Make your own free website on Tripod.com

Karume aahidi kufuata nyayo za Alhaj Mwinyi

Majira Juni 14

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Aman Abeid Karume amesema akichaguliwa kuwa rais atafuata nyayo za Rais Mstaafu Alihaji Hasani Mwinyi.

Akihutubia mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi na wanachama wa CCM Zanzibar jana katika viwanja vya Kibanda Maiti mjini hapa, alisema atafuata yote mazuri yaliyofanywa na Rais Mstaafu Mwinyi.

Alisema maneno aliyoambiwa na Bw. Mwinyi wakiwa Dodoma hivi karibuni yalimwingia sana na hivyo kuamua atakapokuwa katka madaraka atayatekeleza bila kusita.

Lipumba,Seif kusafiri kwa ndege tu

Majira Juni 14

CHAMA cha Civic United Front (CUF) kimetangaza kuwa wagombea wake wa viti vya urais, Profesa Ibrahim Lipumba kwa upande wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Maalimu Seif Shariff Hamad anayewania Zanzibar sasa watakuwa wakisafiri kwa ndege kila wanapokuwa safarini na si kwa magari hususani kutoka mkoa mmoja hadi mwingine.

Hatua hiyo imekuja huku mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Bw. Amaan Abeid Karume kurejea Dar es Salaam kwa ndege ya lifti akitokea Dodoma juzi na baadaye jana asubuhi kwenda Zanzibar akitumia usafiri wa boti iendayo kasi.

Tanesco kutumia milioni 100/= kwa ajili ya Ukimwi

Nipashe juni 14

SHIRIKA la Umeme Tanzania TANESCO limetenga kiasi cha sh. Milioni 100 kwa ajili ya elimu ya Ukimwi kwa wafanyakazi wake lengo likia ni kuwawezesha kutambua athari za uogonjwa huo na kuwa katika nafasi ya kujiepusha nao.

Hayo yalisemwa na juzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Bw. Baruan Luhanga alipokuwa akifungua semina ya wiki moja kuhusu Ukimwi kwa wafanyakazi wa TANESCO mkoani Dodoma.

Kwa mujibu wa Bw. Luhanga hatua hiyo inalenga katika kupunguza idadi ya vifo vinavyotokna na ugonjwa huo miongoni mwa watumishi wa TANESCO.

Silaha 75,000 zinamilikiwa na watu wa kawaida - magufuli

BUNGE lilielezwa mjini hapa kwamba jumla ya silaha 75,228 zinamilikiwa na wananchi wa kawaida nchini.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi Bw. John Magufuli alipojibu swali la Bw. Mutamwega Mugahya (NCCR Mageuzi - Mwibara).

Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Mohamed Seif Khatibu.

Bw. Magufuli alisema kulingana na takweimu zinazoishia Desemba 29 mwaka jana silaha zinazomilikiwa na raia wa Kawaida nchini ni bastola 35,378,Shortgun 13,533, rifles 24,287 na air rifles 2,080.

Alisema jumla ya silaha zote ni 75,228

Naibu Waziri alisema mpaka sasa ni mashirika mawili tu ambayo ni Mzinga Corporation Limited lililopo Morogoro na Tanganyika Arms Limited la Moshi ndiyo yaliyopewa leseni ya kuuza silaha nchini.

Bajeti Patupu

Majira Juni 16

SERIKALI imeongeza kodi kwa asilimia 5 katika vinywaji vikali kuanzia Julai Mosi mwaka huu.

Waziri wa Fedha Bw.Daniel Yona alisema ongezeko hilo litakaloipatia serikali sh. 4,644 milioni ni sawa mfumuko wa bei unaotarajiwa mwaka huo.

Waziri huyo pia alisema kodi ya ushuru kwa bidhaa 46 unafutwa na zitakozotozwa ni sita tu ambazo ni mafuta ya petroli, bia, sigara, vinywaji baridi, vinywaji vikali na magari madogo yenye injini zenye uwezo wa zaidi ya cc 2000.

Katika bajeti hiyo misamaha mingine ya kodi imetolewa ambapo sasa michango inayotolewa na wafanyabishara au viwanda kwa ajili ya kusaidia huduma za afya, elimu, maji na barabara itatumika kama matumizi halali wakati wa kukadiria kodi.

Alisema kiasi kinachoruhusiwa ni kisichozidi asilimia mbili ya ziada au faida inayopatikana kwa mwaka.

Hata hivyo Waziri Yona alisema bajeti ya serikali ya mwaka huu ni asilimia 58 ya mahitaji yaliyoombwa na wizara, idara, mikoa na wilaya.

'Mchezo mbaya' wakithiri Kilimanjaro

Mwananchi Juni 15

TABIA ya baadhi ya wanafunzi wa shule za Sekondari mkoani Kilimanjaro kuchangia kondomu moja hadi zaidi ya watu 10 a wasichana na wavulana kuingiliwa kinyume na maumbile inaongezeka siku hadi siku, imeelezwa.

Katibu Mtendaji wa Kituo cha Maadili Kanda ya Kaskazini Senya Florentirie ameyasema hayo alipotoa majumuisho ya warsha zilizoendeshwa katika kituo hicho kwa mwaka 1999/2000 katika shule 12 za sekondari katika mkoawa Kilimanjaro.

Alisema kuwa hali hiyo inatokana na baadhi ya wanafunzi wa kiume kutumia dawa za kulevya zinazowafanya wadhani kuwa kuingiliwa kinyume na maumbile ndiyo starehe kubwa kuliko zote.

Florentirie alisema kuwa pamoja na sababu nyingine, viongozi wa dini yao huwaruhusu wasichana kutumia njia ya kupanga uzazi ya nyota ya kijani na kwamba huelezwa kuwa kuingiliwa kinyume na maumbile ni kujikinga na mimba.

Alisema pia kuwa katika mila na desturi za baadhi ya makabila katika mabara ya Afisa na Afrika wasichana wanaoolewa hutakiwa wawe mabikira na kwa sababu hiyo wengine huamua kufanya mapenzi kunyume na maumbile ili kutunza ubikira wao.

Karume na mimi sawa- Mrema

MWENYEKITI wa Tanzania Labour Party (TLP) Augustine Mrema amejifananisha na Mgombea Urais Zanzibar kwa tikiti ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Amani Abeid Karume.

Akihutubia umati wa watu katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Jangwani baada ya kuchukua fomu jana, Mrema alisema anafanana na Karume kwa hali zote na kusema ataibuka mshindi kwenye uchaguzi Mkuu huo.

Mrema alisema yeye na karume hawana shahada, kigezo walichotumia kumzuia (Mrema) asigombee urais lakini akasema wote wanao uwezo mkubwa wa kuongozana na kueleza kwa kina alivyofanya kazi serikalini kama waziri.

"Mimi sawa na Karume, wote hatuna digrii, CCM walishindwakuwapitisha wasomi waliotaka kugombea Zanzibar wakamchukua Karume kwa sababu anauzika kwa wananchi... Bilali ni daktari wa nyuklia lakini hauziki" alisema Mrema.