Biashara ya kuhifadhi maiti yavamiwa Afrika Kusini

JOHANESBURG, Afrika Kusini

Biashara ya kuhifadhi maiti katika jimbo la Guorten inasemeakana kuwa katika hali mbaya kutokana na kuvamiwa na wafanyabiashara wasiotambulika.

Inasemekana hali hiyo imesebabishwa na watu binafsi kujenga vyumba vya kuhifadhi maiti na kufanya kazi hiyo bila uthibitisho.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti moja la nchi hiyo, "The Star" ambalo hufanya shughuli zake mjini Johanesburg, umeonesha kwamba kuna maiti zinazozagaa katika mabanda zinamo hifadhiwa.

Aidha, kuna kambi zinazofanya kazi za kuhifadhi maiti bila kutambulika na mamlaka ya nchi hiyo.

Gazeti lachini Afrika Kusini ni kawaida pengine kukuta maiti zimezagaa majalalani limelipoti gazeti la the star.

Kuhusiana na hali hiyo, polisi nchini afrika kusini itafanya uchunguzi kuhusu biashara ya kuhifadhi maiti inayofanywa na watu binafsi nchini humo.

Papa ataka kumalizwa kwa mapigano Indonesia

VATICAN CITY

KIONGOZI Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Yohane Paulo wa Pili, amerudia wito wake wa awali wa kutaka kumalizwa kwa mapigano katika Visiwa vya Molucca nchini indonesia ambako mapigano kati ya Waislamu na Wakristo yalizuka tangu Januari mwaka jana.

Akizungumza na maelfu ya waamini katika Wiwanja vya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatcan City, Baba Mtakatifu amelaani mashambulio hayo ya mabomu yaliyoua watu wanane na kuwajeruhi zaidi ya 90 nchini Urusi na kuua mtu mmoja nchini Hispania katikati ya juma.

Ameshutumu mashambulio ya mabomu yaliyofanywa nchini Urusi na Hispania.

Ameelezea masikitiko yake juu ya mauaji hayo na kurudia wito wake wa kuwataka Wakristo kufanya maombi kwa ajili ya kumalizika kwa ghasia hizo ambazi zinavuruga amani nchini Indonesia.

Marekani yakataa kusemea mtoto aliyeuawa na fisi Botswana

Gaborone, Botswana

UBALOZI wa Marekani nchini Botswana, umekataa katakata kutoa maoni au kali yoyote kuhusu kifo cha mtoto wa Kimarekani aliyeuawa na fisi katika mbuga za wanyama nchini Botswana.

Habari kutoka katika shirika moja la safari la Capricon, zinasema kutokana na Botswana kukosa mahali pa kuzikia, mtoto huyo wa miaka 11 ambaye alikuwa akiambatana na mama yake katika safariya kutembelea nchi za Botswana na Zimbabwe kwa muda wa majuma mawili yaliyopita, alizikwa nchini Afrika Kusini.

Habari zinasema mtoto huyo alishambuliwa na fisi katika mbuga za wanyama nchini Botswana katika safari hiyo na mama yake.