Njia ya kumshupaza mtoto mwoga

KWA kawaida binadamu yeyote hupenda kutiwa moyo na hujisikia vibaya anaposhutumiwa, japo anaweza kukosolewa kistaarabu asijisikie vibaya. Kwa watoto wadogo umakini zaidi unahitajika kuliko ilivyo kwa watu wazima kwa vile wanahitaji kutiwa moyo kwa kila wanalojifunza ili wajenge tabia ya kujiamini. Kuwashutumu kila mara kuna madhara makubwa kuliko faida. Endelea na Mfululizo wa makala zetu kutoka kitabu cha Shirika la Uchapishaji wa Lugha za Kigeni la Beijing, China juu ya Afya.

"Je unaweza kutuambia njia yoyote itakayofanikisha kumshupaza mtoto mwoga?" Tuliwahi kuulizwa swali kama hili mara nyingi na wazazi vijana waliokuja kwenye kliniki yetu ya saikolojia iliyoanzishwa maalum kwa ajili ya kutolea maelekezo.

Wazazi kama hao hulalamika kuwa mtoto wao ni mwoga sana na huku hujieleza jinsi walivyo waangalifu sana katika kumtunza mtoto huyo Tunafahamu sana hamu waliyonayo ya kutaka kupatia mtoto wao afya njema ya kifikra na kimoyo na pia tunaelewa wasiwasi wao juu ya upungufu unaowezekana katika tabia ya mtoto wao iwapo hawatapewa ushauri unaostahili.

Siku moja tulitembelewa na baba mmoja mwenye mtoto. Baba mtu alisema: "Mwanangu ana umri wa miaka mitano sasa, tumegundua kwamba kuwa mwoga tangu alipokuwa na umri wa miaka mitatu,. labda sababu yenyewe iliyomfanya awe hivyo ni kwamba tuliwahi kumtisha kwa kumtajia chui au dubu wakati tulipojaribuku kumnyamazisha kilio chake cha deko. Lakini baadaye tulijua ubaya wa kutumia njia ya kumtishatisha, hivyo tukaacha. Lakini mtoto anazidi kuwa mwoga na hata hathubutu kwenda msalani au jikoni mwenyewe" Nilimuuliza "Je nyie wazazi mliamua kufanya nini wakati mtoto wenu alipoonekana kuwa mwoga?".

Baba huyo akanijibu: "Tulijaribu kumbembeleza kumdekeza na kumpa chakula kitamu anachokipenda"

Nilimwambia kwamba wazazi wenyewe ndio waliosababisha mtoto wao kuwa mwoga. Si vizuri kumtisha mtoto mdogo na ni vibaya zaidi kumbembeleza na kumdekeza kupita kiasi wakati mtoto anapoogopa kitu au jambo fulani. Kwa kumfanyia vitendo vya namna hiyo woga wa mtoto wao huzidi. Baba mtu aliniambia waziwazi kwamba hakuweza kuelewa vyema sababu niliyomwambia. Ilimbidi nimsimulie jaribio tulilofanya: Mtoto mdogo aliachwa chumbani peke yake,halafu tukamwingiza paka chumbani humo kwa kupitia tundu la ukutani. Mwanzoni mtoto alionekana hana hofu yoyote kuhusu paka yule, na hata alijaribu kumshika mkia na kumchezeachezea. Baadaye mfanya jaribio alimtoa nje paka, halafu akamwingiza chumbani tena lakini safari hii paka alipojitokeza chumbani mfanya jaribio alifanya kishindo kwa kupiga sakafu, kishindo chake kikamtisha mtoto, na jaribio hilo lilirudiwa mara nyingi, mpaka baadaye mtoto alipomwona paka tu akawa na hofu hata bila kusikia kishindo chochote.

Kipindi cha pili cha jaribio hilo kiliendelea baada ya muda fulani ambapo mtoto huyohuyo aliachwa chumbani tena peke yake na wakati paka alipoonekana tu mtoto aliona hofu, na wakati huo huo mfanyajaribio alimletea mtoto chakula kitamu na vitu vya kuchezea na wakati paka alipotolewa chumbani, chakula na vitu vya kuachezea navyo pia viliondolewa. Paka akionekana tena chakula na vitu vya kuchezea hurudishwa tena kwa mtoto, vivyo hivyo, kila mara akionekana mwishowe mtoto akawa hana hofu tena na paka hata bila ya kuuletewa kitu kitamu.

Sasa baba mtu akafahamu na kusema "Ah hatimaye nimefahamu. Kumbe ni kosa kumsaidia mtoto kukwepa shida yake bali inapasa kumfundisha njia ya kuikabili shida hiyo mtoto akipata chakula kizuri na kuengwaengwa wakati akiwa na hofu basi atazoea hali ya kuwa na hofu kwa vile anaona kuwa hofu yake humletea faida na hivyo atazidi kuwa mwoga"

Kwa kweli wazazi wengi hufanya kosa hilo hilo katika kumfundisha mtoto wao. Kwa mfano wazazi wengi huzoea kusema, "Pole kipenzi, isiwe na hofu, nipo hapa mama yako. Njoo nitakupa kitu kitamu" Lakini kubembeleza kwa namna hiyo kumfanya mtoto kuwa mwoga na huwa mnyonge wa kujitegemea na hushindwa kabisa kupambana na shida yoyote katika maisha yake.

Basi nini njia ya kumsaidia mtoto mwoga kuondoa shida yake? nilimweleza:

Kwanza fahamu kuwa nini hasa mtoto wako anachoogopa, na jaribu kumpa mwongozo unaofaa. Halafu fanya jaribio la mafundisho kwa mujibu wa fikra zoeshi (conditional reflection) Wakati mtoto anapoonekana kuwa na woga wazazi hawana haja ya kumtupia macho sana, badala yake wanaweza kujifanya kutotia maanani woga wake na wakati huohuo jaribu kumshajiisha kupamba na kitu anachoogopa kama vile kumwambia mtoto aende chooni au jikoni peke yake n.k Akishafanya hivyo msifu au mtunukie. Hususan mtoto anapoonekana mshupavu wakati wa kawaida wazazi wasichelewe kumsifu na kumtumikia. Vivyo hivyo majaribio ya mafundisho yarudie rudie kwa mara nyingi na mwishowe mtoto wako hatakuwa mwoga tena.

Lakini jambo la kuzingatia zaidi ni kwamba wakati wa kufanya majaribio inapaswa uchukuliwe tahadhari ili mafundisho yasiwe magumu kupita kiasi hata kikamtisha mtoto badala ya kumshupaza. Bora shauriana na daktari kwanza kabla ya kuanza mafundisho hayo.

Miezi miwili baadaye baba mtu alinipigia simu na kuniambia kwa furaha kwamba mtoto wao si mwoga tena lakini alisema kwamba pengine atalazimika kuuliza swali la "nitafanyeje ikiwa mtoto wangu ni jasiri kupita kiasi?"

ARSENI MKUU: Aliwapiga watu butwaa kwa kulilia makosa ya wengine

Na Josephs Sabinus

INGAWA wapo Watakatifu wengi na huku idadi yao izidi kuongezeka siku hadi siku, bado Kanisa linaendelea kuwatangaza watu wenye sifa muhimu za kuitwa Wenyeheri na Watakatifu.

Hata katika misa na sala rasmi za Kanisa ni wale Watakatifu walio muhimu kwa jumuiya ya waamini ndio hukumbukwa mitume waanzilishi wa mashirika ya Watawa kama Fransisko,Domino na Inyasi.

Hali kadhalika Watakatifu kama Teresia Mtoto wa Yesu wa Lisieux Teresia wa Yesu wa Avila, Ambrose na wengineo wengi wa namna hiyo.

Wapo pia wafiadini wa nchi mbalimbali kama vile wale wafiadini wa Uganda. Japan Amerika ya Kaskazini na Korea ambao ni muhimu kwa maisha yetu na katika kuthibitisha umuhimu wa Kanisa Katoliki katika mataifa.

Watakatifu wa namna hiyo ndio watakatifu ambao Kanisa na watu wake wote linaendelea kuwataja na kusimulia maisha yao kwa ufupi na kwa kadri ya mapokeo yaliyopatikana.

Leo katika safu yetu hii ya Watakatifu tunamuona Mtakatifu Arseni Mkuu ambaye alikuwa mkaa pweke na huyu hukumbukwa kila mwaka ifikapo tarehe ya 20 ya mwezi Julai wa kila mwaka.

Katika siku hii (Julai 20) Mtakatifu Arseni anakumbukwa na kanisa sambamba na Watakatifu wa Afrika kama vile akina Sabinus, Lusianus, Petrus, Agrripinianus, Nonina, Rospestatus, Salvus na Medadulus waliokuwa wafiadini wa Afrika Kaskazini, Mtakatifu Viktoria aliyekuwa mfiadini wa Misri pamoja na Mtakatifu Aurelius aliyekuwa Askofu wa Tunisia.

Arseni Mkuu aliyezaliwa katika ukoo uliokuwa na wabunge wengi katika dola ya Roma mwaka 355. Hivyo, kwa asili yake alikuwa mtu mashuhuri hasa kufuatia umashuhuri wa Ukoo wake.

Tunaelezwa kuwa katika Ukristo wake, alifanikiwa kupata daraja la Ushemasi na kisha akaombwa kuhamia Ikulu huko mjini Konstantinapoli Uturuki ili aende kuwa mkufunzi wa wana wa Kaisari Teodosia.

Na ndivyo alivyoamua pia kuhamia Ikulu ilipoelekea miaka ya 410 hivi ili apate kurudi jangwani Misri na hata kujiunga na Wamonaki.

Inaelezwa kuwa katika miaka yake ya kwanza ya utawa aliiona migumu sana kwake kutokana na ukweli kwamba tayari yeye alishazoea maisha ya raha kule Ikulu.

Lakini kadri alivyozidi kuzoeana na Wamonaki wengine hata kwa muda wa miaka kadhaa hadi kufikia kuishi na kuyazoea kabisa maisha ya Jangwani aliamua kujinyima zaidi na kukaa peke yake kabisa.

"Hawaendelei mbele kwa kuwa hushikilia elimu ile ya kuwafanya wajivune lakini wale wengine wasiosoma wanaelewa maana halisi ya unyonge na upungufu wao hali ya namna hiyo humfanya mtu azifuate fadhila za Mungu na kufaulu"

Ndivyo Mtakatifu Arseni alivyomjibu siku moja mgeni aliyekuja kumtembelea jagwani alipomwambia kwamba inamshangaza kuona kuwa watu wenye elimu hawaendelei sana kuishi kifadhila hali wasio na elimu kabisa ndio wanaofaulu na kukomaa kiroho.

Kwa mujibu wa waandishi wa Zamani tunaaombiwa kuwa kulingana na desturi za Wamonaki Arseni alifanya malipizi mengi na makali sana huku akijinyima mno chakula na kwamba mara nyingi alikesha usiku mzima kwa sala.

Ripoti zilizoenea juu ya ada zake ziliwapiga butwaa wale wote waliozisikia na hii ni kutokanana namna alivyojikalifisha sana kwa njia mbalimbali.

Mtakatifu huyu Arseni Mkuu mwenyewe aliwahi kujieleza hivi " Kila mara baada ya kuongea, nina kitu fulani cha kusikitikia, lakini sijawahi kusikitika hata mara moja nilipo kaa kimya"

Waandishi hao wa zamani wanazidi kusisitiza kuwa makosa ya Arseni mwenyewe na yale ya wengine mara nyingi yalimfanya alie machozi kwa jinsi alivyokuwa akiyahuzunikia sana.

Hata katika kitabu cha Zaburi (119:136) imeandikwa hivi : "Macho yangu yabubujika machozi kama mto;kwa sababu watu hawashiki sheria yako".

Hata ulipofika wakati wa kufa kwake inaelezwa kuwa Wamonaki walimuona akilia machozi; wakamuuliza Baba! kwa nini unalia? Je hata wewe unaogopa kufa?"

Mtakatifu Arseni akajibu akasema "Ndiyo kuogopa naogpa sana nimekuwa nikiaogopa tangu nije huku Jangwani" Akisha kusema hivyo, akakata roho Akafariki katika hali ya utulivu mkubwa huku akiwa na umri wa miaka 95 baada ya kuishi jangwani kwa miaka 40 na huu ulikuwa ni mwaka 450.

TOLEO MAALUM LA SEKTA YA USAFIRISHAJI

OILI ZA BARABARANI NI HATARI

Breki na Ajali za Barabarani:

Pamoja na kuwapo na ajali nyingi barabarani mara kwa mara sababu zinazoleta ajali hizo nyingine hazijaangaliwa kwa undani; hivyo kusababisha ajali kuendelea kupoteza maisha ya watu, mali na kuleta mikanganyo mbalimbali.

Ubora wa mafuta ya Breki ni mojawapo ya sababu zinazochangia kwa kiasi kikubwa ajali na ikahusishwa na uzembe wa dreva.

Gari linapokwenda kasi hata kwa mwendo ulioruhusiwa, uwezo wa dereva kudhibiti gari kwa kulisimamisha na sehemu anayotaka ni muhimu sana katika safari ya salama . Udhibiti huu unategemea ubora wa mfumo wa breki za gari husika. hasa hasa ubora wa mafuta ya breki. Ubora huu unategemea aina viwango vya mafuta, yanavyotunzwa na kutumika.

Gari inayobidi kukanyaga breki mara mbili au tatu ili breki zifanye kazi, inapunguza uwezo wa dereva kudhibiti gari. Inapungua uwezo wa kusimamisha au kupunguza mwendo wakati na muda anaotaka hivyo kusababisha pengine ajali. Ajali kama hizo mara nyingi zinatajwa kama ni uzembe wa dereva.

Makala hii inazungumzia utunzaji na utumiaji wa mafuta ya breki unavyoweza kuwa chimbuko la ajali lisiloonekana.

Mafuta ya Breki:

Kwa wengi huonekana kama mafuta ya breki ni bidhaa ya mafuta inayotolewa na kuuzwa na makampuni ya mafuta. ukweli ni kwamba mafuta ya breki ni madawa.

Hii inaelezea kwa nini bidhaa hii iko chapter tofauti na mafuta ya oili katika rasimu ya (Customs classification code) na labda neno sahihi ingekuwa madawa ya breki au maji ya breki.

Ni jamii ya madawa zinazohimili nyuzi joto hadi 300o C na ina tabia ya kufyonza maji (unyevu unyevu) kutoka kwenye hewa (hygroscopic).

Tatizo la Mafuta ya Breki:

- Tabia yake ya kufyonza maji kutoka kwenye hewa inaleta tatizo la utengenezaji, utunzaji na utumiaji wa mafuta ya Breki. Tatizo ni kubwa zaidi sehemu ambazo kiwango cha unyevunyevu ni juu kama mikoa ya Pwani, hasa Dar es Salaam na kwingineko.

Mafuta ya Breki yaliyoachwa wazi yanavuta maji na kuchanganyika nayo.

- Tatizo la pili ni joto la utendaji kazi. Mkandamizo wa breki unasababisha msuguano ambao unaweza kupata joto hadi kufikia 300oC. Kiwango hiki cha joto hufanya maji yaliyomo ndani ya mafuta ya breki kugeuka kuwa mvuke au hewa. Hewa ndani ya mafuta ya breki yanafanya breki zisifanye kazi au ufanisi wake upungue.

Tumezoea kuona mafundi wakitoa hewa kwenye mafuta ya breki "breeding" wakati wanatengeneza breki za magari. lakini hewa inayotokea baada ya joto kufikia 100oC na zaidi inakuwa haijaondolewa.

Mvuke (vapour) ndani ya mafuta ni moja ya sababu kubwa zinazochangia magari kushindwa kukamata breki wakati yanatembea hivyo kusababisha ajali nyingi kutokea.

Baya zaidi ni kwamba dereva anaweza asiwe na tahadhari kwamba breki zake hazifanyi kazi vizuri. Nchini kwetu tunahitaji kufanya uchunguzi kujua ukubwa wa tatizo litokanalo na mvuke ndani ya mafuta ya breki.

Suluhisho:

Suluhisho lake ni kujitahidi kutumia mafuta ya breki salama kwa kupunguza uwezekano wa mafuta ya breki kufyonza maji kutoka hewani.

Hii inawezekana kwa mtumiaji:

-Kununua mafuta yaliyofungwa moja kwa moja (sealed cans)

-Kutumia kopo mara moja na kutupa

-Kujua viwango vya mafuta ya breki salama

Mapendekezo haya ni mtu binafsi mwenye gari, fundi au dereva anaweza kuzingatia na yakamsaidia. Hata hivyo kuna mambo ambayo yako juu ya mtumiaji kama:

-Endapo mafuta yaliyofungwa (sealed) sio salama au,

-Kuwapo kwa mafuta ya breki yasiyo salama kama mafuta yanayouzwa barabarani.

Kuondokana na tatizo hili pengine taasisi kama TBS. kamati ya Taifa ya Usalama wa Barabarani na mamlaka za leseni n.k kuingilia kati hasa kudhibiti na kupiga marufuku:-

i) Uuzaji wa mafuta ya breki yasiyo salama, kupiga marufuku kupima au kuuza mafuta ya breki yaliyo wazi.

ii) Kuchunguza kiwango cha maji kilichomo kwenye mafuta ya breki yanayouzwa hapa nchini.

iii) Kuchunguza mara kwa mara viwanda vinavyofunga mafuta ya breki kama kweli vinazingatia utaalamu unaohitajika na vina nyenzo sahihi.

Mafuta ya breki yanapaswa kutengenezwa (yapakiliwe, yapakuliwe na kufungwa) kwenye mazingira maalum - sehemu isiyo na hewa (under Hydrogen vacuum) Uwezekano wa kuwa na teknolojia hii hapa nchini ni mdogo.

Na hii inaleta swali kubwa kwa kiasi gani,

MAFUTA YA BREKI YANAYOFUNGWA NCHINI NI SALAMA?

G.Nshekanabo

STAR LUBRICANTS (T) LTD

ZIJUE IMANI ZA WENGINE

Uislamu ulivyopenya nchini China

Na Mwandishi Wetu

KUNA hadithi mbili zinazoongelea jinsi Uislamu ulivyopenya nchini China ambako kumekuwa na Wakomunisti wengi wanaopingakuwepo kwa Mungu. Hadhithi ya kwanza inaeleza kwamba mfalme wa Enzi ya Sui (589-604) Yang Jian, siku moja usiku aliiona nyota iliyong'ara sana hata ikambidi amtume mtaalam wa kupiga ramli kuhusu nyota hiyo. Mtaalam huyo alisema kwamba nyota hiyo ni dalili ya kutokea mtu wa ajabu huko nchi ya Tazi (nchi ya kifalme ya Kiarabu), hivyo basi mfalme alipeleka mjumbe kwenda nchi hiyo ili kufanya uchunguzi juu ya ukweli wa tukio hili. Mjumbe huyo alifika huko baada ya msafara mrefu wa mwaka mmoja.alipoonana na Mtume Muhamad (Saw), mjumbe huyo alimwalika kuja China, lakini Muhammad alikataa kwa shukrani, na akamweleza sababu yake.

Wakati huo huo aliwatuma wajumbe wake wanne kufuatana na mjumbe huyo alipoona kwamba Muhammad alikataa mwaliko wake akachora kisirisiri picha yake na akarudi nayo nchini.

Alimkabidhi mfalme picha hiyo na kumjulisha wajumbe wanne aliofuatana nao.

Baada ya kusikia maelezo ya mjumbe na kuiona picha ya Muhammad (Saw) mfalme alifurahi mno,mara moja akatoa amri ya kuitundika picha hiyo ndani ya kasri yake na kutaka kumwabudu, Mjumbe mmoja akamzuia asifanye hivyo akisema "Mtume Muhammad (Saw) ametufundisha tusiiabudu sanamu yoyote kwani mtu anayestahili kuabudiwa ulimwenguni na peponi ni mwenyezi Mungu peke yake" Mfalme aliposikia hivyo aliisifu sana sheria hiyo takatifu na kuwajengea msikiti huko Guangzhou, msikiti hio ulipewa jina la Huaisheng kwa kuonyesha kumbukumbu yake kwa Mtume Muhammad (Saw). Baadaye mjumbe huyo alifariki na alizikwa katika mji wa Guangzhou, mjumbe wa pili alifanya uenezi wa dini mjini Yangzhou, wa tatu na wa nne walifanya uenezi wa dini mjini Quanzohou na wote hao walipofariki walizikwa huko.

Hadithi ya pili iliyoenea zaidi inasema hivi katika miaka ya Zhenguan (627-649) ya Enzi ya Tang siku moja mfalme aliota ndoto mbaya aliona jini moja likimrukia, wakati huo katika hali ya hatari ghafla alijitokeza mzee mmoja aliyevaa joho la kijani na kilemba cheupe kichwani akishika tasbihi mkononi, na akalifukuza jini hilo na hivyo alimwokoa mfalme huyo, siku ya pili mfalme aliwaita mawaziri wake na maofisa wote wa kijeshi kuwaeleza ndoto hiyo na kutaka tafsiri yake.

Waziri mmoja akamweleza kwa kusema kwamba jini ni dalili ya wakorofi, bila shaka watatokea mahaini wa nchi; yule mgeni aliyevaa kilemba cheupe kichwani ni mtu mwenye hekima aliyetoka nchi ya Tazi. Ndoto ya mfalme ina maana kwamba wakipuuza maadili ya ndoto hiyo nchi haitakuwa na amani wala utulivu.

Kwa hiyo mfalme hiyo akamtuma mjumbe wake kwenda nchi ya Tazi na kumwomba Mtume Muhammad (Saw) alete watu wake kueneza dini nchini China.

Muhammad akakubali ombi hilo akalea wnafunzi wke watatu, Bahati mbaya wawili kati yao walikufa safarini na kuzikwa katika mlango wa bahari wa Xingxing, mjumbe mmoja tu ndiye aliyefika China na akakaa nyumba ya wageni katika mji mkuu Changan.

Mjumbe huyo siku zote alikaa kimya na kufanya ibada , siku moja mfalme alipata wasaa na akajifanya kama ofisa wa kawaida, akaena kumtembelea akamkuta mjumbe akikariri Kurani kwa makini huku akielekea upande wa magharibi. Alipomaliza kusoma aya moja akaufunga msahafu wa Kurani, akaueweka polepole juu ya rafu halafu akatoka mlangoni akiw ana tabasamu usoni akisema "karibu ndani mwadhamu. Niwie radhi kwa kuchelewa kukupokea" Mjumbe akacheka bilaya kujubu hivyo watu hao wawili wakakaa kitakio wakishikamana mikono na kuanza kuzungumza. Mfalme alitaka kupima akili zake akatoa masuala kadha wa kadha, mjumbe akamjibu akamjibu sawasawa bila wasiwasi. Mfalme huyo alifurahi sana akamruhusu kukaa kwa muda mrefu huko mji mkuu Changan kueneza dini ya Kiislamu.

Baada ya miaka mingi mjumbe alifikiri sana nyumbani kwake, akaomba kurudi kwao lakini akakataliwa na Mfalme. Baada ya hapo akatoa tena ombi hilo Mfalme baada ya hapo akatoa tena ombi hilo. Mfalme akajisemea kimoyomoyo akipapasapapasa ndevu zake, "Inanibidi kutafuta njia ya kumbakiza" kwa kushauriwa na Mfalme, mjumbe akamwoa msichana mrembo na hakurudi tena kwao. Alijitolea maisha yote kwa ajili ya uenezaji wa Uislamu katika China.