Marekani yashutumiwa kwa kuwasaidia wanaotoa mimba

Washingtonduniani wiki hii, hatua hiyo ya kulisaidia shirika la umoja huo la kudhibiti idadi ya watu imekuja huku Bunge na Congress la Marekani likiwa limetoa msimamo kwamba serikali hiyo haitatoa msaada kwa taasisi za kiserikali wala zisizo za kiserikali ambazo zinahamasisha utoaji mimba au zinafanya shughuli za utoaji mimba.

Wakati Marekani ikifanya hivyo, nchi jirani yake ya Canada imearifiwa kuwa na ongezeko la vitendo vya utoaji mimba kutoka 111,659 mwaka 1996 hadi 114,848 mwaka 1997, ongezeko ambalo linaonyesha kuwa kuna ongezeko la asilimia 2.9 kila mwaka.

Kadhalika takwimu mbali mbali nchini humo zinaonyesha kuwa utoaji mimba umekuwa jambo la kawaida hasa kwa wanawake wa wastani wa umri wa miaka ishirini.

Hali hiyo, wachunguzi wa mambo wanasema imesababisha kuanguka kwa kiwango cha vizazi nchini Canada kwa kiwango ambacho kinaendelea kushusha idadi ya watu nchini humo.

Zambia nayo yalemewa na Wakimbizi wa Kongo

JOHANNESBURG, (IRIN)

Wakimbizi zaidi ya 2000 kutoka Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo wanaokimbia mapigano wameingia nchini Zambia katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Taarifa hiyo iliyotolewa wiki hii imemkariri afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Wakimbizi(UNHCR).

"Kuna idadi kubwa ya wakimbizi wanaoingia humu kupitia mpakani eneo la Kaskazini ya Zambia," Kelvin Shimo wa UNHCR alisema mjini Lusaka.

Alisema kuwa wastani wakimbizi hamsini wanaoingia nchini kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kila siku kupitia Kaputa na Sumbu.

Shimo alisema kuanzia mwanzoni mwa Aprili hadi Jumatatu ya wiki iliyopita pekee kumekuwa na wakimbizi 737 waliokwishaingia nchini Zambia wakitokea Jamhuri ya Kongo.

Wakimbizi hao ambao wamekwekwa katika makambi ya muda kwenye maeneo ya Kaputa na Sumbu, wanatarajiwa kuhamishiwa katika kambi ya Mwange huko Mporokoso, ambako wakimbizi wengine 1 9,500 wengi wao kutoka Jamhuri ya kongo wamehifadhiwa.

Taarifa ya UNHCR imesema wengi miongoni mwa wakimbizi walioko katika makambi ya muda wana hali mbaya kiafya na ni wadhaifu kutokana na kutembea kwa umbali mrefu.

Alisema wakimbizi hao wenye hali mbaya wanapatiwa huduma maalumu ikiwemo ya chakula ili kurejesha afya zao.

Hakuna wakimbizi wapya kutoka Angola wanaoingia katika makambi ya Sinjembele nchini Zambia kama ilivyokuwa awali kwa mujibu wa Shimo.

Mahakama yakataa kutambua kesi ya mlevi aliyemgonga mjamzito, kuua mtoto

lYasema mtoto si mtu hadi atoke tumboni na apumue

MWANAUME mmoja dereva aliyedaharau taa nyekundu za barabarani kwa kupitiliza akiwa amelewa na kumuua mjamzito baada ya kumgonga ameachiwa huru.

Tukio hilo lililotokea hivi karibuni nchini Uingereza na kuripotiwa na gazeti moja la nchi hiyo The Times limeeleza.

Kwa mujibu wa habari hizo mhusika amehukumiwa kifungo cha nje cha saa 120 tu..

Mahakama ya North Avon nchini Uingereza (UK) ilishauri kwamba licha ya kwamba mtoto aliyekuwa tumboni mwa mama yake alifariki, lakini dereva huyo hawezi kushitakiwa kwa kuua kwa vile sheria za nchi hiyo zinamtambua mtoto pale tu anapozaliwa na kuvuta pumzi yake ya kwanza.

"So the child’s death could not be taken a

saseparate offence". alisema Hakimu akimaanisha kuwa suala la kifo cha mtoto haliwezi kuchukuliwa kama shitaka tofauti.

Kulingana na maumbile na mafundisho ya Kanisa mtoto ana haki ya kutambuliwa tangu pale mimba inapotungwa. Kwa baadhi ya nchi kama vile Tanzania mtoto hutambuliwa kama raia anapokuwa katika umri wa miezi saba, na katika umri huo akifariki tumboni mwa mama yake anastahili kutolewa na kuzikwa peke yake.

Kardinali amtumia majivu Askofu Mlutheri

Los Angeles

KIONGOZI mmoja wa Kanisa Katoliki Kardinali Roger Mohany amemtumia majivu Askofu wa Kilutheri Paul Egerton ikiwa ni ishara ya kuungana katika kipindi hiki cha Kwaresma katika kuyatafakari mateso ya Bwana Yesu Kristo.

Viongozi hao wawili wa Makanisa walifanya tukio hilo siku ya Jumatano ya Majivu mnamo Machi 8 mwaka huu katika Chuo Kikuu cha Calfonia Kusini mjini Los Angeles.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la CNS viongozi hao waliunganishwa na Askofu Fredrick Borsch