Magazeti Wiki Hii

U - CCM ulimponza askari aliyepigwa - Hamad

Majira Aprili 18

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema Inspekta Asha Mohamedi ana ukereketwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) na ndio uliomponza akapata kipigo kutoka kwa wafuasi wa chama hicho.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jana Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharrif Hamad hata hivyo alisema chama chake kimesikitishwa kwa kipigo alichopata Inspekta Asha hadi kulazwa hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar na kinampa pole.

Alisema CUF daima hulaani vitendo vyote vya ukiukaji haki za binadamu na unyanyasaji vinavyofanywa na vyombo vya dola bila kujali vimefanywa na nani.

Alidai Inspekta Asha alivamia mkutano wa ndani wa CUF uliohutubiwa na yeye Maalim Seif uliofanyika katika uwanja wa ofisi za CUF za jimbo la Magomeni akiwa hajavaa sare za polisi pamoja na askari wengine watatu wakiwa na silaha.

Alisema Inspekta Asha alianza kuchana maturubai waliyokuwa wamejizungushia kama ukuta kuonyesha kuwa ni mkutani wa ndani ambao polisi hawakupaswa kuapo na wafuasi wa CUF waliokuwepo wakanza kumshungulikia.

"Vyama vingine vinafanya mikutano yao ya ndani nje na kuzungushia kamba tu na havivamiwi kuwa ni mkutano wa hadhara iwe sisi tuliozungushia maturubai. Mimi mwenyewe ilibidi niiname sana kupitia kwenye mlango uliowekwa" alisema.

Dereva asakwa kwa kumlawiti abiria wake

Majira Aprili 18

POLISI Mkoani Morogoro wanamsaka dereva wa teksi mmoja (jina linahifadhiwa) kwa tuhumu za kumlawiti abiria aliyekuwa amempakia kwenye teksi yake baada ya kudai hana fedha za kulipia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Bw. Christopher Shekiondo alisema jana tukio hili lilitokea Aprili 13 mwaka huu saa 6 usiku baada ya kijana mmoja (jina limehifadhiwa) kuteremka kwenye basi maeneo ya Msamvu na kuomba msaada wa kufika mjini ili apate mahala pa kulala.

Kamanda Shekiondo alisema dereva teksi huyo alimpakia kijana hiyo mwenye umri wa miaka 16 na kumfikisha mjini na kumtaka atoe fedha za kuikodisha.

Bw. Shekiondo alisema kijana huyo baada ya kudai hana fedha ndipo dereva huyo alimwambia amlawiti ikiwa kama ni fidia.

Alisema kijana huyo alipojaribu kumzuia mtuhumiwa alimtishia kwa kisu na baada ya kumaliza uhalifu wake aliondoka.

Kijana huyo aliamua kwenda polisi kuripoti na dereva huyo.

Kamanda Shekiondo amewaonya wananchi kuacha kutembea usiku na pia wanapopata usafiri wawe makini na watu wanaowapatia usafiri.

Msekwa atupa hoja ya kutaka Sumaye ajiuzuli

Mtanzania Aprili 17

SPIKA wa Bunge, Pius Msekwa amemzuia Mbunge wa Siha, Makidara Mos (NCCR -Mageuzi) kuwasilisha hoja yake Bungeni kwamba ingeweza kusababisha malumbano ya kisiasa.

habari zilizopatikana Bungeni Dodoma zilisema Makidara alikuwa awasilishe hoja yake hiyo Aprili 7 mwaka huu, lakini Spika alimwandikia barua Aprili 6 kuikataa hoja hiyo.

Kwa mujibu wa habari hizo hoja yenyewe ilikuwa inasema "Yahusu ufafanuzi wa serikali zinazoashiria matumizi mabaya ya madaraka ya kisiasa na ukiukwaji wa haki za binadamu na Katiba ya Nchi.

Maaskofu kuunda kundi la kuangalia uchaguzi Mkuu

Mchana Aprili 18

BARAZA la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limesema litaunda kikundi chake cha watazamaji wa Uchaguzi Mkuu utakao fanyika baadaye mwaka huu.

Pamoja na kikundi hicho tayari Kanisa Katoliki pia limeshaandika vitabu na kuandaa kaseti za video na vipindi vya redio, vyote vikiwa na lengo la kutoa elimu ya uchaguzi kwa wananchi.

Mmoja wa mapadri waliozungumza kwa masharti ya kutotajwa jina ameiambia MCHANA kwamba kitabu hicho kinaitwa ' kwa nini kujali uchanguzi'

Ilielezwa kwamba vitabu, kanda za video na vipindi vya redio vimeandaliwa kwa pamoja kati ya TEC, chama cha Wanataaluma wa Kikristo Tanzania (CPT) na Tume na Amani ya Maaskafu.

Kwa Mujibu wa padre huyo vyote vimeshasambazwa katika majimbo yote nchini. Habari zilizotolewa na Makamu wa Rais wa TEC Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na kutangazwa na kituo cha Televisheni zilise,a kwamba mpango huo una lengo la kiona jinsi gani uchaguzi utakayoendeshwa.

Baadaye Padri Kaombe ambaye ni msemaj wa Mwadhama Polycarp aliiambia MCHANA kuwamba mpango huo wa TEC umelenga kuzhakikisha uchaguzi unakuwa huru nawa haki

Amuua mkewe, mtoto na baadaye kujinyonga

Mtanzania Aprili17

WATU watatu wa familia moja wa Kijiji cha Mmbezumanamole wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya walifariki dunia mwishoni mwa wiki katika matukio mawili tofauti.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya Laurian Sanya aliwataja watu hao kuwa ni Chuma Kilwamba , mkewe aitwaye Namwalizi Sunyinga na mtoto wao wa kiume mwenye umri wa miaka minne.

Sanya alisema Kilambwa alimuua mkewe pamoja na mtoto wao, Adamu baada ya kutokea mzozo kati ya wazazi hao wawili. Hata hivyo, chanzo cha ugomvi huo bado hakijafahamika.

Kamanda huyo aliendelea kueleza kuwa baada ya Kilwamba kumuua mkewe na mtoto wao alijiua mwenyewe kwa kutumia kamba ya katani