Waasi wa Kiislamu wamteka mtoto wa Meya

MANILA, Ufilipino

TELEVISHENI moja ya Ufilipino, imesema kuwa polisi katika Jimbo la Kusini mwa nchi hiyo, Sulu wamesema wanazifanyia kazi taarifa za kuchukuliwa mateka mtoto wa Meya wa mji wa Talipao, Tambrin Tulawi na waasi wa Kiislamu

Gavana wa Jimbo la Sulu, Abdusakur Tan amekaririwa na Televisheni hiyo ya Ufilipino akisema kuwa mtoto wa Tulawi, Abdu Assi Tulawi, aliyekuwa anaishi na baba yake, alitoweka Alhamisi asubuhi na inadhaniwa kuwa huenda alichukuliwa na waasi hao wa Kiislamu wanaopigania taifa la Ufilipino lenye Wakristo wengi ili liwe la Kiislamu.

Waasi wa Abu Sayyaf wanawashikilia mateka wapatao ishirini wakiwamo raia wa kigeni akiwamo Mmarekani Jeffrey Schilling ambaye amtishiwa kuuawa.

Wengine miongoni mwa mateka hao ni Wafilipino.

Kwa mujibu wa Taarifa ya televisheni hiyo, Waziri wa wa Ulinzi, Bw. Orlando Mercado, tayari amepewa taarifa za kutoweka kwa kijana huyo na amelitaka jeshi kutafuta ukweli wa tetesi za kutoweka kwake.

Umoja wa Mataifa wakaribisha taarifa ya Kongo

NEWYORK, Marekani

BARAZA la Usalama la Umoja wa Mataifa limeikaribisha taarifa ya taifa lililokumbwa na vita la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kwamba sasa kwamba askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wataruhusiwa kuwepo nchini humo ingawa Baraza hilo llilitaka maelezo zaidi.

Kiongozi wa zamani wa Nigeria Jenerali Abusalaam Abubakari, ambaye pia ni mjumbe wa Umoja wa Mataifa, amerudi katika kutaka kukutana na Rais Laurent Kabila ili kutaka ushirikiano wake katika kushughulikia misuada ya mgogoro wa Kongo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na Baraza hilo katika kikao cha faragha, Jenerali Abubakari, amesema kwamba Rais Kabila amekubali uwekaji wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa katika miji ya Bandaka, Kananga na Kinshasa.

Na pia kulegeza baadhi ya vikwazo juu ya nyendo za vikosi vya Umoja wa Mataifa. Hadi hivi karibuni, Kabila alikuwa akipinga uwekaji wa vikosi hivyo katika miji mikubwa inayodhibitiwa na vikosi vyake.

Kwa mujibu wa Jenerali abubakari, Kabila alikasirishwa kwa madai kwamba miezi kumi na moja wakati nchi yake inavamiwa, hakuna mtu yeyote yule aliyethubutu kunyosha kidole cha kukemea na kuja kuiokoa nchi hiyo tofauti na kile kilichotokea huko Kongo, Timur ya Mashariki na kwingineko.

Sababu ya ajali ya ndege ya Concord yaelezwa

PARIS, Ufaransa

SHIRIKA linaloshugulikia ajali za anga la Ufaransa katika ripoti yake ya mwanzo ya ajali ya ndege ya CONCORD ya Air France majuma sita yaliyopita, inahitimisha kwamba pancha katika gurudumu iliyosababishwa na chuma kilichotupwa katika uwanja wa ndege, ilicharusha mkasa ule wa kutisha.

Ripoti hiyo yenye kurasa 80 ikiambatana na taarifa ya radio, inafichua kwamba mnara wa kuongozea ndege katika uwanja wa ndege uliwaambia waendeshaji wake kwamba ndimi za moto zilikuwa zinatapikwa kutoka bawa la kushoto.

Marubaniwaliizima injini namba mbili halafu waliamua kujaribu kutua katika uwanja wa karibu wa jeshi. Baada ya sekunde kadhaa, ndege ile ya safari nambari 4590 ilianguka na kuua watu waliokuwamo 113.

Madege yote 12 yaliyosalia ya aina hiyo ya concord, yanayomilikiwa na Air France na yale ya British Airways, tangu wakati ule yalisimamisha safari zake.

Wataalamu watakutana tena septemba 7, kwa madiliano zaidi