Michezo

Simba haipati kitu kwetu ng'o - Mtibwa

Na Gerald Kamia, Morogoro

Timu ya soka Mtibwa Sugar ya Turiani Morogoro, imesema kuwa klabu ya Simba haina ubavu wa kumnyakuwa mchezaji hata mmoja toka klabu hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mwishoni mwa juma mjini hapa, Kocha wa timu hiyo, John Simkoko, alisema kuwa, ni ndoto na wala timu hiyo ya Simba isitegemee kupata mchezaji kutoka katika timu hiyo ya Mtibwa kwa kuwa wachezaji wake tayari wamekwisha jigundulia siri yao.

Kocha huyo amesema kuwa wachezaji hao wa timu ya Mtibwa, wamejifunza mengi kutokana na vilabu vya Simba na Yanga ambavyo haviishi migogoro na kudai kuwa, timu hizi zilikuwa kwa kiwango kikubwa, zikichangia kuua viwango vya wachezaji hapa nchini.

Kocha huyo ameongeza kusema kuwa, kama ni ubingwa, basi timu yake ndiyo bingwa wa Ligi Kuu na wachezaji wanapewa fungu lao ipasavyo sasa, huko Simba wakafuate nini, au kwenda kuua viwango vyao vya soka?

Kauli ya kocha huyo, inafuatia kauli ya Kamati ya Simba iliyokaaa hivi karibuni na kupendekeza jumla ya wachezaji saba watakaosajiliwa na timu hiyo msimu ujao wakiwamo majina ya wanandinga kutoka timu ya Mtibwa ambao ni Zuberi Katela, Kassimu Issa na Dua Said.

Shungu: Usisajili walevi Yanga

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Kocha mkuu wa klabu ya soka ya Yanga ya jijini Dar-Es-Salaam, Roul Shungu, ametakiwa kusajili wachezaji wasio walevi na na wenye uwezo mkubwa katika kusakata kabumbu katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Safari Lager.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, baadhi ya wanachama na wapenzi wa timu hiyo wa mjini Morogoro, wamesema kuwa ulinzi wa timu hiyo umekuwa hauridhishi kutokana na kuwa na wachezaji walevi pamoja na wale wasio kuwa na uwezo mkubwa wa kusakata kabumbu.

Wanachama hao, wamemtaka kocha huyo Roul Shungu ambaye ni raia wa Kongo kuwa makini katika usajili wake ili kuhakikisha timu hiyo inakuwa na uhakika inaposhiriki katika michuano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

Wamemtaka kocha huyo atilie mkazo zaidi katika safu ya ulinzi wa timu hiyo ambayo imedaiwa kuwa ni mbaya sana.

Wanachama hao wamesema udhaifu wa ngome yao, ndio sababu kuu iliyopelekea timu hiyo kukosa ubingwa wa Tanzania Bara msimu uliopita.

Tanzania yasifiwa kwenye Olimpiki lakini ..Mhhh!

Na Modesti Msangi

TIMU ya Tanzania inayoshiriki michezo ya Olimpiki huko Sydney Australia, imesifiwa kuwa miongoni mwa timu nzuri kutoka barani Afrika lakini, huenda haitafanya vizuri kutokana na maandalizi duni yanayotokana na serikali kutotilia mkazo sekta ya michezo

Kwa mujibu wa televisheni moja ya Afrika Kusini inayoonesha mashindano hayo moja kwa moja toka Sydney, wakati wa ufunguzi, ilisema Tanzania inao wanariadha wazuri na wenye uwezo wa kushindana na wakashinda lakini, hali halisi inaonesha kuwa hawapati maandalizi ya kutosha na hiyo inafanya matumaini ya kupata medali za dhahabu kuwa finyu mno.

Televisheni hiyo ilisema hali hii inatokana na Tanzania kuwana sera mbovu katika michezo na si tu kwa riadha, bali kwa karibu michezo yote na kwamba ndiyo maana Tanzania imekuwa msindikizaji wa katika michuano mingi ya kimataiafa.

Ilisema nchi kama Ethiopia na Kenya ni miongoni mwa nchi za Afrika zenye wanariadha bora na ikadokeza kuwa huenda Kenya ikachukua nafasi itakayoachwa na Tanzania katika michuano hiyo kwa kuwa inaonekana kufanya vizuri kuliko Tanzania.

Televisheni hiyo ilidokeza kuwa sababu kubwa ya Tanzania kufanya vibaya katika mashindano mengi ya kimataifa, ni kutumia fedha zake nyingi katika kuhudumia wakimbizi badala ya kuziwekeza katika sekta ya michezo ili kuinua kiwango.

Ilisema kama Tanzania ingewaandaa vizuri wanariadha wake, ingejizolea medali nyingi za dhahabu na ikaongeza kuwa ubinafsi wa viongozi wa michezo ni moja ya sababu nyingine zinazodumaza michezo nchini.

Katika michezo hiyo ya Olimpiki inayofanyika nchini Australia, Tanzania inawakilishwa na wachezaji 4 wa riadha na viongozi 13 huku mwanariadha, mwanadada Lwiza John, akiwa ameondolewa na Kamati ya Olimpiki ya Taifa kwa madai kuwa hana viwango vinavyohitajika.

Yeye mwenyewe Lwiza, alidai kuwa na kiwango hicho na alithibitisha kuwa na uwezo huo baada ya kushiriki mashindano ya riadha ya wazi huko Ulaya.

Katika mashindano hayo, Lwiza alimaliza akiwa wa pili nyuma ya bingwa wa mbio za Meta 800 wa Olimpiki ya mwaka 1996 huko Atlanta Marekani na hivyo, kujipatia nafasi ya kushiriki mashindano ya dhahabu yaliyowashirikisha mabingwa wa riadha hasa katika mashindano yanayofanyika Ulaya.

Lwiza John ni Mtanzania wa kwanza kupata tiketi ya kushiriki mashindano hayo ya dhahabu na kwa hivi sasa, yupo huko Sydney Australia kama mtazamaji wa mashindano hayo ya Olimpiki mwaka huu.

Ratiba 'inaibeba' Mtibwa - Shungu

Na Gerald Kamia, Morogoro

WAKATI michuanao ya Ligi Kuu ya Muungano inaanza Jumatano hii, timu ya soka ya Yanga imekumbwa na mchecheto mkubwa na kudai kuwa ratiba hiyo, inaibeba timu ya soka ya Mtibwa ya mjini hapa.

Akizungumza na KIONGOZI mjini hapa, mwishoni mwa juma, Kocha Mkuu wa timu hiyo Roul Shungu, amedai kuwa kitendo cha FAT kupanga pambano la timu ya Yanga na Mtibwa lianze jijini Dar-Es-Salaam badala ya Morogoro, ni njama za kuibeba makusudi timu ya Mtibwa.

Shungu amesema mara nyingi FAT imekuwa ikipanga mechi baina ya timu hizo, ianzie Dar-Es-salaam badala ya Morogoro ili kuipa fursa timu ya Mtibwa kutumia uzalendo katika mchezo wa marudio ambao hufanyika Morogoro.

Kocha huyo wa Yanga amesema hali hiyo inawatia wasiwasi na kuiweka timu hiyo katika hali ya tahadhari wakati ligi hiyo itakapoanza Jumatano.

Hata hivyo, Kocha Mkuu wa Mtibwa, John Simkoko, amedai kuwa huo ni mchecheto tu, wa timu ya Yanga hasa baada ya kuchapwa 2-1 katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Safari Lager uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini hapa.

Kocha huyo amesema timu yake iko tayari kufanyia mchezo huo mahali popote utakapopangwa, pawe Dar-Es-Salaam au Morogoro kwa kuwa, inao uhakika wa kuibuka na ushindi kwa mara nyingine tena.

MASHINDANO YA KIMATAIFA YA MPIRA WA WAVU KOMBE LA BONITE:

Tanzania yawa uchochoro wa kupenyea

Na Mwandishi Wetu

Kushindwa kushiriki kwa tiku za Metro na Jeshi Stars, kwenye mashindano ya kimataifa ya wazi ya mpira wa wavu Kombe la Bonite, kumeifanya Tanzania kuwa uchochoro wa kupitisha timu za nje.

Wakati kiongozi wa Metro ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Wavu nchini(TAVA), Adam Gwao, amesma timu yake haikushiriki mashindano hayo ya 13 ya michezo hiyo ya kila mwaka kwa kukosa fedha, wapinzani wao wakubwa, Jeshi Stars, wameshindwa kushiriki mashindano hayo kutokana na sababu ambazo hazikuelezwa bayana.

Mratibu wa mashindano hayo Filbert Uwisso, aliliambia gazeti hili katikati ya wiki kuwa, alipokea taarifa kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)ambalo ni mmiliki wa Jeshi Stars kuwa timu hiyo haingeshiriki mashindno hayo kutokana na sababu zisizozuilika.

Alidokeza kuwa sababu mojawapo ni kutokuelewa kati ya uongozi wa timu na uongozi wa JWTZ.

Timu ya Jeshi Stars inafundishwa na Kocha Yusuf Mkalambati ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Makocha ya TAVA.

Mwaka jana timu yake ilicheza fainali na timu ya General Motors ya Kenya ambayo ni bingwa wa kombe hilo kwa miaka mitatu mfululizo iliyopita. General Motors ilishinda kwa seti 3-2

Kushindwa kushiriki kwa timu hizi vinara wa mchezo huu nchini, kumekuwa mteremko kwa timu za nje zinazoshiriki mashindano hayo.

Timu kutoka Kenya zinazoshiriki ni saba ambazo ni, bingwa mtetezi wa wanaume, General Motors, Chuo Kikuuu cha Nairobi-wanawake na wanaume, Nairobi Mchanganyiko- wanawake na wanaume.

Nyingine ni Kenya Commercial Bank (KCB)- wanawake na wanaume ambao ni mabingwa wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, na STIMA- wanaume.

Kutoka uganda ni Kampala, Amacha Volleybal Club (KAVC)-wanawake na wanaume, Kampala City Council, ya wamanawake.

Nyingine ni timu ya Visiwi ya Old Kampala (OKD) ya wanaume, Sekondari ya Manyasi -wasichana

Kutoka Malawi ni Lilongwe Stayker - wanaume inayoshiriki michezo hiyo kwa mara ya kwanza.

Ukilinganisha timu hizo za nje ya nchi , ni dhahiri kuwa timu za Tanzania, zina nafasi finyu ya kuingia nusu fainali.

Wapenzi wa mchezo huo, wanatazamia kuona bingwa mpya wa mashindano hayo baada ya kushiriki timu ya KCB ambayo ni kinara wa mchezo huo nchini Kenya. Wanategemea kuona mvutano mkali kati ya Generel Motors, KCB, KAVC, na timu ya STIMA zinazotarajiwa kupeana upinzani mkali.

Nairobi Mchanganyiko, KAVC na KCC kwa upande wa wasichana, zitaoneshana moto katika kuwania kucheza fainali ya mashindano hayo.

Mashindano hayo ya Kombe la Bonite Bottlers, yamesaidia kwa kiasi fulani kuinua kiwango cha mpira wa wavu nchini kwa kuzialika timu toka mataifa jirani kuja kuopambana na timu za nchini.

Jitihada zaidi bado zinahitajika ili kukisaidia TAVA kudhanini timu nyingi zaidi ili ziweze kushindana na kuzipz uzoefu timu za nyumbani kwa ajili ya kushiriki mashindano ya kimataifa.

Mashindano hayo yanatarajiwa kufungwa Jumamosi hii na Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Shwaibu Mwiyunga katika viwanja vya Hindru Mandar, Moshi

WAWATA wafanyia maonesho nyumba ya Makumbusho

Na Dalphina Rubyema

CHAMA cha Kitume cha Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA)ngazi ya Taifa, Jumamosi hii wanafanya maonesho mbalimbali ya sanaa kwenye nyumba ya Makumbusho jijini Dar-es-Salaam ambapo mgeni rasmi atakuwa ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto, Marry Nagu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa WAWATA Taifa, Bibi Oliva Luena, ni moja ya shamrashamra za kusherekea Jubile Kuu na Mwaka Mtakatifu.

Alisema WAWATA kutoka majimbo yote ya Kanisa Katoliki watahudhuria maonesho hayo na Jimbo ambalo litaibuka mshindi, litajinyakulia zawadi ya kombe la Milenia.

Alivitaji vigezo vitakavyotumika kumpata mshindi huyo kuwa ni pamoja na kuangalia ubunifu wa sanaa zitakazooneshwa rasilimali asilia ya eneo husika na jinsi ilivyotumika kutengeneza bidhaa hizo za maonesho pamoja na mwonekano na ubora wa bidhaa zenyewe.

"WAWATA pamoja na kuwa na malengo mengine, vile vile ina lengo la kumwendeleza mwanamke kiroho na kimwili, hivyo kigezo kingine kitakachotumika kumpa mshindi ni kuangalia jinsi anavyo lizingatia suala hilo" alisema Bibi Luena.

Alisema majaji katika maonesho hayo yatatoka katika Shirika lisilo la Kiserikali nchini linaloshughulika na masuala ya uhamasishaji ,kuendeleza na kutafuta masoko ya biashara kwa wazalishaji wadogo linalojulikana kama AMKA.