Kumsaidia mtoto mwenye mazoea ya kujitenga

KATIKA shule ya watoto wadogo, tunaweza kuona watoto wengine ambao hupenda kujitenga na wenzao. Kwa kawaida watoto wa aina hii huwa na tabia ya woga, huona haya kwa kila kitu, na hivyo hupenda kunyamaza kimya wakati wote.

Hata baadhi yao hushindwa kunena kitu wanapoulizwa na mwalimu ingawa swali lenyewe si gumu. Watoto wa aina hii hucheza michezo peke yao na hukataa kujiunga katika michezo ya vikundi vya wenzao. Hawataki kuongea na watu, kama wakilazimishwa kufanya hivyo basi huonekana kuhangaika na kukosa la kusema.

Watoto wa aina hii huficha mawazo yao na hushindwa kuwasiliana na watoto wenzao. Kwa wajihi wanaonekana watiifu sana na wazazi huwasifu kwa utiifu wao. lakini kwa undani, watoto wa aina hii huwa na kinyongo na mashaka mengi moyoni, huwa na tabia ya ukaidi na unyonge. Watakapokuwa watu wazima hukosa uwezo wa kuyakabili maisha na hali ya kijamii. Hushindwa kuwasiliana na wenzao na wengine hata wanashindwa kuchunga maisha yao ya ndoa. Kwa mujibnbu wa uchunguzi, tabia ya kujitenga hutokana na sababu mbili: Sababu ya kwanza ni udhaifu wa neva alizozaliwa nao. Udhaifu huu humfanya ashindwe kujizoesha na mazingira yoyote. Sababu ya pili ni malezi yasiyofaa ya utotoni, yaani ama upendo uliopita kiasi au ukosefu wa u pendo wa wazazi. aina zote mbili za hulka ya upendo huweza kusababisha tabia ya kujitenga kwa watoto. Wazazi wengi hutunza watoto wao kama mboni za macho. daima huwa na wasiwasi kuhusu hali ya watoto wao. Wanahofia mambo kama vile wasije wakaanguka na kuumia au wakagombana na wenzao n.k. Hivyo hupenda kuwafungia nyumbani bila kuwaruhusu kutoka nje. Wazazi wa aina hii huhiari kuwanunulia watoto wao vitu vya kuchezea kwa gharama kubwa kuliko kuwaachia huru hata kwa dakika chache. Ijapokuwa watoto hao hupata kila kitu kimaisha,lakini daima hutawaliwa na upweke. hali kama hii ikiendelea kwa muda mrefu, watoto hupoteza maumbile yao wakawa na tabia ya kujitenga.

Kwa kawaida, watoto watimiapo umri wa miaka mitatu, huanza kuwasiliana na watoto wenzao,huonyesha hamu ya kujiunga na wenzao lakini bado hawajaweza kushirikiana vizuri nao katika michezo. Lakini kwa kupitia mawasiliano ya aina mbalimbali, kama vile kugombana kushindana au hata kupigana, watoto huanza kuwafahamu wenzao wa rika moja hatua kwa hatua. wafikapo umri wa miaka mitano, hujua jinsi ya kutendeana na watoto wenzao, hufahamu adabu na unyenyekevu na wakaweza kuwasiliana na wenzao kirafiki na kushirikiana nao vizuri katika michezo kwa muda mrefu.

Hivyo ukitaka kumfunza mtoto wako awe na tabia na mazoea mema, uwezo wa kuyazoea mazingira ya kijamii, ujuzi wa kuwasiliana na watu wengine, inakubidi umwache ashirikiane na watoto wenzake tangu utotoni ili wapate ujuzi na maarifa katika kuwasiliana na watoto wenzake. Hii ndio njia ya kumwezesha mtoto huyo kujielimisha mwenyewe kwa wenzake.

Ikiwa mtoto ameshakuwa na mazoea ya kujitenga wazazi wanatakiwa kumsaidia kubadilisha mazoea hayo au wanaweza kushirikiana na walimu wa shule katika shughuli hiyo hata hivyo wakati wa kusaidia wazazi hushirikiana na walimu wote wanapaswa kuangalia mambo yafuatayo:

A. Wazazi au Walimu wamtendee mtoto kwa upendo, utulivu na upole ili mtoto ajihisi yu salama na asiwe na wasiwasi hata kidogo.

Mtoto mwenye mazoea ya kujitenga huwa mnyonge na mwoga, hivyo ni mwiko kumlaumu kwa maneno kama vile "Mbona unashindwa kufanya jambo dogo kama hilo! Mpumbavu wee!" Maneno hayo humfanya mtoto azidi kuwa na wasiwasi na upweke na hayaleti faida yoyote itakayomsaidia mtoto. Njia sahihi ni kujaribu kuwashirikisha kuwaongoza hatua kwa hatua ili kujenga mawazo yenye welekea wa amani usalama na shwari.

B. Msaidie mtoto kupata mwenzake, mshajiishe kuwasiliana na wenzake na mwache achague rafiki wa kucheza pamoja kama apendavyo.

kufanya michezo ni njia iwezayo kuwashirikisha watoto pamoja na pia inaweza kuwasaidia kuwasiliana. hivyo wazazi wanashauriwa kuwakaribisha nyumbani watoto wa jirani na wengine ili wacheze pamoja, waimbe kama wapendavyo, wasimuliwe au wasimuliane hadithi, wachore na kubuni mambo. Wakati wanapofanya hivyo huweza kumfanya mtoto ajue jinsi ya kuwasiliana na wenzake na awe na hamu ya kuwasiliana nao.

C. Mvumilie mtoto hata kama analia kwa sababu gani. Ikiwa mtoto amegombana na wenzake katika kucheza kwao na akalia hapo ni mwiko kumlazimisha mtoto wako kurudi nyumbani pia si busara kushutumu au kumdharau kwa kumwambia 'mjinga' au 'mpumbavu'. Bora jifanye kama hukusikia wala hukuona kisa kilichotokea ili kuwapa nafasi ya kutanzua hitialafu yao wenyewe na waweze kuendelea kuwasiliana kirafiki.

D. Msadie mtoto kufaulu kuachana na mazoea ya kuwategemea wazazi. Mtoto anayezoea kujigenga hupenda kuwategemea wazazi wao kwa kila kitu na huwa mnyonge na kujiamulia na kujitegemea kimaisha.

Hivyo wazazi wasijifanye watumishi wake wa kumfanyia kila kitu.Mtoto akiendelea na tabia hii mpaka shuleni, watoto wenzake humchukia na hivyo kuongezekewa na upweke. Hivyo wazazi wanashauriwa kuwafundisha watoto wao kufanya mambo yao kwa kujetegemea na kuwapa nafasi ya kufanya kazi ndogondogo kuwa na afya njema kimawazo na kiwiliwili.

ZIJUE IMANI ZA WENGINE

Uislamu ulivyopenya nchini China (2)

Kwa hiyo mfalme hiyo akamtuma mjumbe wake kwenda nchi ya Tazi na kumwomba Mtume Muhammad (Saw) alete watu wake kueneza dini nchini China.

Muhammad akakubali ombi hilo akalea wnafunzi wke watatu, Bahati mbaya wawili kati yao walikufa safarini na kuzikwa katika mlango wa bahari wa Xingxing, mjumbe mmoja tu ndiye aliyefika China na akakaa nyumba ya wageni katika mji mkuu Changan.

Mjumbe huyo siku zote alikaa kimya na kufanya ibada , siku moja mfalme alipata wasaa na akajifanya kama ofisa wa kawaida, akaena kumtembelea akamkuta mjumbe akikariri Kurani kwa makini huku akielekea upande wa magharibi. Alipomaliza kusoma aya moja akaufunga msahafu wa Kurani, akaueweka polepole juu ya rafu halafu akatoka mlangoni akiw ana tabasamu usoni akisema "karibu ndani mwadhamu. Niwie radhi kwa kuchelewa kukupokea" Mjumbe akacheka bilaya kujubu hivyo watu hao wawili wakakaa kitakio wakishikamana mikono na kuanza kuzungumza. Mfalme alitaka kupima akili zake akatoa masuala kadha wa kadha, mjumbe akamjibu akamjibu sawasawa bila wasiwasi. Mfalme huyo alifurahi sana akamruhusu kukaa kwa muda mrefu huko mji mkuu Changan kueneza dini ya Kiislamu.

Baada ya miaka mingi mjumbe alifikiri sana nyumbani kwake, akaomba kurudi kwao lakini akakataliwa na Mfalme. Baada ya hapo akatoa tena ombi hilo Mfalme baada ya hapo akatoa tena ombi hilo. Mfalme akajisemea kimoyomoyo akipapasapapasa ndevu zake, "Inanibidi kutafuta njia ya kumbakiza" kwa kushauriwa na Mfalme, mjumbe akamwoa msichana mrembo na hakurudi tena kwao. Alijitolea maisha yote kwa ajili ya uenezaji wa Uislamu katika China.

Mabishano mbalimbali kuhusu wakati wa kuingia Uislamu nchini China

Wakati wa kuingia kwa Uislamu nchini China kiungo muhimu cha kujua kwa usahihi historia ya Uislamu katika China. Wakati huo pia umekuwa ni suala linalotakiwa kutatuliwa na wasomo wa Uislamu katika China. wakati huo pia umekuwa ni suala linalotakiwa kutatuliwa na wasomi wa Uislamu. Lakini kitu kinachosikitisha ni kuwa katika suala hilo historia ya China na ya nchi za nje hazina nyaraka za kutosha kuwatolea watu jawabu lililo sahihi. Kwa hiyo mabishano mbalimbali juu yake yanatokea mara kwa mara na haujapatikana uamuzi wa mwisho. Kwa ujumla yamekuwapo maono zaidi ya kumi kwa sasa maoni yaliyoko ndani ya kitabu kilichotolewa mwaka wa pili wa Yonghui wa Enzi wa Tang,

Vipindi viwili vya Uingiaji Uislamu Nchini China

Si rahisi kujua miaka gani hasa Uislamu uliingia nchini China.

Tunaweza tu kukadiria kipindi fulani katika historia.

a) Uingiaji wa Uislamu

Nchini China katika Enzi ya Tang na ya Song

Watu walioleta Uislamu nchini China si wale maharamia wa Kiislamu bali walikuwa ni wafanyabiashara Waislamu.

Uislamu uliendelea taratibu sana nchini China, nao ulichukua muda wa miaka mia saba au nane hivi ndipo ulipoanza kustawi na kuota mzizi. Uislamu kwa msingi ni aina moja ya dini inayoshikilia na si rahisi kutolewa nchini China. Baadhi ya watu wanasema kwamba kuanza kwa Uislamu katika China ni matokeo na dalili ya urafiki wa China na nchi za Kiarabu. Usemi huu una sababu zake.

Urafiki kati ya watu wa China na nchi za Kiarabu ulianzia miaka ya kale sana. Katika enzi ya Han baada ya Zhang Qian aliyekuwa mjumbe kupelekwa kwenye sehemu za magharibi njia ya usafiri wa biashara kati ya China na sehemu za Kaskazini Magharibi nayo si nyingine bali ni njia ya hariri iliyojulikana duniani kote na njia ya mnikato kwenye sehemu za pwani ya kusini mashariki.

Njia hizo mbili zilileta mabadilishano ya utamaduni wa kale kati ya China na nchi za Kiarabu.

Uislamu ulianza kufana mwishoni mwa Enzi ya Sui na Enzi ya Tang ya China. Inasemekana kwamba ili kuwashajiisha waumini wa Kiislamu kujenga urafiki na kuongeza ujuzi Mtume Muhammad (SAW) alitoa funzo takatifu lisemalo "Ingawa China iko mbali sana na lakini kwa manufaa ya kupata ujuzi mnastahili mfike" maneno hayo yanadhihirisha kwamba mwanzilishi huyo wa Uislamu alikuwa akipenda sana ustarabu wa kale na urafiki mkubwa kwa watu wa China.

Kwa sababu ya kuenea kwa Uislamu na kuanzishwa kwa nchi ya kifalme ya Tazi wafanyabiashara Waislamu wamefululiza kuja nchini China wakikiuka milima na mabonde na kuvuka bahari. miaka ya mwanzoni ya Enzi ya Tang wafanyabiashara hao waliweza kuonekana kila pahala katika mji mkuu wa Changan.

Kwenye soko la magharibi na la mashariki la mji huo maduka ya Waislamu yalianzishwa sana na watu wa Tazi na Uajemi yakiuza pembe za ndovu pembe za vifaru, marashi , vito ambavyo ni mali ya Asia ya Magharibi na Afrika.

Yasiyo ya Kawaida

Kutana na Paka tajiri kuliko wote duniani

lAnamiliki jumba la Kifahari na gari la fahari

lAnayo mamilioni ya Paundi kwenye akaunti yake benki

Na Masha Otieno Nguru JR

NI jambo la kushangaza kuwa wapo wanyama matajiri kupita hata binadamu ambao wamepewa upeo wa hali ya juu wa kiakili kuwapita wanyama wenyewe.

Mengi yamesimuliwa kuhusu mbwa tajiri kupita wote duniani ambaye anaishi huko Milano Italia pia masikio ya walimwengu yalisikia na macho yao kuona kwenye televisheni wakati Mahakama Kuu nchini Australia ya dola zilizorithishwa na tajiri mmoja wa huko kwa mbwa wake aliyempenda sana.

Kitendo hicho kilichochukuliwa na raia walio wengi wa Australia kuwa kama dharau.

Hivyo baada ya tajiri huyo kufa fedha chache tu ndio alibakizwa Mbwa huyo kwenye akaunti yake na zilizo nyingi zikachukuliwa na Serikali kusudi ziende kuwasaidia maendeleo ya jamii.

Lakini kana kwamba hayatoshi leo hapa baada ya kupekua hapa na pale tunazo paha habari za paka tajiri na Milionea kupita binadamuu na mapaka wenzake.

Hadi tukiingia mwaka huu wa 2000 tuliopo na Barney ya kuwa tajiri kupita mapaka wengine wote duniani na binadamu wengi tu.

Barney Paka mdogo mweusi ambaye bado ni mtoto anaishi huko Gloucester nchini Uingereza pamoja na utajiri mkubwa wote alio nao paka huyo ajabu ni kuwa kwa sasa anamilikiwa na Kisichana kidogo chenye umri wa miaka 3 tatu kwa jina la Sophie Chiu.

Sophie ambaye humpenda paka huyo upeo alimrithi kutoka kwa bibi Kizee mmoja Catherine Rodman aliyekuwa akiishi jirani nao maajabu ni kuwa bibi Kizee huyo asiye na watoto ambaye sasa amezeeka kupita kiasi kituo cha kulelea vikongwe ameuandika urithi wake wote kwa paka huyo.

Mali alizoandika apewe kama urithi paka huyo ni pamoja na jumba lake la Kifahari lililoko hapo Gluocester gari lake aina ya Rolls Royce na akaunti yake benki yenye Paundi milioni 20 za Uingereza.

Imetokeaje basi mtoto mdogo Sophie akamrithi paka mwenye utajiri mwingi kiasi hicho?

Mama wa mtoto huyo Bi. Claire Chiu analijibu swali hilo kama alivyohojiwa na jarida la 'Rolling Stone'

'Mwanangu alipendana sana na Bi. Kizee huyo na mara nyingi alimsaidia kumlisha na kumsafisha paka huyo , bila shaka hilo limechangia'

Paka huyo hivi sasa anaishi na familia ya Sophie na binti huyo.

Barney ni Paka ambaye amekuwa gumzo kwenye vyombo vya habari ndani na nje ya Uingereza.

Ili kuhakikisha kuwa maharamia hawamteki paka huyo tajiri kama kigezo cha kujioatia donge nono.

Chama cha wanyama wa kundi la mamalia nchini Uingereza 'Mammal Society of England' wamemuajiri mlinzi wa kuangalia usalama wa paka huyo mahala popote anapokuwepo.

Hata anapotoka kwenda matembezini na rafiki yake Sophie ndani ya gari la kifahari paka huyo huwa chini ya Uangalizi maalum.

Inashangaza kuwa wakati hapa Afrika tunahangaika kung'oa umaskini katika nchi zilizoendelea wapo paka na mbwa tajiri kupita hata matajiri na wasomi wa Kiafrika.

Makanisani Wiki hii

Sumaye kuzindua Kanisa la Kilutheri Ukonga

Na Agatha Rupepo, DSJ

WAZIRI Mkuu Bw. Frederick Sumaye Jumapili hii anatarajiwa kuweka jiwe la msingi katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), usharika wa Ukonga jijini.

Kwa mujibu wa mchungaji wa kanisa hilo, Marko Ndumi aliyezungumza na Mwandishi wa habari hizi katika ofisi za Kanisa hilo Ukonga jijini, ujenzi wa kanisa hilo litakalozinduliwa na Waziri, ulianza mwaka 1994 kwa nguvu za waumini baada ya kuona kanisa lililopo ni dogo chini ya mchungaji wa kike, Deborah Manyerere.

Alisema hadi lilipofikia sasa, kanisa hilo, limekwisha gharimu kiasi cha shilingi milioni 55/= zilizotokana na michango ya waumini.

Aliongeza kusema kuwa ili ujenzi wa kanisa hili ukamilike zinahitajika shilingi milioni 80/= zaidi.

Alisema katika sherehe hizo za kuweka jiwe la msingi, kutakuwa na harambee kwa ajili ya kuchangia kutunisha mfuko wa ujenzi wa kanisa hilo.

Sherehe hizi za uwekaji wa jiwe la msingi zitahudhuriwa pia na Askofu Jerry Mngwamba wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ya KKKT.

Wakati huo huo: Kanisa la Kiinjili la Kilutheri ,Usharika wa Ukonga linatarajia kuanzisha chama cha kuweka na kukopa kwa vijana.

Mchungaji Marko Ndumi amesema mpango wa kuanzisha chama hicho ni kuwasaidia waumini waweze kujiajiri wenyewe katika shughuli ndogondogo.

"Serikali sasa hivi haiajiri wafanyakazi, hivyo kupitia chama hiki vijana wataweza kujiajiri wenyewe kwa kuweka na kukopa kutoka katika chama hicho" alisema Mchungaji Ndumi.

Alisema mbali na chama hicho cha kuweka na kukopa kanisa linatarajia kuanzisha darasa la ufundi seremala na uashi ili kuwasaidia vijana wanaomaliza darasa la saba na kushindwa kuendeleza na masomo ya sekondari waweze kujiajiri wenyewe baada ya kupata mafunzo hayo.

Aliongeza kusema kuwa ujenzi huo wa darasa la ufundi utakwenda sambamba na ujenzi ya shule ya awali kwa ajili ya watoto na waumini na watoto wengine. Kutokana na tatizo la maji jijini Dar Es Salaam, Kanisa pia limeamua kuchimba kisima ili kuwasaidia wanafunzi wa darasa la shule ya awali waweze kupata maji karibu. Pialina mpango wa kujenga ukumbi wa mikutano na Hosteli.

Maisha na Mikasa

Mlokole aeleza yaliyomkumba na kusema:

l Waganga wakampa baba mbuzi ili amuue lakini, kibao kikanigeukia mimi

lUsiku kucha watu walikuwa wananikaba koo

l Niliponea chupu chupu lakini sasa, nina jicho la ‘mbuzi’

Na Dalphina Rubyema

"Najua walitaka wanisaidie lakini kumbe... masikini sijui mganga aliwambiaje maana hata mama hataki kuniambia ukweli lakini, usinione hivi nimetoka mbali. Kifo nimekiona machoni na hata hili jicho langu..."

"Sikupenda hata kidogo mambo ya ushirikina hivyo nilikuwa najisikia vibaya sana mama alipokuwa akinieleza kuwa wazazi wangu walijihusisha katika mambo hayo na matokeo yake ndiyo hili jicho langu kama la mbuzi"

Ndivyo anavyosema Bi. Maria Longino alipomsimulia mwandishi wetu kisa cha yeye kupata ulemavu wa jicho na hatimaye kuokoka ambapo sasa ni muumini wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) la Galilaya, Tabata jijini Dar Es Salaam.

Maria ambaye ni mkazi wa Tabata Aroma, jijini anasema kuwa sababu kubwa iliyomfanya aokoke ni mambo ya ajabu yaliyokuwa yakimsumbua wakati alipokuwa kijijini kwao Isimani Mkoani Iringa.

Akisimulia kwa ufupi fupi mkasa uliomfikisha alipo sasa, Maria anasema, "Nilipokuwa mdogo huko Iringa, usiku nilipokuwa nikilala, nilikuwa ninakabwa kooni na watu ambao nilikuwa siwafahamu ingawa nilikuwa ninawaona kabisa na ninashindwa kuzungumza wala kutoa sauti yoyote."

"Hali hii ilikuwa inaninyima usingizi usiku kucha. Nilikuwa sipati raha wakati wote maana nilikuwa sasa naogopa hata kuingia ndani hata mchana."

Anasema kutokana na hali hii wazazi wake; Mzee Longino Kidungu na Bi. Elizabeth Muleleu walimshughulikia sana wakimtafutia matibabu ili kuondokana na hali hiyo.

"walinipeleka kwenye hospitali nyingi lakini wapi hata nasikia kwa waganga wengi wa kienyeji walifika lakini hakuna walichonisaidia. Hali hii ilikuwa inanikatisha tamaa mno maana mtu ninashinda mchana wote sina raha ; usiku ukifika naanza kuogopa." anasema Maria.

Anasema siku yaliyomkuta makubwa, ni siku ambayo baba yake mzazi,Mzee Lengino, aliondoka nyumbani asubuhi na mapema (hakumbuki ni lini).

Anasema aliporejea nyumbani kwao akiwa na mbuzi begani na alipomfika eneo la nyumba yake alimtupa kwa nguvu mbuzi huyo akitaka amuue kwa kumbamiza mtini lakini masikini kitendo hicho kikamrudi na kumdhuru Maria ambaye kwa wakati huo alikuwa akimsaajabia baba yake kuja na mbuzi.

Bado Maria ambaye alipatwa na Kisanga hicho akiwa bado mdogo sana anasema kuwa hakufahamu Baba yake huyo mbuzi alimpata wapi na alikuwa na maana gani kumrusha chini kwa nguvu na badala ya huyo mbuzi kufa hali ikamgeukia yeye.

"Hapa sijui baba alikuwa na maana gani maana hata mimi nilikuwa mdogo... hata hizi habari nimesimuliwa na mama," anasema.

"Ingawa sikujua ni kwanini baba alifanya hivyo, lakini mama aliponisimulia siku nyingine, nasasa hivi ninavyojua mambo, najua labda mganga ndiye alimwambia afanye hivyo, labda pengine walidhani ningepona".

Anasema kitendo cha Mbuzi kurushwa kwa nguvu kilimsababishia yeye Maria kuanguka chini ghafla na kupoteza fahamu hapo hapo na ndipo akapelekwa katika hospitali mbalimbali lakini ilishindikana.

Anasema katika harakati za kuokoa maisha yake wazazi wake walimleta katika Hospitali ya Rufaa Muhimbili ambapo alipatiwa huduma na baada ya kukaa kwa kipindi kisichopungua wiki moja huku alishwa kwa mipira ndipo alipoweza kufungua macho na ndipo akajigundua amepa kilema cha maisha katika jicho moja la kulia.

bado Maria ambaye alipatwa na Kisanga hicho akiwa bado mdogo sana anasema kuwa hakufahamu Baba yake huyo mbuzi alimpata wapi na alikuwa na maana gani kumrusha chini kwa nguvu na badala ya huyo mbuzi kufa hali ikamgeukia yeye.

Anasema baada ya kupatwa na mikasa kama hiyo aliona hakuna haja ya kusubirisubiri dawa ni moja tu ya kuokoka na ndipo alianza kumfuata Bwana mnamo mwaka 1998.

Hata hivyo Maria ambaye ni mfanyakazi wa nyumbani jijini Dar Es Salaam, anasema kuwa pamoja na kwamba yeye ameokoka wazazi wake ni watumiaji wazuri wa kileo.

"Mimi na dada yangu Anna Longino ambaye anakaa Iringa Mjini tumeokoka lakini baba na mama ni walevi mno nikimwambia mama aokoke, anasema la maana nimwombee kwa Yesu uzima lakini yeye hawezi kuokoka na kuachana na pombe lakini nina imani kuwa ataokoka" anasema Maria.

Yafuatayo ni mahojiano ya Mwandishi na Maria mwenyewe.

Mwandishi: Maria, nipe historia ya maisha yako?

Maria: Nilizaliwa mnamo mwaka 1981 katika kijiji cha Isimani huko Iringa. Kwetu, mimi ni mtoto wa tatu katika familia yetu ya Mzee Longino Kidungu na Bi. Elizabeth Muleleu yenye jumla ya watoto wanne.

Mwandishi: Nini kilikufanya uokoke, au wewe ni miongoni mwa wanaookoka kwa kufuata mkumbo na au kukata tamaa ya maisha?

Maria: Mimi sifuati mkumbo wa mtu. Nimeokoka baada ya kupata mikasa mbalimbali nikaona namna ya kumshukuru Mungu ni kumtumikia.

Kwa kuanza kukupa mikasa yangu ni kwamba usiku nilipokuwa nimelala nilikuwa nakabwa na watu ambao wanadhaniwa kuwa wachawi.

Hali hii ilipoendelea ilibidi dada yangu Anna anayeishi Iringa, mjini anichukue na kuishi naye huko.

Dada yangu huyo alikuwa ameokoka tuliishi huko tangu 1994-1995 baada ya muda huo wazazi wangu walinichukuwa tena vijijini kwa nia ya kuwasaidia kazi kwani kulikuwepo na mgonjwa ambaye ni dada yangu marehemu Loyisia.

Nilipokuwa huko nilianza kukabwa tena na wachawi kitu kilichowafanya wazazi wangu wajiingize katika mambo ya ushirikina ingawa hata sasa mimi sipendezwi ninaposikia au kukumbuka mambo hayo. Hivyo, nilitamani sana kuokoka kama dada yangu Anna.

Hata hivyo kwa kipindi hicho, nilishindwa kufanya hivyo kwa vile wazazi wangu walilipinga sana suala hili la kuokoka.

Mipango ya Mungu hashindwi. Siku moja tukiwa nyumbani kwetu Iringa alifika dada mmoja aliyeitwa Rose ambaye alikuwa anatafuta mfanyakazi na baada ya kuniona mimi aliniombea ruhusa kwa wazazi wangu.

Wazazi wangu bila hila walikubali ombi la Rozi, hivyo nikawa nimekuja naye Mwanza sehamu ya Nyamanolo ambako alikuwa akiishi.

Baada ya kufika Mwanza, dada Rozi ambaye alikuwa ni mfanyabishara wa samaki alinionyesha ukarimu na kwa ujumla maisha ya pale nyumbani hayakuwa mabaya kwani hakukuwepo na kazi nyingi pale tulikuwa tukiishi watatu tu yaani mimi, Dada Rozi mwenyewe na mtoto wa dada yake aliyeitwa Luka (4).

Hali ilikuja kubadilika ghafla badala ya kuona raha katika mji wa Mwanza sasa niliona karaha kwani sasa dada Rozi alibadilika. Alianza kuninyanyasa, kunipiga kipigo ambacho kilizidi hata kile anachopigwa mwizi.

(Alitulia akanitazama kwa mshangao kwa macho yaliyohitaji kuungwa mkono)

Nakumbuka kuna siku moja dada Rozi alinipa dawa ya miti shamba ninywe nami kwa vile sikujua inatibu nini niliikataa.

kitendo hicho kilimuudhi sana alinitoa nje na kunicharaza hadi damu ilitoka puani.

Nilitamani sana kutoroka lakini jambo kubwa lilikuwa juu ya nauli.

Kwa vile sikuwa na mizigo, nilichukua sh. 50 ambayo ilibaki kwenye hela ya mboga siku hiyo.

Nikapanda daladala, na kwa vile nilikuwa sijaufahamu vizuri mji wa Mwanza, nikaona nitapotea hivyo nikateremka katika kituo kilichofuatia.

Nikaanza kuulizia penye kazi; nyumba hadi nyumba na kila niliyoingia kuomba kazi, nilikataliwa katakata.

Nadhani ni kufuatia maelezo niliyokuwa nikiyatoa maana nilikuwa nikieleza kila kitu kilichonipata kwa dada Rozi.

Mungu hamtupi mjakazi wake baada ya kupita nyumba kadhaa bila kupata kazi nilifanikiwa kumpata mama mmoja ambaye hakunitajia jina lake ambaye kwa vile jua lilikuwa limeanza kuzama alinikaribisha nyumbani kwake na kuniambia kuwa nikae pale nitulie.

Nilikaa pale na kumsimulia mama huyo mkasa mzima ambapo alisema atanirudisha kwa Rozi.

Baada ya hapo kesho yake tulipanda gari lakini baada ya kuteremka kwenye kituo nilichopandia siku nilipotoroka nilishindwa kuelewa njia ya kwenda kwa dada Rozi hivyo huyo mama aliona anisalimishe kituo cha polisi naye kuondoka zake.

Huko nyuma Rozi alinifuata na kufanikiwa kunikuta polisi.

Kesho yake dada Rozi alikata tiketi ya treni na kunileta kwa kaka yake ambaye alikuwa anaishi eneo la Kinondoni Moscow jijini..

Baada ya kunifikisha Kinondoni Rosi alirudi Mwanza nami kuendelea kuishi pale Kinondoni.

Nikiwa Kinondoni nilipata habari kuwa kuna Kanisa moja la walokole wa Kipentekoste ambako lilikuwa karibu na pale nilipokuwa nikiishi kwa vile nilikuwa nimeisha pata mikasa ya kutosha niliona hiyo ni sababu tosha ya kunifanya niokoke hivyo nikaenda kwenye hilo Kanisa na kubatizwa kama Mlokole na huo ni mwaka 1998.

Baada ya kukaa Kinondoni kwa kaka yake Rozi nilifanikiwa kupata kazi ya ‘U-house girl’ hapa kwa mama Collins eneo la Tabata Aroma ambako nafanyakazi bila usumbufu wowote na ninasali katika kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) la Galilaya Tabata.

Nimeokoka na nampenda Bwana.

Mwandishi: Sijasikia ukitaja lolote kuhusu hilo jicho lako, hivi ulizaliwa hivyo ama ni kilema ambacho ulikuja kukipata baada ya kuzaliwa?

Maria: Mmmh! Acha tu dada (Mwandishi). Huu ulemavu wa jicho niliupata baada ya kuzaliwa. Mama yangu ndiye alikuwa akinisimulia ilivyokuwa mpaka nikapata hiki chongo.

Mama alikuwa akiniambia kuwa nilipokuwa mdogo baba alikuja na mbuzi begani kutoka kwa waganga wa kienyeji.

Alipofika, alimdondosha chini kwa nguvu kwa nia ya kumuua lakini kitendo hicho, kikanigeukia, kikanifanya nianguke chini na kuzimia kwa dakika hiyo hiyo.

Wazazi wangu wote walinipeleka katika hospitali ya Iringa bila mafanikio. Ndipo baadaye wakaamua kunileta Muhimbili nilipopata matibabu na kufanikiwa kufungua macho ambapo nilipata kilema hiki kwani baada ya kufungua jicho hili la kushoto lilionekana kama nimewekewa jicho la mbuzi.

Mwandishi: nadhani huyo mbuzi alikuwa ni wannini na kwanini alikudhuru wewe?

Maria: sikuambiwa alikuwa ni wanini lakini binafsi nadhani ni hizo imani za kishirikina na Mungu kudhihilisha kuwa hazifai ndio maana mimi nikadhulika.

Mwandishi: Je wazazi wako wameokoka?

Maria: Wazazi wangu hawajaokoka ni watumiaji wazuri sana wa kilevi nikimwambia mama aokoke ananijibu yeye hawezi kuokoka na kuacha pombe.

Mwandishi: Unaonaje maisha ya ulokole?

Maria: Kwa kweli ni mazuri mno na namshauri kila mmoja aokoke.

"Ndugu mwandishi hili jicho langu siyo kwamba lilitoka na kuwekewa jicho lingine hapana yote mawili yalikuwa mazima ila baada ya kuugua kwa muda mrefu bila kufumbua macho siku nilipoyafungua ndipo nilipo nilipojikuta hivi" anasema Maria na kuelekeza kidole kwa jicho lake la upande wa kushoto ambalo linaonekana kama aliweka jicho la Mbuzi