Wasio Waislamu kutungiwa sheria tofauti Nigeria

Tehera, Iran

WAKATI Jimbo la Kanu Nchini Nigeria limetangza kutumia sheria za Kiislamu kuanzia Juni 21, mwaka huu watu wasio Waislamu jimboni humo wamekumbwa na hofu kuwa juu ya hatma ya Usalama wao na Uhuru wa kuabudu Redio Teheran Iran imesema.

Hata hivyo hatua hiyo ambayo iliungwa mkono kwa maandamano ya Waislamu patao 2500 mwishoni mwa wiki imeelezwa na Serikali ya Jimbo la Kanu kuwa haitawanyima haki wasio Waislamu.

Msemaji mmoja wa Serikali ya Kanu Bw. Salum Mohamed alikaririwa akisema Alhamisi iliyopita kuwa matumizi ya sheria ya kiislamu yatasaidia kupunguza kiwango cha uovu na uhalifu hususani vitendo vya uzinzi, uasherati na wizi. Bw. Mohamed alikuwa akiongea na Shirika la Habari la Uingereza BBC.

Alisema kuvunjika kwa maadili na uigaji wa utamaduni mchafu wa kimagharibi vitakoma kutokana na ukali wa sheria ya kiislamu.

Hata hivyo majimbo ya Kaskazini mwa Nigeria ambako kulizunguka machafuko na kusababisha vifo vya mamia ya watu wakati sheria iliyotangazwa kutumika zitawekwa sheria nyingine za kawaida kwa ajili ya wasio Waislamu.

Kanu linakuwa jimbo la Sita nchini Nigeria kutangaza matumizi ya sheria ya Kiislamu tangu vuguvugu hilo lilipoanza Februari na Machi mwaka huu.

Mugabe atishia kuwatia mbaroni wasimamizi wa Uchaguzi

Harare, Zimbabwe

SERIKALI ya Chama cha ZANU- PF kinachotawala nchini Zimbambwe imesema itawatia mbarano na kuwachukulia hatua za kisheria waangalizi wote wa kimataifa wa uchaguzi watakaokaidi amri ya Rais Robert Mugabe ya kujihusisha na Uchaguzi wa Rais na Wabunge unaofanyika nchini humo.

Waangalizi wa kimataifa wapatao arobaini wanaoshirikiana na taasisi zisizo za kiserikali nchini humo wamepigwa marufuku kujihusisha na uangalizi wa zoezi la upigaji kura. Waangalizi kutoka nchi za Kenya na Nigeria nao wamepigwa marufuku kutokana na uhusiano wao na Serikali ya Uingereza.

Zimbambwe imekuwa katika hali ya kutoelewana na Uingereza kwa miezi kadhaa sasa kutokana na hatua ya Rais Mugabe kutowazuia mashujaa wa kale wa vita nchini humo kupora mashamba ya wazungu.

Rais Mugabe amewaonya wananchi wa Zimbabwe kutodanganywa na alichokiita vyombo vya habari vinavyopotesha ukweli na akamshutumu Kiongozi wa upinzani wa chama cha MDC Bw. Morgan Tsangirai, kuwa ni miongoni mwa waliodanganywa.

Viti vya Bunge vipatavyo 120 vinagombewa nchini humo.

Naye mpinazani mkuu wa Rais Mugabe Bw. Morgan Tsangarai alikaririwa akisema mwishoni mwa wiki kuwa ana uhakika wa kushinda katika kiti cha Rais kwa vile anaungwa mkono na Wazimbabwe wengi.

Zimbabwe imeingia katika Uchaguzi Mkuu huu Uchumi wake ukiwa unakadiriwa kuporomoka kwa kiasi cha asilimia 5 mwaka huu na kukiwa na uhaba wa chakula kutokana na pilikapilika za uvamizi wa raia weusi katika mashamba ya Wazungu , kiwango cha ukosefu wa ajira nchini humo ni asilimia 50.

Wauawa katika Uchaguzi wa Sekta ya Chai Kenya

Nairobi, Kenya

WATU watatu walipoteza maisha yao baada ya polisi nchini Kenya kuwafyatulia risasi katika vurugu zilizozuka wakati wa uchaguzi wa Viongozi wa Sekta ya chai wilayi Thika.

Kufuatia tukio hilo Mbunge mmoja wa Upinzani Bw. Patrick Mururi alikamatwa Alhamisi iliyopita kwa tuhuma kwamba alihusika na uchochezi wa ghasia hizo.

Pamoja na Mururi Viongozi wengine kadhaa wa chama cha wakulima wa chai wilayani humo walitiwa mbaroni.

Hata hivyo Rais Daniel Moi alikaririwa na vyombo vya habari akisema mwishoni mwa wiki kuwa polisi walifanya makosa kuwaua raia kwa risasi na amekemea vikali na kuonya juu ya hatua hiyo ya polisi.

Iran, Misri zafufua Uhusiano

Tehran, Iran

RAIS Hosni Mubarak wa Misri wiki hii alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais Mohamed Khatani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa nia ya kurejesha uhusiano wao ulioporomoka katika miaka ya tisini.

Mahusiano ya Iran na Misri yalivurugika kutokana na Misri kushiriana na Israel ambayo ilikuwa na maelewano mabaya na Misri na pia madai ya Misri kuwa Iran ilikuwa ikivifadhili vikundi vya magaidi wa Kiislamu katika mashambulizi dhidi ya nchi hiyo.

Mazungumzo hayo yameelezwa na wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuwa ni hatua muhimu katika kufufua mahusiano hayo mapya.