughuli za jamii wala katika kuunda sera. Kukosa msimamo wa kisiasa au kukaa kimya ni kikwazo kikubwa sana katika ujenzi wa Demokrasia ya kweli.

Watu ni lazima washiriki kikamilifu na wajifunze kujiunga pamoja na kushinikiza uongozi wa Serikali ngazi ya Taifa na sehemu wanamoishi kutekeleza matakwa yao. Bila ushiriki wa watu na kukosekana kwa mfumo wa wananchi kudhibiti Serikali hutoa mwanya kwa wale walio madarakani kuamua wanachotaka na kutekeleza bila kujali mahitaji ya watu wa kawaida.

Tunaweza kujiuliza sisi wenyewe, hivi tunapokutana katika mikutano ya kawaida ya kanisa au katika Kamati ili kutekeleza jukumu maalum la mahali fulani au katika sherehe nini uzoefu wetu.. Viongozi wa makundi hayo wanaonekana kuwa na tabia gani? Wajumbe wengine wanashirikianaje? Je wanasikiliza tu ama kueleza maoni yao au wanakaa kimya na baadaye kutoa maoni ya kukosoa na kulalamika kwa pembeni.

Ni kwa kiwango gani tunashiriki katika maamuzi ya pamoja ndani ya vikundi vidogo, ngazi ya kijiji au ya mtaa kwa mijini? Kwa kiasi gani tumejifunza kutetea matakwa yetu na kuunganisha nguvu zetu pamoja na vikundi vingine vyenye kuishi hali kama ya kwetu.

Lazima tuangalie hili kwani hivyo ndivyo tunaweza kujenga demokrasia ya kweli.

Demokrasia ni zaidi ya kupiga kura tu wakati wa uchanguzi. kwa upana kuwa mwana Demokrasia inamaanisha:

v Kuhimiza wengine kushiriki

v Kuhimiza wengine kutoa maoni yao kubainisha mtazamo wao katika jambo fulani na kuhamasisha washiriki majadiliano.

v Kutafuta njia za kupunguza matumizi mabaya ya madaraka.

vKuunda na kuunga mkono vikundi vinavyotetea na kulinda maslahi ya makundi maalum katika jamii.

vKujitoa nafsi yako ili kuweza kulinda na kuwasemea maskini, dhaifu na vilema katika kutetea na kulinda maslahi yao.

Demokrasia inapaswa kuweka muundo wa Kiserikali na kiutawala ambayo inaruhusu watu kupata huduma za watawala na watumishi wa Serikali. Tunahitaji Serikali na Tawala zenye urafiki wa karibu na watu toka ngazi za chini katika kutoa huduma za jamii elimu na afya. Kuwepo kwa muundo na uhusiano huu kunasidia viongozi wasiwe wanatumia madaraka yao vibaya au kukandamiza wengine.

Maswali:

i) Uchaguzi unapawa kuandaliwa na kuendeshwa kwa namna na misingi gani hivyo kwamba watu watakuwa tayari kuyakubali matokeo yake?

ii) Je, kwako wewe utakachopendelea na kuzingatia ni maoni ya chama chako ama ya watu wa Jimbo/eneo lako?

iii) Katika utendaji wako utatembelea eneo lako na kukutana na wananchi mara ngapi kwa mwaka?

iv) Je utakuwa tayari kushirikisha makundi yapi na watu gani kukushauri katika kazi yako?

v) Kama Chama chako hakitashinda na kuingonza Serikali, ni mbinu zipi utatumia kuwasilisha mahitaji ya watu wako na kutetea maslahi na matakwa yao Serikalini?

2. UONGOZI:

Ndugu Masanja ameishi Buhigo kwa miaka mingi alikuwa kiongozi anayeheshimika katika Kamati ya Kijiji na pia mwakilishi katika ngazi ya Wilaya alikuwa mtu mwaminifu na aliwapenda watu wake kwa kuwa tayari kutetea matakwa ya watu hata kama yanapingana na misimamo ya baadhi ya watu ndani ya Chama Tawala. Siku moja alipingana vikali na Mbunge wa eneo lao.

Katika Mkutano wa kuchagua mgombea wa Serikali ya Mtaaa kwa uchaguzi uliofuata Mbunge alizungumza dhidi ya ugombea wa Masanja akisema wote wanamshukuru kwa mchango wake aliotoa kwa miaka yote. Alisisitiza kuwa kwa wakati huu wanahitajika watu waliosoma na wenye uwezo wa kusoma nyaraka mbalimbali na kuzielewa pia wenye kumudu kubuni, kuandika na kuanzisha miradi . Kwa kauli ya Mbunge watu wakachagua mgombea mwingine kijana ambaye ni msomi na muda wake mwingi anaishi mjini.

Bila kutafakari undani ilionekana ni mwelekeo wa maendeleo lakini ukweli ni kwamba mbunge hakumtaka Masanja kwa kuwa namkosoa na anwatetea watu. Yote haya ili aweze kujitajirisha yeye binafsi. Masanja alikuwa kiongozi mzuri na hivyo hakutakiwa na wenye uchu wa madaraka.

Sifa ya kwanza Kiongozi si kuwa msomi wa diploma na anayejua mengi, bali cha msingi ni kuwa mtu mwadilifu mwenye kusimama katika haki na mwenye hekima. Kiongozi sharti awe anaamini kwamba mamlaka yote yanatoka kwa Mungu kwa manufaa ya wote na Taifa zima. Hana budi pia kuamini kwamba kuna thamani na maadili ya jamii yanayopaswa kulindwa ili tuweze kuishi pamoja kama jamii yenye kuthamini amani na yenye lengo la kumpatia kila mmoja mahitaji yake na haki zake za msingi ili kumwezesha kuishi kwa amani na utulivu.

Kama ilivyo kwa viongozi wote Viongozi wa Kisiasa wanapaswa kuwa watu wenye kushika maadili ya uongozi. Huna budi kuwa mtu anayetaka kuongoza jamii kufikia manufaa ya wote. Kiongozi mwadilifu ni yule anayeonyesha mfano mzuri ndani y a familia yake na ndani ya jamii kwa kuishi maisha maadilifu. Hii inamaanisha kwamba maneno anayoongea yajidhihirishe katika matendo yake . Kiongozi sharti awe;

Y Mtu mkweli na mwenye kujitoa

Y Mwenye kuwajibika na kujitoa kutimiza azma yake.

Maisha na Mikasa

Mchungaji aelezea alivyokuwa mwizi

lAsema aliwahi kuliibia Baraza la Maaskofu,

lMkewe alimtoroka na sasa ana mchumba

lMama yake mzazi alikufa kwa mgomo wa kula

Elizabeth Steven na Josephs Sabinus

" Nilipotoka Tunduma ambapo tulikuwa tunashona viatu na wenzangu, nilikuja huku Dar-Es-Salaam, hapahapa Kurasini. Nikakutana na marafiki ambao tulikuwa tunakunywa nao kwenye mabaa na kujadili dili."

Tukajenga uhusiano na walinzi wa magodauni mengi tu, tukiwapa pesa walau kidogo, walinzi wanaturuhusu tunaingia tunachukua vitu tunavyotaka halafu wanatusindikiza na hata siku hizi watu wanafanya hivyo hivyo.

Usinione hapa hata watu wa hapa huwa wananizomea eti ‘we Mushi nini wewe, tunakufahamu.’ Niliwahi kuiba hata pale Baraza la Maaskofu na Tanzania Road Haulage. Tukachukua mafriji, cherehani..."

Ndivyo alivyosema kwa kinywa chake mwenyewe Mchungaji wa Kanisa la Fire General Gospel International Church, lenye makao makuu yake eneo la Kurasini, Shimo la Udongo jijini Dar-Es-Salaam alipozungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita.Mchungaji huyo Samson John Mushi(44), anasema kabla ya kujitoa kumtumikia Mungu,alipitia vipindi fulanifulani vigumu na hata kujiunga na makundi ambayo yalimfikisha katika vitendo vya wizi na hata yeye mwenyewe anasema, aliwahi kuiba sana kwenye magodauni.

Miongoni mwa maeneo anayoyataja kuwa aliwahi kuyaibia ni pamoja na makao Makuu ya baraza la Maaskofu katoliki Tanzania (TEC), Tanzania Road Haulage,Sweedish Free Mission, na katika magodauni ya GAPCO.

Mchungaji Mushi anayedai aliachana na vitendo hivyo bada ya mara kwa mara kutokewa na msukumo wa kusali usiku kwa mwaka mzima na hivyo kuamua kuyabadili maisha yake, anaelezea mtiririko wa maisha na matukio yaliyompata.

" Mimi nilizaliwa mwaka 1956 huko Uru- Shimbwe kule Moshi. Ni mtoto wa tano katika familia ya baba, mzee John Kisarika na ,mama alifariki mwaka 1965 aliponiacha nikiwa darasa la pili huo ndio ukawa mwisho wa masomo yangu kabisa," anaendelea kusimulia.

Mama, alikuwa anaitwa Matemba. Aliniacha katika maisha ya kulelewa na mama wa kambo kwa kuwa baba alikuwa na wanawake wawili. Huyo mama wa kambo naye hivi sasa ni marehemu maana yeye alikufa mwaka 1980.

Gazeti hili lilipomuuliza sababu ya kifo cha mama yake mzazi kilichotokea akiwa na miaka tisa tu, Mushi alisema, "Unajua kulikuwa na kaka yetu mkubwa aliyeitwa Joseph Simpendi.

Hata mama na sisi wote tulikuwa tunamtegemea sana maana kwa kuwa baba alikuwa na wake wawili, matunzo kwetu yalikuwa ya shida tu. Huyo kaka ndiye alikuwa tegemeo.

Sasa mama aliposikia eti Simpendi ameangukia na mizigo bandarini (Dar), akagoma kula chakula kabisa.

Yaani alikataa akawa anajifunga kanga tumboni akitembeatembea barabarani, akiwa kama mwehu mpaka kiutaniutani akafa, hakuna aliyekuwa anaamini eti atavumilia njaa mpaka afe.

Na hiyo ni baada ya watu wa bandari kuleta vitu vyenyewe kule Shimbwe, wakamzika wenyewe huku Dar.

Anasema baba yao alielekeza mapenzi kwa watoto wa mke ndogo aliowataja kwa majina ya Tarisis, Denis, Bosco, Catherina (hivi sasa ni marehemu) pamoja na Joseph. Anaongeza kuwa wao walikuwa, Jeradi, Venance,marehemu Joseph (Simpendi), Mwajabu, yeye mwenyewe na mdogo wake Focus.

"Baada ya kuona maisha sasa yanakuwa hivyo hivyo, na hata kushindwa kuendelea kusoma, nikaamua kwenda Kahe, huko huko Moshi ambako niliajiriwa kwa mzee mmoja anaitwa Maiko, nikawa ninamchungia ng’ombe, ananilipa Sh.15.

Mwaka 72, niliamua kwenda Mombasa,Kenya, kumfuata kaka Venance ambaye alikuwa na biashara ya bucha ya nyama ya ng’ombe, lakini mwaka 73, kaka akarudi Moshi na kuniacha huko Mombasa nikifanya kazi kwa Mhindi.

Mwaka 1974, hii Jumuiya ya Afrika Mashariki ilipovunjwa, na mimi nikakimbia kurudi kwetu maana mipaka ilifungwa na watu wengi walikamatwakamatwa sana."

"Sasa,huko Moshi nikawa ninafanya biashara ya kuuza nyanya na viazi katika soko la Kahe.

Mwaka 1976, nikaja huku Dar na kufikia kwa ndugu yangu Richard Silayo, ambaye alikuwa anaishi KekoMachungwa.

Nikiwa hapo kwake alinisaidia sana nami nikawa ninashonashona viatu hadi mwaka 1977, katika maeneo ya Msimbazina Mtaa wa Uhuru pale keep left. Hata hivyo ingawa hatukukosana kabisa na Silayo, niliamua kukaa kwa ndugu yangu mwingine huko Ubungo, maana naye alikuwa fundi viatu kama mimi. Na hii niliiamua kwa makusudi tu, ili nipate akili ya kujitafutia."

"Mwaka uliofuatia, nikaenda Tabora na kisha Tunduma, kote huko nilikuwa naendelea na kazi hiyo hiyo ya kushona viatu, tena huko Tunduma, mpakani mwa Tanzania na Zambia.

Sasa huko ndipo mambo yalianza kunichanganya akili kidogo maana sikujua ni kwanini, lakini nikawa ninawaacha mafundi wenzangu ambao tuliungana, mimi nikawa nakuja Dar es Salaam. Kutafuta mali za kushona viatu tunauza, nikipata ninatuma, mimi nabaki huku.

Sasa hata neno la Mungu linasema kuwa ukikaa na mwenye hekima, utakuwa na hekima lakini ukikaa na mpumbavu, na wewe utakuwa mpumbavu." Mchungaji Mushi, akatulia kidogo, kisha akaendelea tena kusimulia.

"Sasa nilipokuwa nakuja huku Dar-Es-Saalam, tena huku Kurasini, nikawa nakutana na vijana wengi, tukawa tunaongea,tunakwenda kwenye mabaa. Sasa wakawa wananiambia, "bwana kama una pesa, tufanye biashara." Nikaona ni sawa; si tunatafuta pesa bwana!

Tukawa tunakwenda kwenye magodauni mbalimbali na bandarini, tunafanya misheni na kuchukua vitu, kisha tunaondoka kwenda kuuza. Siyo siri, mimi nasema wazi na hata watu wote wa hapa Kurasini wanajua mimi Mushi nilikuwa mwizi kweli. Hata siku hizi huwa wananitania "we Mushi, utatuambia nini wakati tumeiba wote, halafu sasa hivi unajidai umeokoka."

Tulikuwa tunaingia,tunafekenyua makufuli mpaka yanafunguka au tunayakata kabisa na kuweka mengine."

Alipoulizwa ni kwanini walikuwa wanaweka makufuli mengine, Mchungaji Mushi alisema, "Unajua haya mambo wala asije akudanganya mtu kwamba walinzi huwa kweli wanalinda. Tulikuwa tunawapa pesa tunaingia, tukishindwa kufungua,tunavunja halafu tunaweka jipya ili wakubwa wao wasishituke.

Tulikuwa tunachukua vitu vingi vingi sana. Kama haya mafriji na vyerehani. Tumechukua sana, lakini cha ajabu pamoja na vitu vyote hivyo, hakuna pesa iliyokaa ikatulia walau kufanyia jambo.

Alipotakiwa kutaja maeneo aliyowahi kushiriki uhalifu huo wa wizi na kisha kuulizwa anajisikiaje sasa kama anaweza kurudia, alisema, "kati ya mwaka 1980/81 tuliwahi kuiba Baraza la Maaskofu, wakati huo walikuwawanalinda Wamakonde na ndio tulioshirikiana tukachukua Friji na mitumba. Hata kabla DAPCO halijafa wakati magodauni yake ya kule Chang’ombe.

Alipozidi kuulizwa kama aliwahi kujeruhi au kujeruhiwa katika maisha yake ya uhalifu, Mchungaji huyo wa anachokiita Fire Gospel International Church, alisema, "Nakuambia isingeweza kama kukamatwa wakati walinzi wa magodauni hayo ndio walikuwa hata wanatuambia siku ambazo kuna hali nzuri.

Tena ukikuta sehemu inayolindwa na hawa askari(akimaanisha majeshi), hao ndio wanatulinda na hata wanazuia watu wengine wasipite karibu.

Hata hivyo, mimi namshukuru Mungu kuwa sikuwahi kuibia mtu binafsi, wala kujeruhi na hata mimi mwenyewe sikuwahi kujeruhiwa.

Nakumbuka ni siku moja tu, walinzi wa bandari walikosea kidogo, wale tuliopanga nao, wakafanya kosa nikakamatwa na walinzi wengine.

Anasema wateja wao walikuwa ni watu ambao mpaka sasa ni watu maarufu kibiashara na anasikitika kwamba ingawa walikuwa wanawapatia mali nzuri na za thamani, bei ambayo alikuwa anawalipa, ilikuwa ni kichekesho. (hataki kuwataja). "Wateja ni watu matajiri mno. Mpaka sasa ndio wanaowatuma vibaka na kununua mali za wizi; ndio wateja hao. Ila kibaya mno, ni bei wanayolipa kweli wanalipa vibaya mno na ndiyo maana wanatajirika kwa kasi.

Nakuambia wizi hautaisha kwa sababu wanaolinda ndio wanaoshirikiana na wezi bila watu wote kumkubali Mungu katika maisha yao. Kwa sababu hata maaskari magari yao ndiyo mengine wanayatumia kufanya mambo haya.

Akiendelea kuelezea historia ya maisha yake, Mchungaji Samson Mushi, anasema, mwaka 1990 (hakumbuki siku wala mwezi), alianza kuandamwa usiku na hali iliyokuwa ikimsukuma kuomba na kila mara mwenyewe kujiona mdhambi mbelea za watu "Hali iliendelea kwa karibu mwaka hivi, maana nilikuwa nikiweka kichwa kitandani tu, najisikia vibaya kabisa mpaka usiku huo mara nyingi saa tisa, naamka kufanya maombi na ndipo najisikia vizuri na kupata usingizi.

Mara nyingi nilikuwa namwambia Mungu anitoe kwenye shimo. Sikuwa ninajua ni shimo gani kila wakati ninalitaja lakini baada ya kuokoka, ndipo sasa nimejua ni zile dhambi.

Siku moja nikapata taarifa za mkutano wa Injili kule Jangwani(Dar), ambapo kulikuwa na Mhubiri kutoka Uganda anaitwa, Kayanja. Nilikwenda mkutanoni siku ya tatu.

Siku hiyo walipoita wanaotaka maombi sikwenda , siku ya pili pia hivyo hiyvyo, lakini ghafla nikaanguka nilipokuwa nimesimama na mwavuli wangu, huku nikipiga makelele. Baada ya maombi, nikajisiia mwepesi.

Kutokaana na mabadiliko niliyoyaona kwangu baada ya kukiri moyoni kuachana na vitendo vyote kinyume na mapenzi ya Mungu, niliporudi nyumbani, niliwapiga marufuku wale vibaka wenzangu wote; wasije kwangu tena. Wakawa wananizomea eti wewe Mushi unajidai umeokoka wakati hujatajirika, tutaona utafika wapi. Mimi sikujali la mtu.

Nikawa najishonea mabegi na vitu vingine ninauza.

Kweli ghafla sijui ni kwanini, kweli vile vipesa nilivyokuwa napata, vikaanza kupotea taratibu. Hata shemeji yangu nikampa mabegi ya biashara ya sh. 55,000/=, kwa wakati huo zilikuwa nyingi, alipoondoka kwenda kuyapeleka Shinyanga, hakurudi tena. Sasa vikawa vinapotea kwa njia hiyo hiyo.

Ndipo hata Mke wangu mwanamke mmoja wa Kinyiramba, alikuwa anaitwa, Evarina Makupa(Mama Matemba),watu wakamwambia eti nimeokoka tutakufa maskini na hata yeye alipoona chai tulikuwa tunakunywa maziwa yenyewe sasa hatuinywi , akaamini mambo yao, akakimbia na kuniachia watoto wawili wadogowadogo baada ya wengine wawili wa kiume kufariki.

Nikabakiwa na Salome ambaye sasa hivi yupo Keko Magurumbasi na Beatrice ambaye amemaliza darasa la saba huko Moshi. Tangu aondoke imepita miaka kumi sasa hata nimekwisha pata mchumba mwingine ambaye nitamuoa Mungu akipenda.

Hata hivyo alipoulizwa endapo mke wake huyo tajirudi akamrejea na hali siku hizi hali ya ukimwi ni mbaya zaidi itakuaje, alisema, "Mke yeyote nitakayeamua kukaa naye, lazima, lazima tufunge ndoa kabisa siyo kukaa hivi hivi.

Masuala ya ukimwi kwa mke huyo na yeyote , mimi najua kwa Mungu kila kitu kitawezekana, siwezi kumuacha eti kwa kuwa ameugua , ili mradi tu akiri kwa moyo na athibitishe kuwa sasa ataishi maisha ya kiMungu. na hapo naamini hata huo ukimwi utajiishia wenyewe bila madhara."

Wakati huo nilikuwa naabudu EAGT kule Mnazi Mmoja , mambo niliyoyaona huko, kama watu hatutabadilika kiroho, sijui. Nikaona uokovu wangu utapotea bure kwa kuwa mimi sikuokoka kwa ajili ya kukimbia matatizo wala ugonjwa wengine huokoka wakikata tamaa au ili wapate misaada.

Nikahamia Temeke ambako nilikuwa naandika jumbe zangu mbalimbali, lakini nilipotaka ziandikwe jina la kanisa zinapotoka, Mchungaji aliyekuwapo wakati huo akakataa hasa baada ya kupendekeza ziitwe Fire Gospel, akasema hata kam ingekuwa Foolish Gospel."

Sasa ndipo nikaamini kwamba huwezi kusimama shamba lingine ukalima lingine, maana ukitaka kulima shamba lazima usimame kwenye shamba hilohilo.

Ndipo nikaanza kufanya ibada peke yangu na kuanza kupata wafuasi. Wakati huo nilikuwa nimepanga kwenye hii nyumba(anaonesha nyumba ya jirani).

Kisha anendelea, "Kutokana na niliyoyaona, sitaki mtu anayeitwa mlokole aje kanisani kwangu." Alipoulizwa kuwa haoni alikuwa anafanya kosa la kuwatenga wenzake, alitulia na hata kukataa katakata kutaja madhambi aliyoyaona kwenye madhehebu hayo mengine.

Anatoa ushauri kwa madhehebu ya Kikristo na jamii kwa ujumla kujiunga pamoja ili kufanya kazi za kumfurahisha Mungu badala ya wenyewe kwa wenyewe kuzidi kumegeka na kutoshirikiana katika Kristo.

Anasema anashangaa kwa baadhi ya madhehebu kuanza kubagua Wakristo wengine na kuwaona si chochote, wala si lolote na kwamba Neno la Mungu ni moja."

Yesu ametupa kila kitu ili tuwe na umoja duniani kama ilivyo mbinguni, kwa kuwa mambo ya ajabu yanayofanywa na baadhi ya waamini wa madhehebu kadhaa, yanampa shetani mwanya wa kutuvuruga.