175,000 wakimbia makazi yao Lubumbashi

Umoja wa Mataifa

WAKATI taarifa za hivi karibuni zilisema watu wapatao 145,000 wamehama makazi yao katika wilaya za Katangan, eneo ambalo linategemewa sana kwa kilimo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imebainika kuwa watu wengine wapatao 30,000 wameyakimbia makazi yao mjini Lubumbashi.

Kwa mujibu wa habari zilizosambazwa kwa mawasiliano ya kompyuta kutoka Umoja wa Mataifa, wengi wa watu hao waliotoroka makazi ni wakulima kutoka Katanga Kaskazini.

Watu 22,800 wamearifiwa kuishi na familia za wenyeji wakati waliosalia wanaishi katika makambi yapatayo saba.

"Wakimbizi" kadhaa katika makambi mawili wanajishughulisha na mpango wa kilimo kwa ajili ya kujipatia chakula katika mpango wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)na Shirika la chakula duniani (FAO). Baadhi, kwa mujibu wa habari hizo wamekuwa wakipatiwa msaada wa chakula na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na ICRC.

Hata hivyo watu wapatao 2,300, wengi wakiwa wa familia za wanajeshi

hawajapatiwa msaada wa kutosha na wanakabiliwa kwa kiwango kikubwa na utapiamlo.

Wakati huo huo, kikundi cha kutetea haki za binadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ASADHO nacho kimelalamikia vikali uvunjaji wa haki za binadamu kutokana na mashambulizi ya kijeshi ambayo yamekuwa yakielekezwa kwa raia mashariki ya nchi hiyo.

Taarifa ya ASADHO imesema mashambulizi hayo yamekuwa yakifanywa katika kile kinachoitwa kudhibiti wanamgambo wa Mayi-Mayi ambao walivamia na kushambulia raia katika kambi za Mulume Munene. Vijiji vilivyoathirika zaidi na hatua hiyo ni Izege,

Karibu na Walungu. ASADHO imewanukuu wanakijiji wakisema kuwa askari hao waliwaamuru watoke nje ya nyumba zao na watano kati yao waliokataa waliuawa.

Uvamizi wa Karamajong wasababisha 135,000 kupoteza makao Uganda

Kampala, Uganda

Huku ukame ukiendelea kukumba wilaya ya Karamoja, kaskazini-mashariki mwa

Uganda, mashambulizi makali na uporaji unaofanywa na Wakaramajong katika

wilaya jirani za Katakwi, Lira, Kitgum, Soroti na Kumi yamesababisha

upotevu mkubwa wa makao, taarifa ya OCHA ilisema.

Wakaramajong, ambao kwa kawaida huvamia wilaya jirani nyakati za ukame, mwaka huu wanaripotiwa kuchanganya uporaji wao na ubakaji, mauaji na vipigo vikali ambavyo havijawahi kutokea hapo awali. Jambo hili huenda limechokonolewa na ahadi za mara kwa mara za serikali za kuwanyang’anya silaha Wakaramojong hao,

OCHA ilisema.

Wakati huo huo, ukosefu wa usalama unaoendelea kutokana na kuwepo kwa waasi na shughuli za Lord’s Resistance Army za hapa na pale ina maana kuwa juhudi za kutoa misaada kwa watu waliopoteza makao na wanaoweza kuathiriwa umesababisha

kusimamishwa kwa juhudi hizo huko wilaya za kaskazini za Gulu na Kitgum,

kwa mujibu wa taarifa ya OCHA.

Licha ya kuwepo kwa mashirika ya kibinadamu katika wilaya hizo operesheni nyingi zimebaki tu mijini kwa sababu yanakosa ryksa ya kiusalama ya kuingia vijijini mara nyingi. Waasi wa LRA wamekataa sheria ya msamaha wa serikali na wanaendelea kufanya mashambulizi katika eneo hilo. Jeshi la Uganda mnamo siku ya Jumanne

lilimua Luteni-Kanali Onen Kamdulu, naibu jemadari wa kikundi cha Opiro cha LRA ambacho kilikuwepo wilayani Gulu, wakati wa vita kali katika

Vilima vya Kilak huko wilayani Adjumani, gazeti lisilo rasmi kabisa la

‘New Vision’ liliripoti.

PEMBE YA AFRIKA: Hakuna njaa, mjumbe wa UN asema

Mjumbe maalumu wa Katibu-Mkuu kwa Pembe ya Afrika, Catherine Bertini, alikanusha kuwa tatizo la ukosefu wa chakula katika eneo hilo limefikia

Kiwango cha kuwa baa la njaa, lakini akahimiza jamii ya kimataifa kutoa

kwa ukarimu ili kuepuka baa la njaa.

"Hili ni tatizo kubwa linalowakumba watu wa eneo hilo, na kazi yetu, kama ilivyoelekezwa na Katibu Mkuu, ni kuleta nyenzo za kutosha ili kuhamasisha, kupanga mifumo inayotosha ili tuweze kuepuka baa na kuepuka njaa," aliambia mkutano wa waandishi wa habari huko Nairobi hivi karibuni.

Nchini Ethiopia, Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu imesema imesafirisha kwa ndege misaada ya chakula cha tani za kimetriki 150 hadi eneo la Gode la Ethiopia tangu Aprili 12,mwaka huu. Kiasi cha tani 15-17 zinafika Gode kila siku kwa ndege aina ya Hercules C-130, kwa mujibu wa taarifa ya ICRC kutoka Addis Ababa.

Wazee wa kijiji wanagawa chakula hicho, wakisimamiwa na watumishi wa ICRC

na Chama cha Msalaba Mwekundu cha Ethiopia.

AFP liliripoti kuwa wahisani wamekuwa wachoyo kutoa fedha za kutosha

kusaidia juhudi za Shirika la Kimataifa la Mpango wa Chakula (WFP)

kusaidia wanaokabiliwa na njaa, lakini kuwa ufadhili uliongezeka kufuatia

ziara ya Mkurugenzi wa WFP Catherine Bertini huko Pembe ya Afrika.

Maafa ya njaa bado yapo Somalia

Umoja wa Mataifa, Washington

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO, limeonya kuwa ugavi

wa chakula huko kusini mwa Somalia unazorota kwa kasi, likieleza hali hiyo

kuwa ya "wasiwasi mkubwa."

Licha ya mavuno mazuri mwezi wa Februari, kiasi cha watu 650,000 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula huku maeneo ya Bakool, Gedo, Bay na Hiran yakiathiwa zaidi, taarifa ya FAO iliyotolewa juma hili ilisema. Mkrugenzi wa WFP kwa Nchi ya Somalia, Kevin Farrell, aliiambia IRIN kuwa maeneo ya kaskazini na kaskazini-magharibi mwa Bakool na Gedo yanaleta wasiwasi mkubwa. "Wasiwasi unaendelea kuongezeka kuhusu hali katika eneo hilo," alisema.

Aliongezea kuwa kama mvua zinazotarajiwa zisiponyesha au zikinyesha chini ya wastani, sehemu iliyoathiriwa inatarajiwa kuongezeka kwa kasi, na uzito wa tatizo kuongezeka.

Wakati huo huo, juhudi za Rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh za kuyaleta makundi ya Somalia pamoja kwa mazungumzo ya amani hazijafua dafu.

Mazungumzo hayo ya amani, ambayo yalikuwa yameungwa mkono na mashirika ya kanda ya IGAD na OAU, yalikuwa na lengo la kuweka serikali ya mpito.

Kikundi kimoja cha Wasomi 60 wa Kisomali, wakiungwa mkono kimya kimya na jamii ya kimataifa, walipendekeza kuwa tarehe ya kuanza kwa mkutano huo - uliokuwa umepangwa kuanza huko Djibouti Alhamisi iliyopita inapaswa kuahirishwa kwa

Mashauriano zaidi na matayarisho ya ajenda, mashirika ya habari yaliripoti.