Make your own free website on Tripod.com

George Bush kugombea Urais

PHILIDELPHIA;Marekani

GAVANA wa Taxes,George Bush,ameteuliwa kuwa mgombea wa kiti cha Urais kwa tiketi ya chama cha Republican.

Uteuzi huo umekuja baada ya mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika hivi karibuni ,mijini Philadelphia.

Baada ya kuteuliwa kugombea nafasi hiyo,Bush amemteua Richard Cheney kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi huo utakaofanyika Novemba mwaka huu.

Mpinzani wa George Bush anatarajiwa kuwa Al Core wa chama cha Democrat ambaye atapitishwa mwezi ujao huko Los Angeles.

Banyamlenge waanzisha upya mapigano

Kinshasa,Congo

Mapigano mapya ya kikabila yameibuka upya nchini Congo ambapo mara hii yameanzishwa na kikundi cha Watutsi wanaojulikana kwa jina maarufu la Banyamlenge.

Mapigano hayo yameanza huku waasi wakisherekea mwaka wa pili tangu walipo anzisha uasi dhidi ya serikali ya Rais Laurent Kabila.

Mapigano hayo inaelezwa zaidi kuwa yatawaathiri zaidi wananchi.

Habari ambazo Shirika la Habari la Utangazaji la Uingereza lilizipata,zinasema kuwa Watutsi 37 waliuwawa hivi karibuni katika kijiji kimoja nchini humo na wengine kuchomwa moto wakiwa hai majumbani mwao.

Makundi ya haki za binadamu yameeleza kuwa si waasi wala serikali wanaoweza kutamba kuwa wamefanikiwa.

Vile vile Mashirika ya misaada yameonya kuwa miezi ijayo kutakuwa na uhalifu mkubwa dhidi ya binadamu Mashariki mwa Congo ,huku maeneo mengi yakishindwa hata kupata misaada kutoka nje.

Wakulimwa wa Kizungu watiwa moyo

Harare;Zimbabwe

WAKULIMA wa Kizungu nchini Zimbabwe wametiwa moyo kwa kuambiwa kuwa hatima ya tatizo la mashamba yao yaliyochukuliwa na wapiganaji wa zamani wa nchi hiyo,litapatiwa ufumbuzi mwishoni mwa mwezi huu.

Kauli hiyo ya matumaini kwa wazungu hao imetolewa na Rais wa nchi hiyo,Rais Robart Mugabe.

Rais Mugabe alitoa kauli hiyo baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Afrika ya Kusini ,Thabo Mbeki,mazungumzo ambayo yalichukuwa zaidi ya masaa matano.