CDS yaongoza Burkina Faso

OUAGADOUGOU,Burkina Faso

CHAMA kinachotawala Burkina Faso cha Congress Democrat and Social (CDS), kimeonyesha kuongoza kwenye matokeo yasiyorasmi ya uchaguzi wa Serikali nchini humo.

Chama hicho kinaonyesha kushinda majimbo 42 kati ya majimbo 49 nchini Burkina Faso.

Imeelezwa kuwa kikundi kimoja cha upinzani kinachoongoza vyama vya upinzani nchini humo kilikataa kushiriki katika uchaguzi huo kikidai kuwa uchaguzi ulitawaliwa na wizi wa kura.

Mahakama yamkosa kwa mara nyingine Rais wa Suharto

JAKATRA,Indonesia

RAIS wa zamani wa Indoneshia ,Bw.Suharto kwa mara nyingine tena alishindwa kufika kwenye Mahakama Kuu ya nchi hiyo kusikiliza kesi inayomkabili ambapo anadaiwa kuhusika na tuhuma za kuhusika katika ubadhirifu wa mamilioni ya dola za Kimarekani.

Hata hivyo Jaji anayesikiliza kesi hiyo juzi baada ya Rais huyo wa zamani kushindwa kufika mahakamani hapo kwa mara ya pili,ameshindwa kutoa uamzi ambapo alisema nasubiri jopo la madaktari walioteuliwa kuchunguza afya ya kiongozi huyo.

Rais huyo wa zamani anatuhumiwa kuhusika na ubadhirifu wa dola za Kimarekani zaidi ya milioni 500 zilizopotea wakati wa utawala wake wa miaka 32.

Hata hivyo imebainika kuwa Mahakama ilikuja kufuta kesi hiyo baada ya jopo la madaktari waliokuwa wakichunguza afya ya Rais huyo wa zamani, kutoa taarifa kuwa hawezi kusikiliza mwenendo wa kesi katika maisha yake yote.

Wakati huo huo,Mtoto wa Bw.Suharto, amehukumiwa kwenda jera miaka 18 baada ya kupatika na hatia ya rushwa.

Baada ya Mahakama kutoa hukumu hiyo,hali ya ukosefu wa amani ilitawala nje ya ofisi ya kikundi cha kutetea haki za binadamu mjini hapa ilitanda baada ya kulipuliwa kwa bomu.

Hata hivyo hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo.

Kukosekana kwa ushahidi kwamnusru Netanyahu

TELAVIV,Israel

MAHAKAMA nchini Israel imemfutia kesi Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo,Bw.Benyamin Netanyahu baada ya Wakili wa Mwanasheria aliyekuwa kimtetea, Elyakim Rubinstein kusema kuwa hakuna ushahidi.

Kufuatia hatua hiyo,Bw.Rubinstein ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo ameamua kufunga faili la Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Israel ambaye alikuwa akishtakiwa kupokea zawadi na huduma za bure wakati wa utawala wake.

"Nimeamua kufunga faili la Bw.Netanyahu kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kumtia hatiani"alisema Mwanasheria huyo Mkuu.

Bw.Nitanyahu na mkewe wadaiwa kupokea zawadi na huduma mbalimbali wakati wa utawala wake katika kipindi cha mwaka 1996-1999 kabla ya Waziri Mkuu wa sasa Ehud Barak kushika nafasi hiyo.

Mapigano yazuka maeneo matakatifu

JERUSALEM,Israel

ZIARA ya kiongozi wa Upinzani wa Israel mwenye msimamo mkali,Ariel Sharon imezuna mapigano makali kati ya Wapalestina na pilisi wa Israel ambao walikuwa wakipinga ziara hiyo.

Mapigano hayo yalifanyika katika maeneo matakatifu ,kuzunguka msikiti wa Al-Aqsa mjini hapa.

Katika kutuliza ghasia hizo,polisi walifyatua risasi za mipira na kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya Wapelestina.

Inasemekana kuwa katika ghasia hizo polisi 25 na Wapalestina watatu walijeruhiwa.

Hata hivyo Sharon na wenzake wa chama cha Likud,alitembelea eneo hilo chini ya ulinzi mkali.