Papa kutoa sadaka za madhabahuni Msumbiji

lUjumbe wake wa Pasaka mwaka huu ni katika lugha 40

Vatican City

SADAKA zilizopatikana katika Ibada ya Alhamisi Kuu ya mwaka huu iliyoendesha na Papa Yohane Paulo wa Pili mjini Vatican zitapelekwa nchini Msumbiji kwa ajili wa kuwasaidia wahanga wa mafuriko ya hivi karibuni ambao wameathirika vibaya.

Taarifa iliyotolewa na Askofu Piero Marini,wakati wa kutangaza ratiba ya wiki ya Papa hivi karibuni imesema kiwango cha sadaka kilikachokusanywa kingewasilishwa kwa Papa wakati wa matoleo hayo.

Juma Takatifu la Papa mwaka huu lina mabadiliko mawili kulingana na miaka iliyopita.

Ibada ya Alhamisi Kuu haitahusisha Meza ya Bwana kama ilivyo kawaida katika St. John Lateran, ila Vatican, ili kutoa nfasi kubwa zaidi kwa mahujaji.

Pia maneno (text) ambayo hutolewa na Papa wakati wa Ijumaa Kuu safari hii ameayaandika mwenyewe kulingana na ujumbe wake utokanao na ziara yake ya Mashariki ya Kati.

Katika Jumapili asubuhi Papa Yohane Paulo wa Pili atasherehekea Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na kutoa ujumbe wake kwa lugha 40.

Mandela kwenda Burundi mwisho wa mwezi

IRIN,

Msuluhishi katika mazungumzo ya amani ya Burundi, Nelson Mandela, atazuru

Bujumbura mnamo 28 Aprili, afisa wa Mfuko wa Mandela huko Afrika Kusini

aliiambia IRIN siku ya Jumatano. Afisa huyo alisema hakuwa na maelezo

zaidi kuhusu ziara hiyo. Shirika la habari la Burundi liliripoti siku ya Jumatatu kuwa madhumuni makuu ya Mandela ni kufanya mazungumzo na viongozi

wa jeshi la Burundi.

Lilinukuu taarifa za upinzani zikisema kuwa Mandela

atakutana pia na vikundi vilivyoko Burundi na mashirika ambayo yanapinga

harakati ya sasa ya amani ya Arusha.

Wakati huo huo habari zimesema, kiasi cha watu 18,198 ambao ni asilimia tano ya jumla ya raia wa Burundi 352,168 waliolazimishwa katika kambi za serikali za mkusanyo tangu miezi ya mwisho ya mwaka uliopita, wamerejea majumbani ilipofikia 7 Aprili,kikundi cha mashirika cha kutathmini kiligundua hayo. Kikundi hicho

kiligundua kuwa watu waliopoteza makao nchini (IDPs) 16,912 walichagua

kutorejea majumbani mwao, taarifa za kibinadamu zilisema.

Serikali imedai kuwa imevunja vituo 23 lakini kazi ya tathmini iliyofanywa hivi majuzi iligundua kuwa ni vituo tisa tu vilivyokuwa makambi ya mkusanyo -

"vilivyosalia vikiwa ni kambi za waliopoteza makao ndani," ziliongezea.

Wakazi wa vituo 14 vya waliopoteza makao nchini walikataa kurejea

majumbani mwao.

Naye Rais Pierre Buyoya na Berhanu Dinka, Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu wa

Umoja wa Mataifa kwa Eneo la Maziwa Makuu, walikutana hivi karibuni

huko Bujumbura kujadili vipengele vya mgogoro wa DRC kwa eneo, harakati ya

amani ya Arusha kwa Burundi na mkutano wa kimataifa uliopendekezwa kuhusu

eneo la Maziwa Makuu miongoni mwa masuala mengine, taarifa ya Umoja wa

Mataifa kwa vyombo vya habari ilisema. Dinka ataendelea na mashauriano

yake kuhusu mkutano huo na viongozi wa nchi nyingine eneoni, ikihusisha

Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kuanzia juma lijalo.

Amekwishazuru Uganda, Tanzania, Burundi na OAU huko Addis Ababa katika

wadhifa wake wa sasa. "Eneo litatoa mawazo muhimu na mchango kwa ufafanuzi

zaidi wa mfumo wa kimawazo kwa mkutano uliopendekezwa=85 Harakati yenyewe,

tangu kubuniwa kwake, lazima imilikiwe na eneo lenyewe na haipaswi

kulazimishwa kutoka nje," Dinka alisema.

Afrika Kusini yaanzisha ushirikiano wa kijeshi na Nigeria

JOHANNESBURG, (IRIN)

USHIRIKIANO wa kiufundi katika masuala ya Kijeshi kati ya majeshi ya Afrika Kusini na Nigeria umeanzishwa kama njia mojawapo ya kuimarisha nguvu za kijeshi barani Afrika.

Afisa Usalama Mkuu wa Majeshi ya Afrika Kusini Luteni Jenerali Johanes Matau, aliwasili nchini Nigeria Jumapili iliyopita katika ziara ya siku tano ya Kiserikali kama hatua za awali za kuasisiwa kwa mshikamano wa Kijeshi miongoni mwa mataifa hayo yenye nguvu katika eneo la Kusini mwa jangwa la Sahara.

Gani Yaroms, Mtafiti katika Chuo cha Taifa cha Kijeshi cha Nigeria aliliambia Shirika la habari la IRIN kuwa ziara hiyo inahusisha kutazamwa kwa kubadilishana mawazo juu uwezekano wa vipi kila moja kati ya nchi hizo zinaweza kupeana misaada ya kijeshi.

Tangu Serikali ya Kidemokrasia iliyochanguliwa na wananchi baada ya miaka mingi ya utawala wa kijeshi Mei, mwaka jana serikali ya Nigeria imejitahidi kuboresha huduma ndani ya jeshi lake, kuwastaafisha zaidi ya maafisa 100 na kuwaleta wataalamu wa nje, hususan kutoka Marekani ili kulipatia upya mafunzo jeshi lake.

Nigeria ni taifa moja la Afrika lenye ushaiwishi mkubwa wa kisiasa na mwakla jana Rais wake Oluseguni Obasanjo alipotembelea Afrika Kusini alisema mnchi yake na Afrika ya Kusini zina wajibu mkubwa katika kurejesha na kutunza amnai barani.